top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

31 Mei 2020 16:23:13

Nebivolol

Nebivolol

Utangulizi


Nebivolol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa beta bloka. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Bystolic na hupatikana katika mfumo wa kidonge.


Nebivolol hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa;


• 2.5mg

• 5mg

• 10mg na

• 20mg


Namna dawa inavyofanya kazi kupunguza shinikizo la damu.


Dawa jamii ya beta bloka ikiwa pamoja na Nebivolol hufanya kazi zifuatvyo ili kupunguza shinikizo la damu;


Hufanya kazi kwa kuzuia matendo yanayosababisha mapigo ya moyo kwenda kasi kwa kupinga utendji kazi wa seli za beta adrenorisepta.


Matendo ya Nebivolol kwenye seli za alfa 1 adrenejik risepta hufanya misuli ya damu kulainika, hivyo hupelekea kupungua kwa upinzani wa mzunguko wa damu ndani ya mishipa ya damu. Matendo haya hupelekea kupungua kwa shinikizo la damu na hivyo kuruhusu mzunguko wa damu kuwa mzuri mwilini.


Nebivolol pia huzaniwa kupunguza matokeo ya renin kwenye figo ambayo huongeza shinikizo la damu kwenye mwili.


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;


• Acebutolol (Sectral)

• Betaxolol (Kerlone)

• Bisoprolol (Zebeta, Ziac)

• Carteolol (Cartrol)

• Carvedilol (Coreg)

• Labetalol (Normodyne, Trandate)

• Metoprolol (Lopressor)

• Nadolol (Cornard)

• Pindolol (Visken)

• Propanolol (Inderal)

• Sotalol (Betapace)

• Timolol (Blocadren)


Kazi za dawa


Hutumika kushusha shinikizo la damu kwa wagonjwa wenye ugonjwa wa shinikizo la damu la juu


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;


• Acebutolol

• Betaxolol

• Bisoprolol

• Carvedilol

• Celiprolol

• Clonidine

• Digoxin

• Diltiazem

• Esmolol

• Labetalol

• Lofexidine

• Metoprolol

• Nadolol

• Penbutolol

• Pindolol

• Propranolol

• Rivastigmine

• Saquinavir

• Sotalol

• Timolol

• Verapamil


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;• Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Beta bloka


Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;


• Wagonjwa wenye haipathairodizim

• Wagonjwa wenye shida ya Moyo kuferi

• Wagonjwa wenye umri mkubwa


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili;


• Dawa hii haiathiriwi na chakula

• Mabaki ya dawa hii hutolewa mwilini asilimia 67 kupitia mkojo na asilimia 13 kupitia kinyesi

• Nusu ya maisha Dawa hii ya Nebivolol huwa ni masaa 12


Kundi la dawa kipindi cha ujauzito


Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito


Matumizi kwa mama mjamzito


Dawa hii itumike wakati wa tahadhari ambapo amna dawa nyingine ya mbadala ya kummpa mama mjamzito.


Matumizi kwa mama anayenyonyesha


Dawa hii haijulikani kama inawezekana kuingia kwenye ya mama au la, hivyo inashauriwa isitumike kwa mama anaonyonyesha.


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;


• Kizunguzungu

• Kukosa usingizi

• Maumivu ya kichwa

• Kuharisha

• Kichefuchefu

• Mwili kuchoka


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:27

Rejea za mada hii:-

1.Drugs.Nebivolol.https://www.drugs.com/mtm/nebivolol.html. Imechukuliwa 23/4/2020

2.Medscape.Nebivolol.https://reference.medscape.com/drug/bystolic-nebivolol-342363. Imechukuliwa 23/4/2020

3.WebMd.Nebivolol.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-149866/nebivolol-oral/details. Imechukuliwa 23/4/2020

4.MedicinePlus.Nebivolol.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a608029.html. Imechukuliwa 23/4/2020

5.Clinical pharmacology and Therapeutics Written by James M Ritter ISBN 978-0-340-90046-8 ukurasa wa 190 na 214
bottom of page