top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

5 Novemba 2021 18:11:56

Image-empty-state.png

Rhesus na ujauzito

Je hali yako ya rhesus ni nini?

Mama anapoenda hosptali kwa mara ya kwanza kabisa anapokuwa mjamzito hupata fursa ya kupima vipimo mbalimbali kama wingi wa damu, kundi la damu ( A, B, AB au O) na hali ya rhesus yaani rhesus positive ama Negative (rhesus chanya ama hasi)

Hali ya Rhesus hurithiwa katika vinasaba ambavyo hutengeneza protini inayoitwa D antigen. Ukiwa ni rhesus chanya (+) maana yake ni kwamba unayo protini hiyo katika chembe zako nyekundu za damu na ukiwa hasi (-) maanake hauna protin hiyo na utaitwa rhesus hasi. Watu wengi duniani huwa ni rhesus chanya

Ni vip hali yako ya rhesus inadhuru mtoto?

Rhesus husababisha kuharibika kwa ujauzito zinazofuata baada ya ujauzito wa kwanza. Hutokea kwa mama mwenye rhesus hasi aliyebeba mtoto mwenye damu ya rhesus chanya aliyorithi kutoka kwa baba yake.

Kama damu ya mtoto itagusana na ya mama wakati wa kujifungua, kinga yako ya mwili (mama) itaamsha chembe hai za ulizi dhidi ya damu hiyo ya rhesus chanya kutoka kwa mtoto, chembe hizi huzalisha kemikali zinazokaa mwilini kwa muda mrefu sana na pia hutunza kumbukumbu. Kwa mimba ya kwanza mama atajifungua vema tu.

Mama atakapopata ujauzito mwingine basi chembe hizi na chemikali hizo hupita katika kondo la mama na kuingia kwa mtoto na kumuua. Mambo haya hutokea kwa sababu mtoto hutambuliwa kuwa kitu kigeni na mfumo wa kinga ya mwili wa mama.

Hivo wamama wengi wenye tatizo hili huwa na historia ya kuwa na mtoto mmoja na mimba zinazofuata zote mtoto hufia tumboni.

Je sindano ya ant-D hufanya kazi gani?

Dawa hii huzuia kutengenezwa kwa kemikali zinazoleta madhara kwa mtoto pia huharibu chembe chembe za mtoto katika mfumo wa damu wa mama na hivo husababisha kuzuia kutengenezwa kwa kemikali hizo. Ni jambo la msingi kuzuia kutengenezwa kwa kemikali hizi kwa sababu endapo zitatengenezwa hudumu katika mwili wako daima.

Dakitari wako atakuchoma sindano hii kwenye bega

Dawa hii itachomwa kwenye wiki 28 na 34 za ujauzito, baadhi ya klinic hutoa kwenye wiki ya 28 na 30 kiwango kikubwa cha dozi ya dawa hii.

Dawa hii unatakiwa kupewa pia ndani ya masaa 72 kwenye tukio ambapo damu ya mtoto itagusana na damu ya mama (wakati wa kujifungua, kupigwa tumboni, kutokwa na damu baada ya wiki 20 za ujauzito, kutolewa maji kwenye kifuko cha mimba,kufuzungushwa kwa mtoto ili kichwa kitangulie kutoka kwa mtoto ambaye alikuwa ametanguliza makalio, ujauzito kutishia kutoka)

Vipi kama nina kemikali hizi zinazoua mtoto?

Mtaalamu wa afya atapima damu yako mapema kabisa katika ujauzito wako na katika wiki ya 28 ya ujauzito kuangalia kama kunakemikali hizi. Wakati mwingine kemikali hizi zinaweza kutengenezwa bila wewe kujua endapo mimba ilitoka ama ujauzito ulitungwa nnje ya mfuko wa kizazi .Kama umepimwa na ukakutwa unakemikali hizi basi hutachomwa sindano hii, kwa sababu dawa hii huzuia kutengenezwa kwa kemikali hizo na ikiwa zimeshatengenezwa basi hutapewa maana haitakuwa na msaada kwako. Mbadala wake ni kwamba utahitaji kuonana na mtaalamu wa kinamama ili upate uchunguzi na uangalizi wa karibu

Mtaalamu huyu atakuwa anacheki hali ya mtoto endapo anaishiwa damu atapewa damu hata kabla ya kuzaliwa. Matibabu haya huwa na matokeo mazuri na mtoto huweza kuzaliwa, ingawa hushauriwa mtoto kuzaliwa kabla ya wakati kwa kuanzisha uchungu ama kufanyiwa upasuaji. Mtoto anapozaliwa hulazwa wodi maalumu ya vichanga kwa unagalizi zaidi, endapo atapata manjano atapewa matibabu ya mwanga ili kusaidia ini lake kusafisha kemikali manjano mwilini mwake

Nini hufanyika mtoto anapozaliwa?

Mtoto anapozaliwa damu kwenye kitovu chake huchukuliwa na kupimwa kundi lake na hali yake ya rhesus

Endapo mtoto ni rhesus chanya, mama utachomwa sindano nyingine ya ant-D na hii hutolewa ndani ya masaa 72 ya kujifungua ili kwamba kinga zako za mwili zisiamke na kutengeneza kemikali zinazoua mtoto kwa mimba ijayo.

Endapo mtoto wako ni rhesus hasi na wewe ni rhesus hasi basi hutachomwa dawa hii.

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

10 Juni 2023 11:55:58

Rejea za dawa

  1. John Costumbrado, et al. Rh Incompatibility. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK459353/. Imechukuliwa 5/11/2021

  2. Frequently asked questions. Pregnancy FAQ027. The Rh factor: How it can affect your pregnancy. American College of Obstetricians and Gynecologists. https://www.acog.org/Patients/FAQs/The-Rh-Factor-How-It-Can-Affect-Your-Pregnancy. Imechukuliwa 5/11/2021

  3. Moise KJ. Overview of Rhesus (Rh) alloimmunization in pregnancy. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 5/11/2021

  4. Moise KJ. Prevention of Rh (D) alloimmunization. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 5/11/2021

  5. American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG) Committee on Practice Bulletins. Obstetrics. ACOG Practice Bulletin No. 192: Management of alloimmunization during pregnancy. Obstetrics & Gynecology. 2018;131:611.

  6. American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG) Committee on Practice Bulletins. Obstetrics. ACOG Practice Bulletin No. 181: Prevention of Rh D alloimmunization. Obstetrics & Gynecology. 2017;130:e57.

bottom of page