Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
18 Aprili 2020 19:51:10
Sitagliptin
Sitagliptin ni dawa ya inayotumika katika tiba ya ugonjwa wa kisukari aina ya pili, ipo kwenye kundi la dawa linaloitwa dipeptidyl peptidase-4 (DPP-4) na hufahamika kwa jina jingine la januvia.
Dawa zilizo kundi moja na Sitagliptin
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na sitagliptin ni;
Saxagliptin
Alogliptin
Linagliptin
Vildagliptin
Ufanyaji kazi wa sitagliptin
Hufanya kazi kwa kuongeza kiasi cha homoni za kimetaboli zinazoitwa inkretin ambazo huthibiti kiwango cha glukosi kwenye damu kwa kuchochea kuzalishwa zaidi kwa homoni ya Insulin, hasa baada ya kula
Hupunguza kiasi cha sukari kinazalishwa na ini kisha kuingia kwenye damu.
Sitagliptin hutibu nini
Hutumika kwenye matibabu ya kisukari kwa wagonjwa wenye kisukari aina ya pili.
Mwingiliano wa Sitagliptin na dawa zingine
Sitagliptin haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Erdafitinib
Pombe na ethano
Lasmiditan
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Sitagliptin
Sitagliptin haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye mzio na dawa hii
Wagonjwa wa kisukari cha aina ya kwanza
Angalizo
Hatari kwa wagonjwa wa moyo, inapaswa kutumika kwa uangalifu
Itumike kwa tahadhari kwa mgonjwa wa figo
Huweza kusabababisha pankriataitizi
Matumizi ya Sitagliptin kwa mama mjamzito
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito
Matumizi ya Sitagliptin kwa mama anayenyonyesha
Hakuna athari zozote kwa mtoto ikitumika kwa mama anayenyonyesha.
Maudhi madogo ya Sitagliptin
Nasofarinjaitizi
Kuharisha
Maumivu ya kichwa
Kutoa haja kubwa ngumu-kosntipesheni
Idima
Kichefuchefu
Maumivu kwenye jointi
Maambukizi kwenye mfumo wa juu wa upumuaji
Je endapo umesahau dozi ya Sitagliptin ufanyeje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, Tumia dawa mara utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa dozi ingine umefika. Kama muda wa dozi ingine umefika ruka dozi hii uliyosahau na endelea kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:24:13
Rejea za mada hii:-