top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Sospeter B, MD

21 Julai 2023 13:33:35

Image-empty-state.png

Dalili za uchungu wiki ya 34

Wiki ya 34 ya ujauzito umbaji wa viungo vya mtoto unakuwa umekamilika na ukuaji wa unaendelea. Uzito wake inakadiliwa kuwa kilo 2.1 na urefu wa nchi 17.7. Mtoto huonekana kama binadamu na Kama dalili za uchungu zitaonekana katika wiki hii utawekwa chini ya uangalizi wa karibu wewe na mtoto tumboni.


Katika wiki hii, mjamzito huendelea kuona dalili na maudhi mbali mbali kama vile kushindwa kupumua, maumivu ya kiuno na mgongo, bawasiri, haja ngumu, kuvimba miguu n.k


Je, mtoto anakuwa amekamilika?


Hapana. Ni mapema sana kwa wakati huu kupata uchungu na endapo utatokea itaitwa uchungu kabla ya mimba kukomaa au kabla ya wakati. Madhara aina fulani yanaweza kupelekea ukapata uchungu wakati huu kama vile, kuwa na maji mengi kwenye chupa ya uzazi au kuwa na mimba ya mapacha.


Dalili za uchungu wiki ya 34

Si kawaida kupata uchungu katika wiki ya 34, endapo itatokea mtoto akizaliwa anaweza kuwa na afya njema hata hivyo atakuwa kwenye uangalizi maalumu kwa siku za awali. Dalili zifuatazo zinaweza kutokea;


Kujongea kwa misuli ya tumbo la chini

Kwenye wiki hii ya 34 unaweza kuhisi dalili hii kama ishara ya awali za uchungu, dalili hii humaanisha uchungu wa uongo kwa mijongeo ya misuli huwa haina mpangilio maalumu na haitokei mara kwa mara kama uchungu wa kweli.


Kuzibuka kwa kifuniko cha shingo ya kizazi

Kutokwa na makamasi mengi ukeni yanayoweza kuwa ya rangi ya maji, pinki, au kuwa na michirizi yad amu. Dalili hii ni kiashiria cha kutoka kwa kifuniko cha shingo ya kizazi ambacho huzuia vimelea kutoka ukeni kuingia kwenye kizazi. 


Makamasi yanaweza kutoka kwa dakika chache, masaa au siku kadhaa kabla ya uchungu kuanza. Dalili hii huwa haigunduliwi na wanawake wengi.


Maumivu ya mgongo

Maumivu mara nyingi huwa ya mgongo wa chini yaani katika maeneo ya kiuno, ambayo huwa endelevu na huwa makali ya kutovumilika kwenye hatua za mwisho za uchungu. Maumivu haya yanahusishwa kusababishwa na mgandamizo kwenye via na mishipa ya fahamu ya mfuko wa matumbo(peritoniamu) kutokana na unaoletwa na kukua kwa kizazi.


Hisia za za kujisaidia

Ni ishara ya mgandamizo kwenye matumbo na kibofu cha mkojo hivyo kupelekea hisia za kutaka kujisaidia. Hi pia humaanisha mtoto anajongea uelekeo wa kutoka nje ya kizazi kwa jina jingine mtoto kushuka. Mara nyingi hizia hizi huletwa na mgandamizo wa kichwa cha mtoto kwenye maeneo tajwa.


Kupasuka kwa chupa ya uzazi

Kati ya wanawake 10, mjamzito mmoja hupata dalili hii ambayo hutokea sana nyumbani wakati umelala. Baadhi ya nyakati chupa ya uzazi hupasuka kwenye uchungu na wakati mwingine hupasuliwa kwneye hatua ya pili ya uchungu.


Baadhi ya nyakahu huwa ni vigumu kutofautisha kati ya mkojo na maji ya chupa ya uzazi. Hata hivyo kupasuka kwa chupa ya uzazi huambatana na maji mengi yanayochuruzika kwenye mapaja kama mtu amesimama na huwa meupe, hayana harufu na hutoka mengi kwa ghafla au kuendelea kumwagika taratibu.


