top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

27 Oktoba 2020 07:01:00

Dawa ya Tetracycline

Dawa ya Tetracycline

Tetracycline ni aina ya dawa mojawapo ya antibayotiki ambayo hutumika kupambana na Maambukizi mbalimbali kwenye mwili.Dawa hii huwa maarufu kwa majina ya sumycin na Actisite.


Rangi ya dawa


Rangi ya dawa ni ya njano na nyeusi lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza


Muda wa dawa kufanya kazi


Dawa hii hufanya kazi pale inaponyewa Saa 1 au masaa 2 baada ya kula Hakikisha unakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa


Fomu ya dawa


Tetracycline hupatikana katika mfumo wa kidonge na tembe wenye uzito wa milligramu zifuatazo:


250 mg

500 mg



Namna dawa inavyofanya kazi


Dawa jamii ya Tetracycline ikiwa pamoja na tetracycline hufanya kazi Ifuatayo kupambana na bakteria

Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa protini kwenye bakteria


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Tetracycline) na dawa hii ni ;


  • Choltetracycline

  • Oxytetracycline

  • Demexlocycline

  • Doxycycline

  • Minocycline

  • Methacyxline

  • Rolitetracyxline


Kazi ya dawa


Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wa Bronchitis ya muda mrefu

Hutumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa brucellosis


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (Tetracycline)


Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo kwa asilimia kubwa zaidi kuliko njia zingine.

Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa 8 hadi 11 tangu itumike mwilini


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na Tetracycline


Usitumie dawa hii pamoja na; zifuatazo;


  • Acitretin

  • Flibanserin

  • Lomitapide

  • Tretinoin

  • flibanserin

  • lomitapide

  • tretinoin

  • Aluminum hydroxide

  • Aminolevulinic acid

  • Amoxicillin

  • Ampicillin

  • Apalutamide

  • Atracurium

  • Avapritinib

  • Axitinib

  • Bismuth subsalicylate

  • Bosutinib

  • Calcium acetate

  • Calcium carbonate

  • Calcium chloride

  • Calcium citrate

  • Calcium gluconate

  • Carbonyl iron

  • Cisatracurium

  • Cobimetinib

  • Dicloxacillin

  • Eliglustat


Wagonjwa wasiopaswa kutumia dawa hii


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao ;


Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za tetracycline

Wagonjwa wa ini

Na mama mjamzito kwenye miezi 6 ya mwishoni


Tahadhari ya dawa hii


Dozi yake inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo

Huweza kuharibu rangi ya meno kwa mtoto kuanzia kwenye miezi 6 ya mwisho ya mimba hadi miaka 8


Matumizi wwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Dawa hii ipo kwenye kundi D la usalama kwa mama mjamzito

Dawa hii inaweza kutumika kwenye miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito na baada ya hapohairuhusiwi kutumika

Inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa


Maudhi madogo ya Tetracycline


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;


  • Kizunguzungu

  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Kuvimba mdomo

  • Maumivu kwenye sehemu ya juu ya tumbo


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje ?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:54:56

Rejea za mada hii:-

1.British National Formula Written by British Medical Association and pharmaceutical Society ISBN: 978 0 85711 340 5 ukurasa wa 507

2.WebMd.Tetracycline.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-5919/tetracycline-oral/details. Imechukuliwa 21/10/2020

3.Drugs.Tetracycline.https://www.drugs.com/tetracycline.html. Imechukuliwa 21/10/2020

4.MedlinePlus.Tetracycline.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a682098.html. Imechukuliwa 21/10/2020
bottom of page