Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. benjamin L, MD
16 Novemba 2021 17:28:24
Dalili za hatari baada ya kujifungua
Utangulizi
Mara baada ya kujifungua, kama mama atapata dalili zilizoelezwa kwenye Makala hii anapaswa kufika kituo cha afya karibu naye mara moja kwa huduma iwe mchana au usiku kwa kuwa dalili hizi huashiria kuwa hatarini hata kupotesha maisha kwa mama.
Dalili za hatari baada ya kujifungua
Dalili hizi zinapaswa kufahamika kwa mama na ndugu wanaoishi na mama aliyejifungua ili zitakapoonekana wamsaidie aweze pata msaada wa dharura katika kituo cha kutolea huduma za afya pasipo kusubiria. Dalili za hatari baada ya kujifugua ni pamoja na;
Kutokwa na damu nyingi ukeni, damu isiyokoma (kuloanisha zaidi ya pedi moja ndani ya dakika tano)
Mji wa mimba kutokuwa mgumu wala mviringo
Kupumua kwa shida au kuishiwa pumzi
Kupata homa na kuwa dhaifu kiasi cha kushindwa kutoka kitandani
Maumivu makali ya tumbo
Maumivu ya kichwa/kizunguzungu
Kupoteza fahamu
Degedege
Kifafa
Dalili zingine
Baada ya kujifungua, mama anapaswa kufika au kufikishwa kwenye kituo cha huduma za afya haraka iwezekanavyo ikiwa dalili zifuatazo zitajitokeza:
Kupata tabia isiyo ya kawaida kama msongo wa mawazo au kuchanganyikiwa
Maumivu makali katika via vya uzazi, ambayo huweza kusababishwa na kuvilia kwa damu katika mashavu ya uke au kuongezwa njia ya uke wakati wa kujifungua, kuchanika au michubuko
Kutokwa na majimaji yenye harufu mbaya ukeni baada ya kujifungua
Maumivu ya misuli ya nyuma ya mguu
Maumivu yatokanayo na kujaa/kuvimba kwa matiti
Kupata mkojo kidogo sana
Kutokupata mkojo kabisa
Kumbuka
Makala hii ya dalili za hatari baada ya kujifungua imejibu maswali pia kuhusu;
Dalili za hatari kwa mama aliyejifungua
Dalili za hatari kipindi cha puperiamu
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
16 Novemba 2021 17:28:24
Rejea za dawa
Postnatal care of the mother and newborn katika kitabu cha Counselling for Maternal and Newborn Health Care: A Handbook for Building Skills. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK304190/pdf/Bookshelf_NBK304190.pdf. Imechukuliwa 16.11.2021