Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Sospeter M, MD
Dkt. Lugonda B, MD
Imeboreshwa:
2 Aprili 2026, 16:24:55

Septrin
Septrin ni jina la kibiashara la dawa inayojulikana kama co-trimoxazole. Dawa hii ni mchanganyiko wa dawa aina mbili ambazo ni sulfamethoxazole na trimethroprim.
Dawa hii hutumika katika matibabu ya magonjwa mbali mbali yanayosababishwa na bakteria, fangasi, protozoa. Pia hutumika kama kinga dhidi ya magonjwa nyemelezi kwa watu waishio ya Virusi vya Ukimwi.
Uzito wa septrin
Septrin hupatikana katika mfumo wa vidonge, dawa ya maji na sindano katika uzito ufuatao
Vidonge
Septrin 400 mg/80 mg (humaanisha sulfamethoxazole 400 mg na trimethroprim 80 mg)
Septrin 800 mg/160 mg (humaanisha sulfamethoxazole 800 mg na trimethroprim 160 mg)
Dawa ya maji
Septrin 200 mg/40 mg) 5 mls (yaani sulfamethoxazole 200 mg na trimethroprim 40 mg katika ujazo wa mlilita 5)
Sindano
Septrin (80 mg/16 mg) /ml (yaani sulfamethoxazole 80 mg na trimethroprim 16 mg katika ujazo wa mlilita)
Wapi unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu septrin
Soma zaidi kuhusu septrin; magonjwa inayotibu, maudhi yake na maelezo mengine kwenye mada inayohusu Co-trimoxazole
Majina mengine ya kibiashara ya septrin
Majina mengine yanayotumika katika makampuni ya kuzalisha dawa yanayomaanisha septrin ni kama ifuatavyo
Actrim
Bactrim
Bactrim DS
Septra
Septra DS
Cotrim
Cotrim DS
Sulfatrim
Sulfatrim DS
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:24:55
Rejea za mada hii:-
