Mwandishi:
Dkt. Salome A, MD
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
16 Aprili 2022 19:07:17
Wiki ya 12 ya ujauzito
Nini hutokea kwa mtoto
Umbo na sura halisi ya binadamu huonekana lakini masikio huwa hayajakua vizuri
Vidole vya miguu na mikono huwa na umbo linaloeleweka na kucha huanza kutokea
Ngozi ya mtoto huwa nyembamba kiasi cha kuonyesha vilivyomo ndani ya mwili wake kama vile mishipa ya damu
Nyusi na nywele za kichwa huota, na mwili huwa na vinyweleo vichanga vilivyotawanyika (lanugo)
Katika kipindi hiki sehemu za siri za nje huanza kuonesha tofauti kati ya jinsia ME na jinsia KE
Matumbo huhama kutoka katika kitovu cha mtoto na kuwa katika eneo la wazi linalounganisha kifua na kiwamba tumbo
Misuli hupata huwa na mjongeo (primitive reflexes)
Mtoto huanza kucheza tumboni lakini si rahisi kwa mama kuhisi
Nini hutokea kwa mama
Kizazi hutanuka kiasi cha kuweza kupapaswa juu ya kinena
Dalili za kichefuchefu na kutapika huanza kupungua hata hivyo dalili nyingine za ujauzito kama vile kuhisi kuchoka, kukojoa mara kwa mara, kutokwa na ute ute ukeni nk. huendelea kuonekana
Majina mengine
Majina mengine yanayoendana na mada hii ni:
Ujauzito wa wiki 12
Mimba ya wiki 12
Wiki 12 ya mimba
Kijusi cha wiki 12
Mwonekano wa ujauzito wa wiki 12
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 18:50:39
Rejea za dawa
Williams Obstetrics, 26e. CHAPTER 7: Embryogenesis and Fetal Developmenthttps://obgyn.mhmedical.com/content.aspx?bookid=2977§ionid=250337469.