top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

4 Mei 2020 21:09:33

Esomeprazole

Esomeprazole

Esomeprazole

Ni dawa iliyopo kwenye kundi la proton pump inhibita ambayo huzuia uzalishaji wa tindikali kutoka kwenye ukuta wa seli za tumbo na hivyo kutibu hali mbalimbali ambazo husababishwa na tindikali ya tumboni kama vile vidonda vya tumbo na kiungulia. Dawa hii inafanana kwa karibu na dawa nyingine ya kundi hili ambayo ni omeprazole.


Majina ya kibiashara

Nexium

Alenia

Esofag


Fomula ya kikemikali ya Esomeprazole

C17H19N3O3S


Jina la kisayansi (IUPAC)


6-methoxy-2-[(S)-(4-methoxy-3,5-dimethylpyridin-2-yl) methylsulfinyl]-1H-benzimidazole


Fomu na dozi


Inapatikana kama tembe za:


Miligramu 20

Miligramu 40


Inapatikana kama vidonge vya


Miligramu 20

Miligramu 40


Inapatikana katika dozi ya kuchoma kwa sindano;


Miligramu 20/kichupa(vial)

Miligramu 40/kichupa(vial)


Inapatiikana katika dozi ya kimiminika ya kumeza;


Miligramu 10

Miligramu 20

Miligramu 40


Kazi ya dawa Esomeprazole


Kutibu vidonda vya tumbo.

Kutibu vidonda vya tumbo vinavyo sababishwa na dawa zilizopo kwenye kundi la NSAID.

Huchanganywa na dawa nyingine kutokomeza bakteria wa Helicobacter pylori wanaochangia vidonda vya tumbo.

Kutibu ugonjwa wa unaotokana na uzalishwaji wa tindikali nyingi kupita kiasi tumboni (Zollinger-Ellison syndrome).

Hutumika kabla ya kutoa dawa ya usingizi ili kupunguza kuzalishwa kwa tindikali tumboni.

Kitibu ugonjwa wakucheuka. kiungulia kikali (ugonjwa wa gastroesofagio reflux)

Kutibu michubuko kwenye koo la chakula kutokana na tindikali.


Namna ya kutumia dawa Esomeprazole


Tumia kama ulivyo elekezwa na daktari wako.

Dozi yake hutegemea ugonjwa au hali inayotibiwa.

Kwa dawa iliyopo kwenye hali ya kimiminika tikisa vizuri kabla ya kutumia.

Soma maelekezo vizuri kabla ya kutumia.

Ni vizuri kumeza saa 1 kabla ya kula.


Jinsi esomeprazole inavyofanya kazi mwilini


Huzuia hatua za mwisho za uzalishaji wa tindikali (asidi) tumboni. Hili ni muhimu katika kutibu vidonda vya tumbo,kiungulia na hali zingine zinazo sababishwa tindikali ya tumboni.



Umetaboli wa esomeprazole


Hufyonzwa kutoka kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwenda kwenye damu kwa 89%-90%, ingawa kumezapamoja na chakula hupunguza ufyonzwaji hadi 33%-53%.

Huchakwatwa na mwili kwenye ini ili iweze kufanya kazi na kuondolewa sumu.

Muda wa kuanza kufanya kazi hutegemea sana aina ya tatizo linalo tibiwa.

Taka mwili za mabaki ya esomeprazole hutolewa kwa njia ya mkojo (80%) na kinyesi (20%)


Maudhi ya Esomeprazole

Maumivu ya kichwa

Kuharisha

Kichefuchefu

Maumivu ya tumbo

Kutapika

Kujamba

Kizunguzungu

Maumivu ya viungo

Homa kwa watoto.

Maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji kwa watoto.


Esomeprazole marufuku kwa wagonjwa wafuatao;


Wagonjwa wenye mzio na pantoprazole.

Mgonjwa anaetumia dawa zenye rilpivirine.


Tahadhari wakati wa kutumia esomeprazole.

Kuhara wakati wakutumia dawa ya esomeprazole kunaweza kusababishwa na bakteria clostridium difficile.

