top of page

Mwandishi:

Dkt. Adolf S, M.D

Mhariri:

Dkt. Sospeter B, M.D

21 Julai 2023, 12:01:54

Image-empty-state.png

Umri na kimo cha mimba kutofautiana

Kupima kimo cha mimba imekua ni njia rahisi na ya haraka ya kutambua mambo mbali mbali katika ujauzito, pia kukadiria umri wa ujauzito.Njia hii imekua ikitumika sana hasa katika maeneo ambayo hakuna huduma za kipimo cha ultrasound, licha ya kutokuwa njia yenye ufanisi mkubwa kutokana na kuathiriwa na mambo mbalimbali. 


Katika kutambua umri wa mimba, sentimeta 1 ya kimo cha mimba huwa ni sawa na wiki 1 ya ujauzito. Mfano kimo cha mimba sentimeta 28 ni sawa na wiki 28 za ujauzito. Hata hivyo si mara zote uwiano huu huwa sawa.


Je, mambo gani husababisha utofauti kati ya kimo cha mimba na umri wa mimba?

Hali na magonjwa yafutayo huchangia kuwa na utofauti 

  • Kimo cha mimba kikubwa kuliko umri wa mimba

  • Hali hii inaweza kusababishwa na mambo yafutayo;

  • Mtoto mkubwa

  • Mimba ya mapacha

  • Maji mengi ya amniotiki

  • Obeziti 

  • Kupima kimo wakati kibofu cha mkojo kimejaa

  • Kusahau tarehe ya mwisho ya kuanza hedhi ambayo hutumika kutambua umri wa mimba

 

Kimo cha mimba kidogo kuliko umri wa mimba

Hali hii inaweza kusababishwa na mambo yafutayo;

  • Mtoto mdogo

  • Maji ya amniotiki kidogo

  • Kudumaa kwa mtoto tumboni

  • Kushuka kwa mtoto wiki za mwisho za kuelekea leba

  • Kusahau tarehe ya mwisho ya kuanza hedhi ambayo hutumika kutambua umri wa mimba


Nini cha kufanya endapo utaona utofauti kati ya kimo na umri wa mimba?

Ni kawaida kuwa na utofauti kati ya kimo cha mimba na umri wa mimba walau utofauti wa sentimeta 2 mpaka 3, utofauti zaidi ya kiwango hiki huashiria kitu fulani katika mimba.


Hivyo unahitaji kuonana na mtaalamu wa afya kwa uchunguzi zaidi kwa kutumia kipimo cha ultrasound ili kubaini kisababishi.

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

21 Julai 2023, 12:01:54

Rejea za dawa

  1. Measurement of symphysis fundal height for gestational age estimation in low-to-middle-income countries: A systematic review and meta-analysis. NCBI. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC9409500/. Imechukuliwa 21.07.2023

  2. What to Know About Measuring Fundal Height. WebMD. https://www.webmd.com/baby/what-to-know-about-measuring-fundal-height. Imechukuliwa 21.07.2023

  3. Fundal height: What it means, by week, and accuracy. Medical News Today. https://www.medicalnewstoday.com/articles/fundal-height. Imechukuliwa 21.07.2023

bottom of page