Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULY CLINIC
20 Februari 2026, 22:28:24
.jpg)
Nyama nyekundu katika Afya
Utangulizi
Nyama nyekundu ni chanzo kizuri cha virutubisho muhimu kama protini, vitamin B12, na madini chuma. Hata hivyo, ulaji mwingi au ulaji wa nyama zilizohifadhiwa unaweza kuongeza hatari ya magonjwa yasiyoambukizwa. Ili kulinda afya:
Tumia nyama nyekundu kwa kiasi
Pendelea nyama nyeupe na vyanzo vya mimea
Epuka nyama zilizohifadhiwa
Changanya lishe yako na nafaka zisizokobolewa, mboga na matunda
Hii ndiyo njia bora ya kupata virutubisho bila kuathiri afya ya muda mrefu.
Nyama nyekundu ni nini?
Kiafya unaposema nyama nyekundu humaanisha nyama yenye mwonekano wa rangi nyekundu. Nyama nyekundu huwa na mwonekano wa rangi yake kutoka kwenye protini za mayoglobin. Mayoglobini ni protini maalumu inayobeba oksijeni ya misuli, ambayo hutumika kuiwezesha misuli kutengeneza nishati inayowezesha kiumbe kufanya kazi mbalimbali za kifiziolojia kama vile kutembea, kupumua, kusukuma damu n.k

Nyama nyekundu hupatikana kwenye viumbe wengi sana wanaoliwa na binadamu ikiwa pamoja na baadhi ya ndege na samaki ambao hudhaniwa siku zote kuwa wana nyama nyeupe. Licha ya kuwa na viumbe jamii ya ndege wanaofahamika kuwa na nyama nyeupe, viumbe hao huwa na nyama nyekundu kwenye sehemu za miili yao ambazo zinafanya kazi zaidi kama kwenye miguu( kwa kuku wanaotembea) na kwenye mabawa kwa ndege wanaopaa, hata hivyo wanyama wenye nyama nyeupe hata kama wana sehemu zenye nyama nyekundu, nyama hiyo endapo itatumiwa haiwezi kufananishwa na kula nyama nyekundu kutoka kwa wanyama wenye nyama nyekundu.
Viumbe gani waana nyama nyekundu
Wanyama wafuatao huwa na nyama nyekundu;
Kware
Kangaroo
Tausi
Nguruwe
Ngombe
Mbuzi
Kondoo
Ngamia
Nyama nyekundu inafaida gani mwilini?
Kwa ujumla nyama nyekundu huupa mwili nishati, mafuta yaliyoshamiri, nishati na madini chuma ya himu kwa wingi. Nyama nyekundu pia ni chanzo kizuri cha vitamin B12 ambacho hakipatikani kwenye nafaka, matunda au mboga za majani. Virutubisho na madini mengine unayoweza kupata kwenye nyama nyekundu ni;
Mafuta yaliyoshamiri
Protini
Madini ya fosforazi
Hasara za nyama nyekundu
Kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya nyama nyekundu katika nchi zinazoendelea kwa sasa kuliko nchi zilizoendelea, hii inaonekana kuwa ni maisha ya kifahari, hata hivyo kuna magonjwa mengi yasiyo ya kuambukizwa ambayo yanazidi kuongezeka kutokana na maisha haya mapya.
Kwa ujumla nyama nyekundu huwa na kiasi kikubwa cha mafuta yaliyoshamiri, nishati na madini chuma ya himu ambayo huhusika na kuongeza hatari ya kuziba mishipa ya damu hivyo kusababisha magonjwa ya moyo kama kiharusi, mshituko wa moyo n.k, huchosha kongozo inayozalisha homon insulin hivyo kuleta ugonjwa wa kisukari na kusababisha saratani
