top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

24 Aprili 2020, 09:36:06

Nadolol

Nadolol

Utangulizi


Nadolol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la dawa linaloitwa beta bloka. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Corgard.


Rangi yake huwa nyeupe au maziwa ila mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotenegeneza


Ufyonzwaji wa dawa


Asilimia 30 ya dawa hufyonzwa kwenye utumbo na kuingia kwenye mzunguko wa damu, kiwango cha juu kabisa kwenye damu hufikiwa ndani ya masaa 3-4 mara baada ya kunywa dawa. Unaweza kutumia dawa hii bila au pamoja na chakula.


Utofauti wa dawa hii na zingine kwenye kundi lake ni kuwa, huwa haifanyiwi metabolizimu kwenye ini hivyo hutolewa kwa njia ya mkojo kama ilivyo. Hata hivyo nusu maisha yake ni masaa 20 hadi 24 na baadae hutolewa na figo kwa njia ya mkojo.


Nadolol kutokana kuishi masaa 24, inatumika mara moja tu kwa siku.


Nadolol hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu;


•20mg

•40mg na

•80mg


Namna dawa inavyofanya kazi kupunguza shinikizo la damu la juu


Dawa jamii ya beta bloka ikiwa pamoja na Nadolol hufanya kazi zifuatvyo ili kupunguza shinikizo la damu;


Hufanya kazi kwa kuzuia ufanyaji kazi wa homoni epinefrini na kusisimuliwa kwa seli za beta adrenejik zilizo kwenye mishipa ya damu.


Kwa kufanya hivi hupunguza mapigo ya moyo kwenda kasi, shinikizo la damu na upunguza mzigo wa damu kwenye Moyo na kuruhusu mzunguko wa damu kuwa mzuri mwilini


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:


• Acebutolol (Sectral)

• Betaxolol (Kerlone)

• Bisoprolol (Zebeta, Ziac)

• Carteolol (Cartrol)

• Carvedilol (Coreg)

• Labetalol (Normodyne, Trandate)

• Metoprolol (Lopressor)

• Nebivolol (Bystolic)

• Penbutolol (Levatol)

• Pindolol (Visken)

• Propanolol (Inderal)

• Sotalol (Betapace)

• Timolol (Blocadren)


Kazi za hii dawa ni;


• Kutibu shinikizo la juu la damu

• Kutibu Anjina pektorisi

• Kutibu mayokadio infaksheni


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:


• Acebutolol

• Betaxolol

• Bisoprolol

• Carvedilol

• Celiprolol

• Clonidine

• Digoxin

• Diltiazem

• Esmolol

• Labetalol

• Lofexidine

• Metoprolol

• Nadolol

• Nebivolol

• Penbutolol

• Pindolol

• Propranolol

• Rivastigmine

• Saquinavir

• Sotalol

• Timolol

• Verapamil


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:


• Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au jamii ya dawa za Beta bloka


Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;


• Wagonjwa wenye haipathairodizim

• Wagonjwa wenye shida ya figo

• Wagonjwa wenye shida ya Ini

• Wagonjwa wenye shida ya Moyo kuferi

• Wagonjwa wenye umri mkubwa


Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Dawa hii ipo kwenye kundi C ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito


Matumizi wakati wa ujauzito


Dawa hii itumike wakati wa tahadhari ambapo hamna dawa nyingine ya mbadala ya kumpa mama mjamzito. Takwimu zinaonyesha kuwa kuna madhara ya kutumia hii dawa


Matumizi ya dawa wakati wa kunyonyesha


Dawa hii huingia kwenye maziwa ya mama anayenyonyesha, watoto wanaozaliwa na mama anayetumia dawa hii wana hatari ya kupata haipoglaisemia na hupelekea mapigo ya moyo kuwa chini. Hivyo itumike kwa uangalifu


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;


• Kizunguzungu

• Kukosa usingizi

• Haipotesheni

• Choo kigumu

• Kuharisha

• Kichefuchefu

• Kikohozi kikavu

• Mwili kuchoka


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mra pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021, 11:28:46

Rejea za mada hii:-

1. Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasa wa 213-2014

2. FDA. Nadolol.https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2008/018063s060lbl.pdf. Imechukuliwa 23.04.2020

3. Drugs.Nadolol.https://www.drugs.com/mtm/nadolol.html. Imechukuliwa 23/4/2020

4. Medscape.Nadolol.https://reference.medscape.com/drug/corgard-nadolol-342361. Imechukuliwa 23/4/2020

5. WebMd.Nadolol.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-11755/nadolol-oral/details. Imechukuliwa 23/4/2020

6. MedicinePlus.Nadolol.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a682666.html. Imechukuliwa 23/4/2020
bottom of page