top of page

Mwandishi:

Dkt. Peter A, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

5 Novemba 2021 17:51:12

Image-empty-state.png

Maandalizi ya kubeba mimba

Kuna mambo mengi yanayoshauriwa kitaalamu kufanyika kabla ya kushika mimba ili kuboresha afya yako kabla na wakati ukiwa mjamzito. Kuboresha afya husaidia kupunguza hatari ya kujifungua mtoto kabla ya wakati, kujifungua mtoto njiti na matatizo mbalimbali ya ujuzito yanayoweza kutokea. Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa, kubeba ujauzito baada ya kufanya maandalizi huambatana na matokeo mazuri ya ujauzito.


Mambo gani unapaswa kuzingatia kabla ya kubeba mimba?

Makala hii imezungumzia mambo yafuatayo ambayo yanapaswa kufanyika kabla ya kubeba mimba;


Mambo ya kufanya kabla ya kupata ujauzito

 • Fanya vipimo vya mwili wako

 • Tumia vidonde vya folic asidi

 • Fahamu historia ya familia yako

 • Kuwasiliana na daktari kwa ushauri

 • Pata tiba ya akili

 • Kula mlo kamili


Mambo ya kuacha fanya kabla ya kupata ujauzito

 • Acha kutumia pombe na vinywaji vyenye kafeini

 • Acha kuvuta sigara

Acha kuvuta sigara/tumbaku

Kwanini uache uvitaji wa sigara kabla ya kuwa mjamzito?

Uvutaji wa sigara au tumbaku huambatana na mambo yafuatayo;


 • Huchangia kwa asilimia 20 ya watoto njiti wanaozaliwa

 • Huchangia asilimia 8 ya watoto wanaozaliwa kabla ya umri

 • Huchangia asilimia 5 ya vifo vya watoto wakati wa kuzaliwa


Mambo mengine yanayofanywa na sigara

Mbali na kusababisha matatizo kwa mama na mtoto kama yalivyoorodheshwa hapo juu, uvuaji matumizi ya zao la tumbaku huambatana na ugumu katika kushika mimba kwa wanawake wanaotumia sigara. Kemikali ndani ya sigara hupunguza homon estrogen, homon muhimu katika katika ujauzito.


Hata hivyo pia ukiacha kuvuta mazao ya tumbaku unaongeza uwezekano wa kupata mimba haraka na pia kupata mtoto mwenye afya bora

Kutumia folic Asidi

Kwanini kutumia folic asidi?

Folic asidi ni moja ya vitamin muhimu mwilini inayozuia uwezekano wakupata watoto wenye matatizo ya kuzaliwa katika mfumo wa fahamu kama vile mgongo wazi na matatizo mengine yanayotishia uhai wa mtoto.


Wakati wa kuanza kutumia folic asidi?

Wataalamu wa afya wanashauri wanawake wanaotarajia kupata ujauzito kuanza tumia folic asidi kuanzia wiki 4, 6 au 8 kabla ya kupata ujauzito. Hii itafanya uwe na kiwango kizuri kwenye damu kabla ya kupata ujauzito.


Maelezo zaidi kuhusu folic asidi na umuhimu wake yanapatikana katika Makala ya folic asidi kwa mjamzito.


Acha pombe na vinywaji vyenye kafeini

Ni muhimu kuacha matumizi ya pombe na vinywaji vyenye kafeini hasa pale unapotaka kufanya maambuzi ya kubeba mimba.


Baada ya kumaliza hedhi mzunguko unaofuatia huwa wa muhimu sana maana mimba huweza kutungwa kwa kipindi hiki hivo kama unajua unataka kupata mimba basi ni vyema ukaacha vinywaji hivi.


Kama umepata mimba na hukujua na ulikuwa unatumia vinywaji hivi basi unaweza kuendelea na mimba hiyo ila unatakiwa uache matumizi hayo mara moja.


Pombe husababisha matatizo gani kwa kijusi?

Pombe huweza sababisha mama kujifungua mtoto mwenye matatizo katika mfumo wa fahamu, kuwa na uelewa hafifu na kuzaliwa njiti. Matatizo makubwa yanayoweza kutokea ni sindromu ya pombe.

