top of page
Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:

Dkt. Glory, MD

ULY CLINIC

7 Juni 2025, 19:33:10

Damu au kinyama mimba ya mwezi mmoja ikiharibika (1).jpg

Kuonekana kwa HIV kwenye kipimo

Swali la msingi na 01


Habari doctor, Je, mtu anaweza kuishi na maambukiz ya HIV ndani ya miezi sita na kwenye kipimo asioneshe ana maambukizi?


Majibu ya daktari ya swali na 01

Ikiwa mtu amepima baada ya miezi sita na hajashiriki ngono tena baada ya tukio la hatari, na bado hana maambukizi, basi kuna uwezekano mkubwa kwamba hana HIV. Kipindi cha dirisha la matazamio huwa kati ya wiki 2 hadi miezi 3 kwa vipimo vya kisasa, hivyo baada ya miezi sita, majibu ya vipimo vinapaswa kuwa sahihi na kuaminiwa. Ikiwa mtu alikuwa ameambukizwa, kipimo kingeonyesha matokeo chanya. Ikiwa bado una wasiwasi, unaweza kurudia kipimo.


Swali kutoka kwa daktari na 01

Je, inamaanisha kuwa mtu huyu hajashiriki ngono bila kinga kwa miezi sita mfululizo pia?


Majibu ya muulizaji ya swali la daktari na 01

Kashiriki pengine mwez wa pil akapat baadhi ya dalili ila amekaa miez sita anaenda kupima yupo negative akaakaa tena miezi 3 ni negative.


Majibu ya Daktari kutokana na majibu ya muulizaji

Kila mara mtu anaposhiriki ngono bila kinga, anapaswa kupima katika kipindi cha baada ya dilisha la matazamio. Kama ilivyoelezewa hapo awali, vipimo vya sasa vinachukua muda wa wiki 2 hadi miezi 3 kuonyesha majibu sahihi. Ikitegemea aina ya kipimo utakachotumia, unaweza kupima baada ya mwezi mmoja hadi miezi 3 tangu umeshiriki ngono mara ya mwisho.


Mambo ya kuzingatia wakati unasubiri kupita kwa dilisha la matazamio

Katika kipindi cha kusubiria majibu sahihi ya kipimo ili kufahamu kama kushiriki kwako mara ya mwisho kumepelekea maambukizi au la, unapaswa kutumia kinga, la sivyo hutapata majibu sahihi kwa kuwa kila unaposhiriki ngono bila kinga utapaswa kusubiria kipindi cha dilisha la matazamio kupita.


Rejea za majadiliano haya:

  1. ULY CLINIC. Window period. https://www.ulyclinic.com/vidokezo-vya-kiafya/window-period-ya-vipimo-vya-vvu. Imechukuliwa 31.03.2025

Imeandikwa:

7 Juni 2025, 19:27:47

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

bottom of page