Kuwahi kufika kileleni (kumwaga shahawa mapema) hutokea pale mwanaume anapomwaga shahawa mapema tofauti na matarajio yake au mpenzi wake.
Kama unafika kileleni mapema mara kwa mara, itakubi utafute msaada wa kiafya, lakini endapo ni mara chache basi huna haja ya kuhofia maana hutokea kwa wanaume wengi.
​
Ili usemekane kuwa unawahi kufika kileleni, utakuwa unawahi kumwaga manii ndani ya dakika moja unapoingiza mboo kwenye uke, unashindwa kuzuia shahawa kutoka wakati wa tendo mara nyingi au karibia mara zote na unajihisi haupo sawa katika tendo na wakati mwingine unaogopa kushiriki kujamiiana kwa sababu ya woga wa kuwahi kumwaga shahawa.
Mambo ya kisaikolojia na kifiziolojia huchangia mtu kuwahi kumwaga shahawa wakati wa tendo. Hata hivyo matibabu yapo, Â hivyo usiwe na hofu.
Kuwahi kufika kileleni kunaweza kugawanywa katika makundi mawili, kundi la kwanza ni tatizo la maisha ikiwa inamaanisha toka uanze kushiriki kujamiana umekuwa unamwaga upesi. Kundi la pili ni tatizo linalopatikana baadae ikiwa inamanisha ulikuwa na uwezo wa kuchelewa kumwaga lakini sasa unamwaga shahawa mapema zaidi ya matarajio yako.
Visababishi
​
Kuna visababishi vya kisaikolojia, kibayolojia na visababishi vingine
Visababishi vya kisaikolojia
​
Kuwahi kuanza kufanya ngono
Kufanyiwa ukatili wa kingono
Endelea kusoma zaidi kwa kubonyeza hapa