Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
27 Oktoba 2020 06:43:25
Dawa ya Oxytetracycline
Oxytetracycline ni aina ya dawa mojawapo ya antibayotiki jamii ya tetracycline ambayo hutumika kupambana na Maambukizi mbalimbali kwenye mwili.Dawa hii huwa maarufu kwa jina la terramycin.
Dawa hii huathiriwa endapo itatumika pamoja na chakula na maziwa ,Hivyo ni vyema kutumia saa 1 kabla ya kula au baada ya kula
Chlortetracycline hupatikana katika mfumo wa kidonge katika uzito wa;
250 Mg
300 Mg
Namna dawa inavyofanya kazi
Dawa jamii ya Tetracycline ikiwa pamoja na Oxytetracycline hufanya kazi Ifuatayo kupambana na bakteria
Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa protini kwenye bakteria
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Tetracycline) na dawa hii ni ;
Tetracycline
Clortetracycline
Demexlocycline
Doxycycline
Minocycline
Methacyxline
Rolitetracyxline
Kazi ya dawa:
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi yanayosababishwa na bakteria aina ya Claymdia
Hutumika kutibu Pneumonia inayosababishwa na bakteria aina ya mycoplasma
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (Tetracycline)
Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya kinyesi kwa asilimia kubwa zaidi kuliko njia zingine
Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa 6 hadi 8 tangu itumike mwilini
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Acitretin
Flibanserin
Lomitapide
Tretinoin
flibanserin
lomitapide
tretinoin
Aluminum hydroxide
Aminolevulinic acid
Amoxicillin
Ampicillin
Apalutamide
Atracurium
Avapritinib
Axitinib
Bismuth subsalicylate
Bosutinib
Calcium acetate
Calcium carbonate
Calcium chloride
Calcium citrate
Calcium gluconate
Carbonyl iron
Cisatracurium
Cobimetinib
Dicloxacillin
Eliglustat
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za tetracycline
Wagonjwa wa ini
Tahadhari ya dawa hii
• Dozi yake inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii ipo kwenye kundi D la usalama kwa mama mjamzito
Dawa hii inaweza kutumika kwa mama mjamzito endapo hakuna dawa yeyote salama kwenye kipindi hiki
Inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
Kichefuchefu
Kutapika
Kuvimba mdomo
Maumivu kwenye sehemu ya juu ya tumbo
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-