Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
29 Aprili 2020 08:35:35
Exenatide
Exenatide ni dawa mojawapo ya kutibu ugonjwa wa kisukari aina ya pili iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Glucagon like peptide 1 Agonisti. Dawa hii huwa maarafu pia kwa jina la Byetta.
Hakikisha unachoma Sindano kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa, Sindano hii huchomwa kwenye mapaja, tumbo au sehemu ya juu ya mkono. Ni vyema kubadilisha eneo la kuchoma sindano kwenye ngozi ili kuepuka madhara ya kuchoma sehemu moja.
Sindano huchomwa mara mbili kwa siku. Mara ya kwanza ni ndani ya dakika 60 kabla ya chai au chakula cha asubuhi na jioni ni ndani ya dakika 60 kabla ya chakula cha jioni. Exenatide haipaswi kutumika pamoja na chakula sababu haitafanya kazi vizuri
Fomu na uzito
Exenatide hupatikana katika mfumo wa maji kwa ajili ya sindano katika uzito wa;
250mcg/mL
250mcg/mL
Ufanyaji kazi
Exenatide hufanya kazi kwa kuchochea kongosho kuzalisha homoni ya Insulin mara kiwango cha sukari kinapoongezeka kwenye damu.
Homoni ya Insulin husaidia seli za mwili kutumia na kuhifadhi sukari na hivyo kuiondoa kwenye dmau. Kufanya hivi kiwango cha sukari hupungua sana kwenye damu.
Dawa kundi moja
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na Exenatide ni;
Liraglutide
Taspoglutide
Lixisenatide
Semaglutide
Dulaglutide
Exenatide hutibu nini?
Exenatide hutumika kudhibiti kiasi cha sukari kwa Wagonjwa wa kisukari aina ya pili. Huweza kutumika yenyewe au kwa muunganiko pamoja na dawa jamii ya sulphonylurea au biguanide
Endapo kiwango cha usafishaji wa Creatinine mwilini ni chini ya kiasi cha mililita 30 kwa dakika, dawa hii isitumike.
Upekee wa Exenatide
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (GlP1 Inhibitor);
Sindano hii hutolewa mara mbili kwa siku tofauti na dawa zingine kwenye kundi hili
Haina nguvu sana ya kufanya kazi ukilinganisha na dawa zingine kwenye kundi hili
Matumizi ya Exenatide na dawa zingine
Dawa hii inapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu inapotumika na dawa zifuatazo;
Glimepiride
Fosinopril
Fosamprenavir
Fludrocortisone
Etonogestrel
Ethinylestradiol
Estropipate
Estradiol
Eprosartan
Enalapril
Drospirenone
Dexamethasone
Desogestrel
Darunavir
Cortisone
Clozapine
Cinnamon
Chlorthalidone
Chlorpropamide
Chlorothiazide
Captopril
Candesartan
Betamethasone
Benazepril
Bazedoxifene
Azilsartan
Asenapine
Aripiprazole
Acetaminophen
Acarbose
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Exenatide
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye aleji na dawa hiyo
Kama mgonjwa ana historia ya kupata saratani ya tezi ya thairoidi
Mwenye shida ya figo
Tahadhari ya Exenatide
Sio mbadala wa Insulin
Haipaswi kutumika kwa mtu mwenye kisukari aina ya kwanza
Huweza kupelekea kuvimba kwa kongosho
Huweza kupelekea figo kushindwa kufanya kazi
Huweza kupunguza uzito hasa kwa wazee
Matumizi ya Exenatide kwa mama mjamzito
Inapaswa kutumika kwa tahadhari endapo faida ni kubwa kuliko madhara kwa mtoto.
Hakuna taarifa za uwepo wa dawa hii kwenye maziwa ya mama wakati wa kunyonyesha
Matumizi ya Exenatide kwa mama anayenyonyesha
Katika tafiti za panya inaonyesha uwepo wa dawa hii kwenye maziwa ya panya aliyepewa dawa kwenye kipindi cha kunyonyesha hivyo dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama anayenyonyesha kama faida ni kubwa kuliko madhara kwa mtoto.
Maudhi ya Exenatide
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
Uvimbe kwenye sehemu iliyochomwa sindano
Kichefuchefu
Kutapika
Kuharisha
Choo kuwa kigumu
Maumivu ya kichwa
Kizunguzungu
Maumivu ya misuli
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kuchoma dozi yako tumia pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:34:59
Rejea za mada hii:-