Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
3 Mei 2020, 13:09:56
Lecarnidipine
Utangulizi
Lecarnidipine ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa kalisiamu cheneli bloka. Dawa hii iliyo maarufu kwa jina la zanidi mara nyingi huwa na rangi nyeupe lakini huweza kubadilika kutokana na aina ya kiwanda.
Dawa hii inapaswa inaweza kutumika Pamoja na au pasipo chakula
Hakikisha unakunywa kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi kamili.
Baada ya wiki mbili au zaidi tangu ulipoanza kutumia dawa shinikizo la damu litashuka na kuwa kawaida.
Lecarnidipine hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa;
• 10mg
• 20 mg
Namna dawa inavyofanya kazi ;
Hufanya kazi kwa kuzuia kalisiamu kuingia kwenye misuli na mishipa ya damu. Kalisiamu huwa na kazi ya kufanya misuli isinyae kwa nguvu, inapozuiwa na dawa hii mishipa ya damu hutanuka na kuongezeka kpenyo, matokeo yake ni kushuka kwa shinikizo la damu.
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na dawa hii ni;
• Felodipine
• Isradipine
• Nicardipine
• Nifedipine
• Levamlodipine
• Nimonidipine
• Nisoldipine
• Nitrendipine
Kazi za dawa
Hutumika kushusha shinikizo la damu kwa wagonjwa wenye presha
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili ni;
• Huchukua muda mrefu mpaka kuanza kufanya kazi
• Haipelekei kutanuka kwa kuta za moyo
• Mauzi yake madogo madogo huweza kuvumilika
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
• Rifampicin
• Ketoconazole,
• Itraconazole
• Erythromycin
• Clarithromycin
• Nefazodone
• Fluvoxamine
• Fluoxetine
• Sertraline
• Ritonavir
• Indinavir
• Amprenavir
• Saquinavir
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
• Wagonjwa wenye aleji na dawa hiyo
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari ni;
• Wagonjwa wenye moyo ulioferi
Kundi la dawa wakati wa ujauzito
Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito endapo faida ni nyingi kuzidi hatari kwa mtoto
Kwa mama anayenyonyesha tafiti za kwenye wanyama zinaonyesha uwepo wa dawa hii kwa panya anayenyonyesha hivyo inapaswa kutumika kwa tahadhari endapo faida zitazidi hatari kwa mtoto anayenyonya
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
• Kizunguzungu
• Kichefuchefu
• Kuwashwa mwili
• Maumivu ya tumbo
• Maumivu ya kichwa
• Kupata vipele kwenye Ngozi
• Misuli kukosa nguvu
• Miguu kuvimba
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako unapaswa kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:32:15
Rejea za mada hii:-