Fanya vipimo

Kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali hulenga kutambua kama una magonjwa ambayo yana hatari kwenye ujauzito wako na kijusi tumboni haswa yale yanayoongeza hatari ya mimba kutoka na kujifungua mtoto mwenye madhaifu ya kimaumbile.


Magonjwa yanayosababisha madhaifu ya kimaumbile kwa mtoto ni;Vipimo gani unapswa kufanya kabla ya kubeba mimba?

Unaweza kufanya vipimo mbalimbali kabla ya kushika mimba katika makundi yafuatayo;


Vipimo vya magonjwa ya ulemavu

Vipimo vya magonjwa yanayosababisha ulemavu kwa mtoto kama yaliyotajwa kwenye mfano


Vipimo vya magonjwa mengine

Vipimo vya magonjwa mengine ni kama vile;


 • Kipimo cha VVU

 • Kipimo cha gono

 • Kipimo cha magonjwa ya ndani ya mfu


Vipimo vingine

 • Kipimo cha wingi wa damu

 • Kipimo cha rhesus

 • Kipimo cha fosfolipid alfa kwa mwenye kihatarishi

 • Kipimo cha Sickle cell kama unaishi maeneo yenye hali ya juu ya ugonjwa huu


Nini unapaswa kufanya baada ya vipimo?

Mara baada ya kufanya vipimo unapaswa kupata matibabu kama utagundulika na maognjwa hayo kabla ya kufikiria beba ujauzito. Baada ya kupona unapaswa kujilinda pia na magonjwa hayo kulingana na yanayvyoambukizwa ili kuepuka maambukizi. Kwa magonjwa ambayo yanatolewa chanjo, unapaswa kupata chanjo kabla ya kupata ujauzito.


Madhara ya magonjwa ya zinaa kwa mtoto

Magonjwa ya zinaa ni hatari kwani huweza kumdhuru mtoto na kusababisha matatizo ya kuzaliwa nayo kama upofu, kuharibika kwa mimba.

Punguza uzito

Kama una uzito uliozidi kiwango, punguza uzito na dhibiti ongezeko lako la uzito wakati wote wa ujauzito. Kuna kiwango cha uzito kinachokubalika katika ujauzito( unaweza kusoma katika Makala nyingine)


Uzito mkubwa una shinda gani?

Watu wenye uzito zaidi ya kiwango kinachoshauriwa wana hatari ya kupata matatizo mengi wakati wa ujauzito kama, magonjwa ya moyo, kisukari, saratani ya ziwa, ukuta wa ndani ya uzazi na utumbo mpana.


Madhara ya uzito mdogo kupita kiasi

Si tu kuwa na uzito mkubwa ni hatari, kuwa na uzito mdogo huambatana pia na matatizo mbalimbali ya uzazi kama kukosa uwiano mzuri wa homon mwilini, hali inayoweza kupelekea mimba kutoka.

Fahamu historia ya familia yako

Kujifunza historia ya familia yako inaweza kukusaidia kutambua magonjwa ambayo yanarithiwa kwenye familia, hivyo dakitari wako ataweza kukushauri mambo ya kufanya ili kuweza kupata familia bora. Mfano ugonjwa wa sickle cell (SCD) hurithiwa na endapo ugonjwa huu upo kwenye familia, dakitari anaweza kukushauri na kukupima wewe na mpenzi wako kuona kama mna vinasaba vya ugonjwa huu vinavyoweza kusafilishwa kwa mtoto.


Kufanya hivi unazuia hatari ya kupata mtoto mwenye matatizo mbalimbali au kujipanga na mambo yanayoweza kutokea.

Pata ushauri wa dakitari

Daktari anaweza kukuuliza historia mbalimbali ya maisha yako kuhusu magonjwa ulionayo na jinsi yanavyoweza kudhuru ujauzito wako, hivyo kabla hujapata ujauzito ni vema kumwambia daktari kuhusu magonjwa hayo pia unaweza kumkubusha dakitari wako kama asipokuuliza kuhusu ugonjwa ulio nao.


