top of page

Elimu ya magonjwa kwa mjamzito

Sehemu hii utajifunza maelezo ya ziada kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa ujauzito. Unashauriwa siku zote kuwasilaina na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile iliyoandikwa humu ili kupata ushauri unaoendana na hali yako ya kiafya.

Kujifungua kwa uke baada ya upasuaji

Kujifungua kwa uke baada ya upasuaji

Kama ulijifungua kwa upasuaji kwenye ujauzito uliopita kwa sababu ya mtoto kulala vibaya au kutanguliza makalio, una uwezekano wa kujifungua salama kwa njia ya kawaida ukiwa chini ya uangalizi wa mtaalamu wa afya.

Dalili hatari kwenye ujauzito

Dalili hatari kwenye ujauzito

Ukipata dalili kama kutokwa damu, uteute au majimaji yasiyo ya kawaida ukeni, maumivu makali ya tumbo, kuongezeka kwa shinikizo la damu, homa, kutoona vema na kupoteza fahamu, onana na daktari haraka kwa uchunguzi.

Mabadiliko ya mwili kwenye ujauzito

Mabadiliko ya mwili kwenye ujauzito

Kuna mabadiliko mengi ya mwili hutokea wakati wa ujauzito, kufahamu kuhusu mabadiliko hayo hukufanya uwe tayari kuchukua hatua sahihi kwa afya yako na mtoto uliyembeba tumboni.

Uchungu

Uchungu

Ni matokeo ya mijongeo ya misuli ya mji wa mimba, tendo linaloamshwa na kemikali pamoja na homoni mbalimbali zinazozalishwa na mama pamoja na mtoto.

Presha sugu kwa mjamzito

Presha sugu kwa mjamzito

Shinikizo la juu la damu linalotokea wakati wa ujauzito hutishia afya ya mama na mtoto tumboni. Shinikizo la juu huthibitishwa kama shinikizo la sistoliki kwa dayastoliki 140/90 mmHg au zaidi katika vipimo viwili au zaidi vilivyofanyika kwa utofauti wa masaa 2.

bottom of page