Kutumia dawa hii kila siku zaidi ya mara moja kwa muda mrefu kunaongeza uwezekano wa mifupa kuvunjika kwa urahisi.

Matumizi ya kila siku kwa muda mrefu kama zaidi ya miaka mitatu yaweza kusbabisha upungufu wa vitamini B-12 kwa kupunguza ufyonzwaji wa vitamini hizo.

Matumizi ya muda mrefu yanaweza kusababisha kiwango cha magnesium kwenye damu kushuka chini ya kiwango cha kawaida.

Matumizi ya zaidi ya mwaka yanaongeza atari ya polipsi kwenye tezi zilizo kwenye fandazi.

Inaweza leta ugonjwa wa kusambaa wa lupazi erithromatosasi


Muingiliano wa Esomeprazole na dawa nyingine


Esomeprazole hupunguza utendaji kazi wa dawa zifuatazo;


Ketoconazole

Itraconazole

Digoxin

Dawa za chumvi zenye madini ya chuma

Erlotinib

Dasatinib.

Esomeprazole isitolewe na atazanavir na nelfinavir ambazo hupunguza makali ya VVU kwani hupunguza uwezo wa dawa hizo kufanya kazi.

Dozi ya saquinavir inahitaji kupunguzwa pindi dawa hiyo ya kupunguza makali ya VVU inapotolewa na esomeprazole, kwani dozi yake ya kawaida huwa kubwa mwilini na inaweza kuleta mathara.

Epuka kutumia esomeprazole pamoja na clopidogrel kwani hupunguza uwezo wa clopidogrel kufanya kazi.

Epuka kutumia esomeprazole pamoja na St. John’s Wort au rifampin kwani hupunguza uwezo wa esomeprazole kufanya kazi.

Esomeprazole huongeza kiwango cha tacrolimus kwenye damu dawa hizo zikitumika kwa pamoja.

Esomeprazole ikitumiwa pamoja na digoxin huongeza nguvu ya digoxin hivyo mgonjwa anapaswa kuangaliwa kwa ukaribu.

Esomeprazole inawea kuongeza kiwango cha methotrexate kwenye damu kuongezeka ikiwa zikitumiwa pamoja.

Esomeprazole, clarithromycin, na amoxicillin zikitumika kwa pamoja huongeza uwezo wa clarithromycin kufanya kazi.

Kutumia esomeprazole, clarithromycin na dawa nyingine kunaweza kusababisha madhara na hivyo tahadhari inahitajika.


Matumizi ya Esomeprazole wakati wa ujauzito na kunyonyesha

Dawa itumike kwa tahadhari kama faida ya kutumia ni kubwa kuliko madhara; Majaribio kwa wanyama yanaonesha madhara na majaribio kwa binadamu hayajafanyika. Au majaribio kwa wanyama na kwa binadamu hayajafanyika.


Hivyo ni vizuri kuiepuka na kutumia dawa salama Zaidi ili kuepuka kumdhuru mtoto aliyeko tumboni.


Matumizi wakati wa kunyonyesha


Wakati wa kunyonyesha ni vyema kuepuka dawa hii kwani kuna uwezekano wa dawa hii kufika kwenye maziwa ya mama. Hakuna taarifa za kutosha juu ya madhara ya dawa hii kwa mtoto anenyonya na hivyo ni vyema kuiepuka.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:55

Rejea za mada hii:-

1.Goodman & Gilman’s The Pharmacological Basis of THERAPEUTICS twelfth edition ISBN: 978-0-07-176939-6 ukurasa wa 1311.

2.U.S. Food and Drug Administration:
https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2014/202342s002lbl.pdf imechukuliwa 03/04/2020.

3.Medscape: https://reference.medscape.com/drug/nexium-nexium-24hr-esomeprazole-341998#6 imechukuliwa 03/04/2020.

4.PubChem: https://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/compound/Esomeprazole imechukuliwa 03/04/2020.

5.FDA.Esomeprazole.https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2014/022101s014021957s017021153s050lbl.pdf. Imeandikwa 03.04.2020
bottom of page