top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

9 Mei 2020 17:51:54

Eplerenone

Eplerenone

Eplerenone ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Iliyo kwenye kundi la dawa linaloitwa Potasiamu sparing diuretic. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Inspra


Rangi ya dawa ni nyeupe na njano lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza


Hakikisha unakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa.

Eplerenone hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa milligramu zifuatazo:

• 25 mg

• 50 mg


Namna dawa inavyofanya kazi ili kupunguza shinikizo la damu


Dawa jamii ya Potassium Sparing Diuretic ikiwa pamoja na Eplerenone hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu ;


Hufanya kazi kwa kuzuia utendaji kazi wa homoni ya Aldosterone ambayo hufanya kazi ya kuthibiti kiasi cha sodiamu na maji kwenye damu. Kuzuia utendaji kazi wa homonihii husababisha kupotea kwa maji na chumvi mwilini hivyo kupunguza kiwango cha damu katika mishipa ya dam una shinikizo la damu ndani ya mishipa pia hupungua kutokana na kupungua kiwango cha maji. Dawa hii pia huzuia kupotea kwa kiwango cha potasiamu kwenye damu, hii ndo maana jinala kundi hili limeitwa potasiamu sparing duretics


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na dawa hii ni;


• Triamterene

• Amiloride

• Spironolactone


Kazi ya dawa


• Hutumika kushusha shinikizo la damu kwa wagonjwa wenye shinikizo la juu la damu


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili ni;


• Huwa na maudhi madogo madogo machache ukilinganisha na dawa zingine kwenye kundi hili


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;


• Amiloride

• Apalutamide

• Diltiazem

• Drospirenone

• Idelalisib

• Isoniazid

• Drospirenone

• Idelalisib

• Ketoconazole

• Lofexidine

• Potassium acid phosphate

• Potassium Chloride

• Spironolactone

• Triamterene

• Voxelotor


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao


• Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au zingine katika kundi lake

• Wagonjwa wenye haipakalemia

• Haipaswi kutolewa pamoja na dawa yeyote ya Potassium Sparing Diuretic

• Wagonjwa wenye figo iliyoferi na magonjwa sugu ya ini


Tahadhari ya dawa hii


• Dawa hii huweza kupelekea kupoteza kwa madini mwilini

• Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wenye matatizo ya ini na figo

• Hatari ya mgonjwa kupata haipakalemia


Kundi la dawa kipindi cha ujauzito

Dawa hii ipo kundi B la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito


Kwa mama mjamzito

Dawa hii inaweza kutumika kwa mama mjamzito sababu tafiti zilizofanyuka kwa wanyama zinaonyesha hakuna hatari yeyote kwenye ujauzito.


Kwa mama anayenyonyesha


Hakuna taarifa kuhusu dawa hii kuingia kwenye maziwa ya mama, lakini tafiti za wanyama zinaonyesha uwepo wa dawa hii kwenye maziwa ya panya hivyo inapaswa kutumika kwa tahadhari endapo faida ni nyingi kupita hatari kwa mtoto


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;


• Haipakalemia

• Kukosa hamu ya kula

• Kichwa kuuma

• Kichefuchefu

• Maumivu ya tumbo

• Kukohoa

• Kukohoa

• Kizunguzungu

• Kuchoka


Mengine yanayofanyika Mwilini


Dawa hii baada ya kutumiwa huanza kufanya kazi ndani ya saa 1 hadi 2 na kudumu kwenye damu kwa masaa 3 hadi 6. Mabaki ya dawa hutolewa kwa njia ya Mkojo kwa asilimia 67 na kinyesi kwa asilimia 32.


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:55

Rejea za mada hii:-

1.British National Formula Written by British Medical Association and pharmaceutical Society ISBN: 978 0 85711 340 5 ukurasa wa 190

2.DrugBank.Eplerenone.https://www.drugbank.ca/drugs/DB00700. Imechukuliwa 6/5/2020

3.Medscape.Eplerenone.https://reference.medscape.com/drug/inspra-eplerenone-342397. Imechukuliwa 6/5/2020

4.WebMd.Eplerenone.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-64218/eplerenone-oral/details. Imechukuliwa 6/5/2020

5.FDA. Eplerenone.https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2016/021437s013lbl.pdf. Imechukuliwa6/5/2020
bottom of page