top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

26 Oktoba 2020 13:41:59

Dawa ya Propiconazole

Dawa ya Propiconazole

Propiconazole ni antifangasi inayotumika kutibu magonjwa ya fangasi, dawa hii ipo katika kundi la dawa linaloitwa Triazole. Propiconazole huwa maarufu kwa jina jingine la DMI


Fomu na uzito wa dawa


Dawa hii hupatikana katika mfumo wa mafuta ya krimu yenye asilimia 41 ya kiini cha dawa


Dawa zilizo kundi moja na Propiconazole


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;


 • Efinaconazole

 • Epoxiconazole

 • Isavuconazole

 • Itraconazole

 • Posaconazole

 • Albaconazole

 • Ravuconazole

 • Terconazole

 • Voriconazole


Namna Propiconazole inavyofanya kazi


Dawa hii hufanya kazi zake kwa kuingilia kimeng’enya kinachoitwa saitokromu P-450 ambayo ni muhimu kwa ubadilishaji wa lanosteroli kwenda ergosteroli. Hii inasababisha kupunguza utengenezaji wa ergosteroli na kuongeza upenyezaji wa seli ya fangasi kwasababu ya upunguaji wa kiasi cha ergosteroli ambacho huwa muhimu kwenye utengenezaji wa ukuta wa seli ya fangasi.


Kazi ya Propiconazole


Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi ya mwili mzima


Dawa zisizopaswa kutumika pamoja na Propiconazole


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:


 • Alfuzosin

 • Alprazolam

 • Cobimetinib

 • Conivaptan

 • Dihydroergotamine

 • Dihydroergotamine intranasal

 • Disopyramide

 • Dronedarone

 • Eliglustat

 • Flibanserin

 • Ibutilide


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Propiconazole


Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi


Matumizi ya Propiconazole kwa mama mjamzito


Dawa hii bado haijapewa kundi la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito;


Dawa hii inaweza kutumika endapo itahitajika sana kwa mama mjamzito bila kuwepo kwa dawa nyingine mbadala


Matumizi ya Propiconazole kwa mama anayenyonyesha


Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari

Maudhi ya Propiconazole


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na;


 • Kutapika

 • Maumivu ya tumbo na kichwa

 • Kizunguzungu

 • Kuharisha

 • Mwili kuwa wa njano

 • Kuogopa mwanga


Endapo umesahau kunywa Propiconazole


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia a mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:54:56

Rejea za mada hii:-

1. Sciencedirect.Propiconazole.https://www.sciencedirect.com/topics/agricultural-and-biological-sciences/propiconazole. Imechukuliwa 13/10/2020

2. PubChem.Propiconazole.https://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/compound/Propiconazole. Imechukuliwa 13/10/2020

3. Cornell.Propiconazole.http://pmep.cce.cornell.edu/profiles/extoxnet/metiram-propoxur/propiconazole-ext.html. Imechukuliwa 13/10/2020

4. Domyown.Propiconazole.https://www.domyown.com/propiconazole-143-p-16567.html. Imechukuliwa 13/10/2020
bottom of page