Kama ukipata dalili hii hakikisha kuwa si mkojo kwa kunusa, na kama ikionekana si mkojo unapaswa kuzingatia utoshiriki ngono au kutumia pedi ya kuchomeka ukeni au kufanya chochote kinachoweza kuingiza bakteria ukeni. Wakati huu onana na mtoa huduma ya afya. 


Maji yakiwa na rangi tofauti na maji au harufu huweza kuashiria, maambukizi, au kuchanganyika  na choo cha mtoto.


Mabadiliko ya urefu na upana wa shingo ya kizazi

Shingo ya kizazi huwa fupi na nyembamba. Hii ni ishara kwamba sehemu ya chini ya kizazi inajiandaa kwa ajili ya kutoa mtoto kwa kuwa shingo kuwa nyembamba hufanya iweze kutanuka kirahisi Zaidi. Dalili hii hupimwa na mtaalamu wa afya kwa kutia vidole viwili ukeni ili kuifikia shingo ya kizazi.


Ongezeko kipenyo cha shingo ya kizazi

Kuongezeka kwa kipenyo cha shingo ya kizazi ni dalili inayoashiria kufunguka kwa njia ya uzazi ili kichwa cha mtoto. Kizio cha kipimo hiki ni sentimita na kipenyo cha mwisho cha kutanuka ni sentimita 10. Dalili hii huwezi kuifahamu mwenyewe, mtaalamu wa afya hupima shingo ya kizazi kupitia uke kutumia vidole viwili kila baada ya masaa 2 hadi 4 ikitegemea hatua ya uchungu uliyonayo. Hatua za awali za uchungu huweza kuchukua muda kabla ya kwenda kuwa uchungu wa kujifungua


Je, ni salama kujifungua wiki ya 34

Katika kipindi hiki, unakuwa umebakisha wiki 3 hadi 6 kabla ya kujifungua. Ingawa mtoto anakuwa amekamilika uumbaji wa viungo na mifumo mingi, wakati huu viungo na mifumo huendelea kukua na kuimarika. Endapo uchungu utataka kutokea, daktari anaweza kutumia njia mbalimbali kuuzuia ili ufike angalau wiki ya 37 na kuendelea ili kuhakikisha kuwa mapafu ya mtoto yamekomaa.


Kama uchungu utaendelea utachomwa sindamo maarufu ya kukomaza mapafu ya mtoto na baada ya kujigunfua utakuwa chini ya uangalizi maalumu kwa siku kadhaa kabla ya kuruhusiwa kwenye nyumbani na mwanao.


Wakati huu kama uchungu haujaanza ni vema kuepuka pia vyakula, dawa au kitu chochote kinachoweza kuamsha uchungu.

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

21 Julai 2023 15:32:19

Rejea za dawa

  1. Hutchison J, et al. Stages of Labor. 2023 Jan 30. In: StatPearls [Internet]. Treasure Island (FL): StatPearls Publishing; 2023 Jan–. PMID: 31335010.

  2. Melzack R, et al. Low-back pain during labor. Am J Obstet Gynecol. 1987 Apr;156(4):901-5. doi: 10.1016/0002-9378(87)90349-8. PMID: 2953242.

  3. NHS. Pregnancy signs. https://www.nhs.uk/pregnancy/labour-and-birth/signs-of-labour/signs-that-labour-has-begun/. Imechukuliwa 18.07.2023

  4.  Signs and Symptoms of Labor. https://americanpregnancy.org/healthy-pregnancy/labor-and-birth/signs-of-labor/. Imechukuliwa 18.07.2023

  5. William’s Obstetrics Twenty-Second Ed. Cunningham, F. Gary, et al, Ch. 17.

  6. Cleveland clinic. 8 Signs That Labor Is 24 to 48 Hours Away. https://www.google.com/search?q=labor+symptoms&client. Imechukuliwa 18.07.2023

  7. NCBI. Stages of labor. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK544290/#:. Imechukuliwa 18.07.2023

  8. Pregnancy week by week. Week 35. https://www.thebump.com/pregnancy-week-by-week/37-weeks-pregnant. Imechukuliwa 20.07.2023

bottom of page