Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULY CLINIC
15 Juni 2025, 09:45:05
Kwa nini piriodi imesimama?
Kutoona piriodi au hedhi kunajulikana pia kama amenorrea. Ni hali ambayo mwanamke aliyekuwa akipata hedhi kawaida huacha kuona damu ya mwezi kwa muda fulani. Hali hii mara nyingine huitwa pia:
Kutoona period
Kutoona damu ya mwezi
Kuacha kuona period
Kutoingia period
Kusimama kwa period
Kuingia piriod au kipindi cha hedhi hufahamika kama menorhagia. Kutoona daku ya mwezi au period au amenorrhea au majina mengije yaliyoorodheshwa hapo juu humaanisha kutoona damu ha hedhi inayotoka kwa wanawake waliovunja ungo kila mwezi.
Aina ya kutoona hedhi kwenye makala
Makala hii inalenga kuelezea sababu za kutoona hedhi kwa mwanamke aliyekuwa akiona hedhi hapo awali (yaani amenorea baada ya hedhi). Haijadili aina ya kwanza ya amenorrhea ya kuzaliwa (ambapo msichana hajawahi kuona hedhi hata mara moja maishani).
Visababishi vya kutoona hedhi.
Visababishi vimegawanyika katika makundi mbalimbali, baadhi ya visababishi katika kundi la visababishi asili ni:
Kuwa mjamzito
Kunyonyesha
Komahedhi
Visababishi vingine
Visababishi vingine ni mabadiliko ya homoni, matumizimya dawa, madhaifu ya maumbile na maisha.
Maelezo zaidi
Kusoma zaidi kuhusu makala hii soma katika makala ya amenorrhoea inayopatikana kwenye tovuti ya ulyclinic.
Kama una swali zaidi wasiliana na daktari wako kwa ushauri na tiba. Pia unaweza kuwasiliana na daktari wa ulyclinic kupitia linki ya "Pata Tiba" chini ya tovuti hii.
Rejea za mada:
Speroff L, Fritz MA. Clinical Gynecologic Endocrinology and Infertility. 8th ed. Philadelphia: Lippincott Williams & Wilkins; 2010.
American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG). Committee Opinion No. 651: Menstruation in Girls and Adolescents: Using the Menstrual Cycle as a Vital Sign. Obstet Gynecol. 2015;126(6):e143–6.
Klein DA, Poth MA. Amenorrhea: An Approach to Diagnosis and Management. Am Fam Physician. 2013;87(11):781–8.
Deans R, Abbott JA. Review of amenorrhoea and menstrual disturbances in adolescents. Aust Fam Physician. 2010;39(10):751–6.
Practice Committee of the American Society for Reproductive Medicine. Current evaluation of amenorrhea. Fertil Steril. 2008;90(5 Suppl):S219–25.
Gordon CM, Ackerman KE, Berga SL, Kaplan JR, Mastorakos G, Misra M, et al. Functional hypothalamic amenorrhea: an Endocrine Society Clinical Practice Guideline. J Clin Endocrinol Metab. 2017;102(5):1413–39.
Reindollar RH. Diagnosis and initial management of amenorrhea. Am Fam Physician. 2003;67(9):1939–48.
Hoeger KM, Sanfilippo JS. Amenorrhea and Abnormal Uterine Bleeding. In: Berek JS, editor. Berek & Novak’s Gynecology. 15th ed. Philadelphia: Wolters Kluwer; 2012. p. 367–405.
Santoro N. Mechanisms of premature ovarian failure. Ann Endocrinol (Paris). 2003;64(2):87–92.
Hapangama DK, Bulmer JN. Pathophysiology of abnormal uterine bleeding. Best Pract Res Clin Obstet Gynaecol. 2017;40:89–98.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
