top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

2 Mei 2020 16:49:56

Telmisartan

Telmisartan

Telmisartan ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu jamii ya Angiotensini II risepta bloka (ARBs).


Majina ya kibiashara


Telmisartan hufahamika kw amajina mengine ya kibiashara kama Micardis


Matumizi ya Telmisartan na chakula


Telmisartan inapaswa kumezwa pamoja na chakula au pasipo chakula mara moja kwa siku kama utakavyoelekezwa na kushauriwa na Daktari


Hakikisha unakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa .Dozi utakayopewa itategemea hali yako ya kiafya na jinsi mwili unavyoitikia matibabu.


Kukusaidia kukumbuka dozi yako, tumia muda sawa wa kunywa dawa kila siku. Ni muhimu kuendelea kutumia dawa hii hata kama haujisikii kuumwa maana mara nyingi wagonjwa wa shinikizo la juu la damu huwa hawaonyeshi dalili za kuumwa.


Fomu na uzito wa Telmisartan


Telmisartan hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa;


 • 40mg

 • 80mg


Ufanyaji kazi wa Telmisartan


Dawa jamii ya ARBs ikiwa pamoja na Telmisartan hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu;

Hufanya kazi kwa kufunga risepta za Angiotensin II zijulikanazo kama AT1 Risepta, risepta za AT1 hupatikana kwenye moyo,mishipa ya damu na figo. Vipokezi hivi vinapofungwa hupelekea Kutanuka kwa mishipa ya damu na kuwa na kipenyo kikubwa na kupelekea kushuka kwa shinikizo la damu


Hupinga uzalishwaji wa homoni ya Aldosterone ambayo hutumika kuthibiti kiasi cha sodiamu na maji, Kiasi cha sodiamu kinapothibitiwa husababisha kupungua kwa shinikizo la damu kwa kuwa chumvi na maji mwilini hupungua.


Dawa kundi moja na Telmisartan


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Kundi la ARBs) na dawa hii ni ;


 • Candesartan

 • Olmesartan

 • Eprosartan

 • Irbesartan

 • Losartan

 • Azilsartan


Telmisartan hutibu nini


Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (ARBs)


Huweza kutumika kama mbadala wa dawa ya ACEIs katika kuthibiti magonjwa ya moyo

Hukaa na kufanya kazi kwa muda mrefu baada ya kutumiwa kulinganisha na dawa zingine kwenye kundi hili


Muingiliano wa Telmisartan na dawa zingine


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo :


 • Trandolapril

 • Ramipril

 • Quinapril

 • Potassium Phosphate IV

 • Perindopril

 • Moexipril

 • Lofexidine

 • Lithium

 • Lisinopril

 • Fosinopril

 • Enalapril

 • Captopril

 • Benazepril


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Telmisartan


Wagonjwa wenye aleji Telmisartan au dawa jamii ya ARBs pia haipaswi kutumika pamoja na dawa ya Aliskiren kwa wagonjwa wa kisukari


Angalizo


Telmisartan inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;


 • Wagonjwa wenye Haipakalemia

 • Wagonjwa wenye Haipotensheni

 • Wagonjwa wenye shida ya figo


Matumizi ya Telmisartan kwa mama mjamzito


Haipaswi kutumika wakati wa ujauzito, tumia endapo faida ni kubwa kuliko madhara. Dawa hii huwa na madhara kwa mtoto kama haipotension,figo kuferi na kifo


Matumizi ya Telmisartan kwa mama anayenyonyesha


Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu haijulikani kama huingia kwenye maziwa ya mama


Maudhi ya Telmisartan


Baadhi ya maudhi madogo ya Telmisartan ni;


 • Kichefuchefu

 • Kuharisha

 • Misuli kukaza

 • Kizunguzungu

 • Haipotension

 • Angioidima


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kutumia dozi yako ya Telmisartan tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana acha dozi uliyoisahau na kasha endelea na dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:22:51

Rejea za mada hii:-

1.Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasawa 157

2.WebMd.Telmisartan.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-16800/telmisartan-oral/details. Imechukuliwa 1/5/2020

3.MedScape.Telmisartan.https://reference.medscape.com/drug/micardis-telmisartan-342326.Imechukuliwa 1/5/2020

4.HealthLine.Telmisartan.https://www.healthline.com/health/telmisartan-oral-tablet. Imechukuliwa 1/5/2020

5.MedlinePlus.Telmisartan.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a601237. Imechukuliwa 1/5/2020

6.FDA. Telmisartan. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2011/020850s032lbl.pdf. Imechukuliwa 1.05.2020
bottom of page