Mwandishi:
Dkt. Salome A, MD
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
16 Aprili 2022 18:57:33
Wiki ya 11 ya ujauzito
Nini hutokea kwa mtoto
Kijusi hukua na kupata taswira ya binadamu
Kichwa huwa cha mviringo na chenye mabonde
Jicho huwa limefungwa kwa kigubiko cha jicho
Matundu ya vinyweleo huanza kutengenezwa kwenye ngozi
Matumbo huwa yamedumbukia katika kitovu cha mtoto
Sehemu za nje za siri huwepo lakini huwa hazijatengenezwa vizuri hivyo kushindwa kujua jinsia ya mtoto
Nini hutokea kwa mama
Hakuna mabadiliko makubwa ukilinganisha na wiki za awali
Mama huendelea kuhisi dalili za ujauzito kama kuvimba matiti, kubagua chakula, kichefuchefu na kutapika nk.
Majina mengine
Majina mengine yanayoendana na mada hii ni:
Ujauzito wa wiki 11
Mimba ya wiki 11
Wiki 11 ya mimba
Kijusi cha wiki 11
Mwonekano wa ujauzito wa wiki 11
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
15 Julai 2022 18:50:54
Rejea za dawa
https://obgyn.mhmedical.com/content.aspx?bookid=2977§ionid=249396578
Medical Embrology by T.W.Sadler. ISBN: 978-1-260-46273-9
Williams Obstetrics, 26e. CHAPTER 7: Embryogenesis and Fetal Developmenthttps://obgyn.mhmedical.com/content.aspx?bookid=2977§ionid=250337469.