Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
31 Machi 2020, 13:59:31
Potasiamu
Potasiamu ni moja ya madini muhimu mwilini, hufanya kazi nyingi ikiwa pamoja na kusafirisha umeme kwenye mishipa ya fahamu.
Madini haya hupatikana kwa wingi ndani ya seli kuliko nje. Ili seli, misuli na mishipa ya fahamu iweze kufanya kazi inahitaji madini haya ya potasiamu.
Mwili hudhibiti iwango cha madini kiwe kile kinachotakiwa ndani nan je ya seli,madini haya yakizidi husababisha dalili na tatizo la haipakalemia, na yakipungua husababisha dalili na tatizo la haipokalemia
Baadhi ya dalili zinazohusiana na kiwango kisicho sawia katika damu ni kama moyo kwenda ndivyo sivyo, uchovu wa misuli, uchovu mkali wa mwili, kichefuchefu, misuli kuuma na kubana, upumuaji wa shida, maumivu ya kifua kutokana na moyo, matatizo ya kumeng’enya chakula, ganzi na miguu kuwaka moto, na kubadilika kwa hali ya moyo.
Hata hivyo mwili huwez akutumia akiba yake ya potasiamu ili kuhakikisha kiwango kinakuwa sawia kwenye damu.
Baadhi ya vitu vinavyoweza kusababisha madini haya kutokuwa kwenye kiwango kinachotakiwa ni;
Kutapika
Magonjwa sugu ya figo
Matumizi makubwa ya dawa za kuharisha
Kutokwa na jasho sana
Matumizi makubwa ya pombe
Kuharisha
Diabetic ketoasidosisi
Matumizi ya dawa za duretiki
Upungufu wa madini ya foliki aside
Aldesteroinizimu ya awali
Baadhi ya matumizi ya dawa za antibayotiki
Endapo utashukiwa kuwa na kiwango kisicho kawaida cha madini ya potasiamu mwilini, daktari wako atakufanyia vipimo mbalimbali kisha kukupa tiba inayofaa.
Dawa zinazoongeza madini ya potasiamu mwilini
Aldactone. (spironolactone)
potassium chloride ER
Micro-K. potassium chloride ER
Epiklor.
Vyakula vyenye madini ya potasiamu kwa wingi mfano wake ni
Ndizi
Machungwa
Boga
Tunda la apikroti
Matunda ya kukaushwa kama tende na zabibu
Spinachi ya kupikwa
Brokoli iliyopikwa
Viazi
Uyoga
Kunde
Mimea jamii ya tango
Bilinganya
Mimea jamii ya mabogo
Mboga za kijani
Samaki aina kadhaa kama tuna,
Mbegu jamii ya kunde kama maharagwe na kunde
Korosho
Chumvi
Nyama
Wanyama jamii ya ndege
Mpunga wa brauni
Ngano
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:24:46
Rejea za mada hii:-