top of page

Elimu ya magonjwa kwa mjamzito

Sehemu hii utajifunza maelezo ya ziada kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa ujauzito. Unashauriwa siku zote kuwasilaina na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile iliyoandikwa humu ili kupata ushauri unaoendana na hali yako ya kiafya.

Ujauzito uliopitiliza tarehe

Ujauzito uliopitiliza tarehe

Ujauzito kupitiliza umri hufahamika kwa majina mengine ya ‘ujauzito uliopitiliza tarehe’ au ‘uliopitiliza muda’, hutokea endapo mjamzito hajajifungua katika tarehe ya matarajio ya kujifungua baada ya kutimiza wiki 40 kamili au siku 280 za ujauzito.

Mtoto mwenye uzito mkubwa

Mtoto mwenye uzito mkubwa

Kwa kawaida mtoto anatakiwa kuzaliwa na uzito wa kilo 2.5 hadi kilo 3.9, sawa na gramu 2500 hadi gramu 3900. Mtoto kuzaliwa na uzito wa zaidi ya gramu 3900 bila kujali wiki za ujauzito, huitwa mtoto mwenye uzito mkubwa.

Chakula kwa mjamzito

Chakula kwa mjamzito

Matokeo mazuri ya ujauzito kwa mama na mtoto hutegemea mambo mengi ikiwemo lishe ya mama kabla ya kupata ujauzito na katika kipindi chote cha ujauzito. Kupata ujauzito wenye matokeo mazuri pata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa afya.

Malaria kwa mjamzito

Malaria kwa mjamzito

Mabadiliko ya kifiziolojia yanayotokea katika ujauzito, huwafanya wajawazito kuwa katika hatari ya kupata malaria kuliko watu wengine. Jikinge na malaria kuepusha madhara kwako na mtoto.

Ujauzito na VVU

Ujauzito na VVU

Mama mjamzito mwenye maambukizi ya VVU anaweza kumwambukiza mwanae wakati anakua tumboni, kujifungua au wakati wa kunyonyesha.

bottom of page