top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

29 Aprili 2020 08:18:38

Liraglutide

Liraglutide

Utangulizi


Liraglutide ni dawa mojawapo ya kutibu ugonjwa wa kisukari aina ya pili iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Glucagon like peptide 1 Agonisti. Dawa hii ni maarufu kwa jina la Victoza na Saxenda, inapaswa kutumika pamoja na chakula au mgonjwa anapaswa kula kabla ya kutumia dawa hii kama atavyoelekezwa na daktari.


Liraglutide hupatikana katika dozi zifuatazo :

• 18mg/3mL (Victoza)

• 18mg/3mL (Saxenda)


Namna dawa inavyofanya kazi;


Hufanya kazi kwa kuchochea kongosho kuzalisha homoni ya Insulin mara kiwango cha sukari kinapoongezeka kwenye damu.

Homoni ya Insulini husaidia seli za mwili kutumia na kuhifadhi sukari na hivyo kuiondoa kwenye dmau. Kufanya hivi kiwango cha sukari hupungua sana kwenye damu.


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja ni;


• Exenatide

• Taspoglutide

• Lixisenatide

• Semaglutide

• Dulaglutide


Kazi za dawa hii ni;


• Victoza pekee hutumika kudhibiti kiasi cha sukari kwa Wagonjwa wa kisukari aina ya pili

• Saxenda hutumika kwa watu Wenye uzito kupita kiasi ili kupunguza kiasi cha uzito, inapaswa kusimamishwa endapo haitaweza kupunguza asilimia 4 ya uzito wa mtu


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (GlP1 Inhibita):


• Dawa hii husaidia kupunguza uzito mwilini

• Sindano hii haiwezi kupelekea haipoglaisemia


Dawa hii inapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu inapotumika na dawa zifuatazo;


• Acarbose

• Aripiprazole

• Asenapine

• Atorvastatin

• Azilsartan

• Bazedoxifene

• Benazepril

• Betamethasone

• Candesartan

• Captopril

• Chlorothiazide

• Chlorpromazine

• Chlorpropamide

• Chlorthalidone

• Cinnamon

• Clozapine

• Cortisone

• Darunavir

• Desogestrel

• Dexamethasone

• Drospirenone

• Enalapril

• Eprosartan

• Estradiol

• Estropipate

• Ethinylestradiol

• Etonogestrel

• Fludrocortisone

• Fuphenazine

• Fosamprenavir

• Fosinopril

• Glimepiridine

• Glipizide

• Glyburide


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:


• Wagonjwa wenye mzio na dawa hii

• Kama mgonjwa ana historia ya kupata saratani ya tezi ya thairoid

• Mwenye shida ya figo


Tahadhari ya dawa hii;


• Sio mbadala wa Insulin

• Haipaswi kutumika kwa mtu mwenye kisukari cha aina ya kwanza

• Huweza kupelekea pankreataitizi

• Huweza kupelekea kuferi kwa figo

• Huweza kupunguza uzito hasa kwa wazee

• Huweza kupelekea kuwa tegemezi kwa dawa hizi

• Saxenda huweza kupelekea mawazo ya kujiua na kuongeza kasi ya mapigo ya moyo


Kundi la dawa wakati wa ujauzito


Shirika la dawa ulimwengu bado halijaweka dawa hii kwenye makundi ya dawa salama kipindi cha ujauzito


Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Victoza


Kutokana na tafiti za uzazi wa wanyama zinaonyesha uwepo wa hatari kwa kijusi wakati wa ujauzito


Kwenye mimba ya sungura Liraglutide ilipotolewa wakati wa utengenezwaji wa ogani iliweza kupunguza uzito wa kijusi na kuweza kupelekea hatari kubwa ya ulemavu.


Inapaswa kutumika endapo faida zitakuwa nyingi zaidi ya hatari kwa mtoto


Saxenda


Haipaswi kutumika wakati wa ujauzito sababu hupelekea kupunguza uzito na huweza kuathiri kijusi


Kwa mama anayenyonyesha hakuna taarifa za uwepo wa dawa kwenye maziwa ya mama

Tafiti za wanyama zinaonyesha uwepo wa dawa kwenye maziwa ya panya anayenyonyesha Hivyo inapaswa kutumika kwa tahadhari endapo faida ni kubwa kuliko madhara kwa mtoto.


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na;


Victoza


• Kichefuchefu

• Kuhara

• Kutapika

• Choo kuwa kigumu

• Kuhara

• Kuvimba sehemu iliyochomwa sindano


Saxenda


• Kichefuchefu

• Kushuka kwa sukari

• Choo kuwa kigumu

• Kutapika

• Maumivu ya kichwa

• Kupunguza hamu ya kula

• Kuchoka

• Kizunguzungu

• Maumivu ya tumbo

• Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kuchoma dozi yako ya sindano choma mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:30:30

Rejea za mada hii:-

1.British National Formula Written by British Medical Association and pharmaceutical Society ISBN: 978 0 85711 340 5 ukurasa wa 685

2.FDA. Victoza. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2017/022341s027lbl.pdf. Imechukuliwa 21.04.2020

3.Medscape.Liraglutide.https://reference.medscape.com/drug/victoza-saxenda-liraglutide-999449. Imechukuliwa 21/4/2020

4.MedlinePlus.Liraglutide.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a611003.html. Imechukuliwa 21/4/2020

5.Drugs.Liraglutide.https://www.drugs.com/mtm/liraglutide.html. Imechukuliwa 21/4/2020
bottom of page