Magonjwa gani yanapaswa kuripotiwa kwa daktari kwa ushauri zaidi kabla ya kupata ujauzito?

Magonjwa yoyote yale yanayofanya utumie dawa kwa muda mrefu mfano;


Pata tiba ya akili

Akili ni jinsi tunavyo fikiri, hisi, tenda na kuendana na hali ya maisha. Ikiwa unamatatizo kama vile unajisikia hofu zaidi ya kawaida na una huzuni, au misongo ya mawazo ni vema ukaonana na dakitari ili ajue unatatizo gani na aweze kukupa ushauri na matibabu sahihi kabla ya kupata ujauzito. Hali na magonjwa ya akili yanaweza kuathiri ujauzito wako hivyo ni vema kuwasiliana na daktari kabla ya kushika mimba.


Kula mlo kamili

Kula mlo kamili kutakufanya kupata vitamin na madini muhimu kwa afya yako na mtoto tumboni, fahamu kuhusu mlo kamili katika makala ya chakula kwa mjamzito.

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

21 Mei 2023 12:34:55

Rejea za dawa

 1. Stegmann BJ, Carey JC. TORCH Infections. Toxoplasmosis, Other (syphilis, varicella-zoster, parvovirus B19), Rubella, Cytomegalovirus (CMV), and Herpes infections. Curr Womens Health Rep. 2002 Aug;2(4):253-8. PMID: 12150751.

 2. Sarah E Santiago, Grace H Park, and Kelly J Huffman. Consumption habits of pregnant women and implications for developmental biology: a survey of predominantly Hispanic women in California. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3704911.

 3. EMILY OKEN et al. Diet During Pregnancy and Risk of Preeclampsia or Gestational Hypertension. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2532559/?report=reader

 4. CDC mercury fact sheet.https://www.cdc.gov/biomonitoring/Mercury_FactSheet.html

 5. Philip W. Davidson et l. Fish Consumption, Mercury Exposure, and Their Associations with Scholastic Achievement in the Seychelles Child Development Study. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2934742/?report=reader

 6. Wolters Kluwer Health.Obstetrical & Gynecological Survey. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4949006/#!po=14.8352

 7. Katherine Bowerse et al.A prospective study of prepregnancy dietary fat intake and risk of gestational diabetes. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3260071/?report=reader

 8. Graham Devereux, et al. Low Maternal Vitamin E Intake during Pregnancy Is Associated with Asthma in 5-Year-Old Children.https://www.atsjournals.org/doi/10.1164/rccm.200512-1946OC?url_ver=Z39.882003&rfr_id=ori%3Arid%3Acrossref.org&rfr_dat=cr_pub++0pubmed&

 9. Kirsten Herrick, David I. W. Phillips, Soraya Haselden, Alistair W. Shiell, Mary Campbell-Brown, Keith M. Godfrey. Maternal Consumption of a High-Meat, Low-Carbohydrate Diet in Late Pregnancy: Relation to Adult Cortisol Concentrations in the  offspring.https://academic.oup.com/jcem/article/88/8/3554/2845229

 10. High cholesterol foods.https://www.healthline.com/nutrition/high-cholesterol-foods#lowering-cholesterol

 11. Alison N.Thorburn et al. Evidence that asthma is a developmental origin disease influenced by maternal diet and bacterial metabolites.https://www.nature.com/articles/ncomms8320

 12. MK Javaid et al. Maternal vitamin D status during pregnancy and childhood bone mass at age 9 years:alongitudinal study.Published: January07,2006DOI:https://doi.org/10.1016/S0140-6736(06)67922-1

 13. Healthline. 15 healthy foods that are high in folate (folic acid).https://www.healthline.com/nutrition/foods-high-in-folate-folic-acid#10.-Beef-liver

 14. American Red Cross. Iron rich foods.https://www.redcrossblood.org/donate-blood/blood-donation-process/before-during-after/iron-blood-donation/iron-rich-foods.html

 15. Medical news today.10 foods rich in vitamin E.https://www.medicalnewstoday.com/articles/324308

bottom of page