Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
9 Agosti 2020, 16:47:08
Dawa ya Tolnaftate
Tolnaftate ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyopo katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. Dawa hii huwa maarufu pia kwa majina ya tinactin na aftate. Rangi yake huwa ni nyeupe lakini hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza.
Fomu ya dawa Tolnaftate
Tolnaftate hupatikana kwenye fomu ya mafuta yenye asilimia 1 ya kiini cha dawa
Namna Tolnaftate inavyofanya kazi ili kutibu fangasi
Dawa ya tolnaftate ni aina ya dawa ambayo hufanya kazi kwa kufungamana na steroli (ergosteroli) kwenye seli ya fangasi. Kwa kufanya hivi hutengeneza matobo kwenye ukuta wa seli ya fangasi na kufanya ukuta wa seli kuwa na uzaifu ambapo hupelekea kuharibika kwa seli.
Dawa zilizo kundi sawa na Tolnaftate
Amphotericin B
Butoconazole
Capsofungin
Ciclopiro
Econazole
Flucytosine
Griseofulvin
Itraconazole
Miconazole
Naftifine hydrochloride
Oxiconazole nitrate
Sulconazole nitrate
Terbinifine
Terconazole
Tioconazole
Tolnaftate
Voriconazole
Kazi za Tolnaftate
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi mwilini kutokana na maradhi ya ngozi yanayosababishwa na Tinea Corporis na pedis
Fangasi kwenye miguu (athlete's)
Miwasho ya jock itch
Na mashilingi kichwani (maambukiziya ringworms)
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Tolnaftate
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Matumizi ya Tolnaftate kwa mama mjamzito
Dawa hii hushauriwa kutumika kwa hali ya hatari ambapo hamna dawa nyingne mbadala wakati wa kipindi cha ujauzito.Tafiti kwa wanyama zinaonyesha kuwa dawa hii inayo madhara madogo kulinganisha na tafiti za kwa binadamu zinazoonyesha kuwa hakuna madhara yeyote
Matumizi ya Tolnaftate kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari kwa mama anayenyonyesha.
Maudhi ya Tolnaftate
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na :
Kuwashwa ngozi
Je endapo utasahau dozi yako ya Tolnaftate ufanyaje ?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
​
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:27
Rejea za mada hii:-