Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Oktoba 2020 14:19:02
Dawa ya Tavaborole
Tavaborole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Kerydin
Fomu na uzito wa dawa
Tavaborole hupatikana katika mfumo wa maji wenye ujazo wa Miligramu 43.5 kwa mililita yenye kiini cha dawa kwa asilimia 0.5
Dawa hii hutumiwa kwa kupaka kwenye eneo lililoathiriwa nafangasi
Namna Tavaborole inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi zake kwa kuzuia Protini ya seli ya fangasi kutengenezwa kwa kuzuia kimeng’enya cha Aminoacyl-transfer ribonucleic acid (tRNA) Synthetase (AARS) kufanya kazi yake ya kuzalisha vijenzi vya kuta ya seli ya fangasi hivyo kufanya seli ya fangasi kuwa dhaifu na hatimaye kufa.
Dawa zilizo kundi moja na Tavaborole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:
Amphotericin B
Butoconazole
Capsofungin
Ciclopiro
Econazole
Flucytosine
Griseofulvin
Itraconazole
Miconazole
Naftifine hydrochloride
Nystatin
Oxiconazole nitrate
Sulconazole nitrate
Terbinifine
Terconazole
Tioconazole
Tolnaftate
Voriconazole
Kazi ya Tavaborole
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Tavaborole
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Matumizi ya Tavaborole kwa mama mjamzito
Dawa hii bado haijapewa kundi la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii inaweza kutumika endapo itahitajika sana kwa mama mjamzito bila kuwepo kwa dawa nyingine mbadala
Matumizi yaTavaborole kwa mama anayenyonyesha
Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari
Maudhi ya Tavaborole
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na :
Maumivu ya sindano
Kupata vipele
Ukisahau dozi ya Tavaborole
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-