top of page
Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

ULY CLINIC

15 Juni 2025, 09:12:00

Damu au kinyama mimba ya mwezi mmoja ikiharibika (1).jpg

Umri wa mimba ni wiki ngapi?

Kwa kawaida, mimba ya binadamu huchukua wastani wa wiki 40 (sawa na miezi 9 na siku 7) tangu siku ya kwanza ya kuona hedhi ya mwisho. Huu ndio msingi unaotumika kitaalamu kukadiria umri wa mimba na tarehe ya kujifungua.


Je, wiki 40 za mimba huhesabiwaje?

Umri wa mimba huanza kuhesabiwa kutoka siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho na siyo siku ya kushika mimba, kwa sababu siku halisi ya kutungwa kwa mimba huwa haifahamiki kwa urahisi kwa wanawake wengi. Kwa wastani, kutunga mimba hutokea wiki ya 2 baada ya hedhi, lakini umri wa ujauzito bado huhesabiwa kuanzia mwanzo wa mzunguko wa hedhi.


Je, wanawake wote hujifungua wiki ya 40?

La hasha. Ingawa wiki 40 ni wastani, wanawake wengi hujifungua kati ya wiki ya 37 hadi 42, kama ifuatavyo:

  • Wiki 37–38: Ujauzito huitwa "Ujauzito mwanzoni mwa ukamili

  • Wiki 39–40: "Ujauzito kamili" – kipindi salama zaidi kwa kujifungua

  • Wiki 41: Hapa ujauzito huitwa mwanzoni mwakupitiliza ukamili

  • Wiki 42 au zaidi: Hapa ujauzito huitwa ujauzito uliopitiliza ukamili


Kwa mujibu wa tafiti, takribani 60% ya wanawake hujifungua kati ya wiki ya 39 hadi 40, lakini pia ni kawaida kwa wengine kujifungua mapema au kuchelewa kulingana na hali zao za kiafya.


Rejea za mada hii:
  1. ULY Clinic. Ujauzito uliopitiliza tarehe [Intaneti]. [Imechukuliwa 2024 Oktoba 2]. Inapatikana kutoka: https://www.ulyclinic.com/elimu-kwa-mjamzito-magonjwa/ujauzito-uliopitiliza-tarehe

  2. ULY Clinic. Wiki 40 za ujauzito [Intaneti]. [Imechukuliwa 2024 Oktoba 2]. Inapatikana kutoka: https://www.ulyclinic.com/elimu-kwa-mjamzito-magonjwa/wiki-ya-40-ya-ujauzito

  3. ULY Clinic. Dalili za uchungu wiki 40 [Intaneti]. [Imechukuliwa 2024 Oktoba 2]. Inapatikana kutoka: https://www.ulyclinic.com/elimu-kwa-mjamzito-magonjwa/dalili-za-uchungu-wiki-ya-40

  4. ULY Clinic. Kujifungua ni wiki ngapi? [video]. YouTube. [Imechukuliwa 2024 Oktoba 2]. Inapatikana kutoka: https://www.youtube.com/watch?v=-glj98daTDQ

  5. Cunningham FG, et al. Williams Obstetrics. 25th ed. McGraw-Hill Education; 2018.

  6. WHO. Pregnancy, Childbirth, Postpartum and Newborn Care: A guide for essential practice. 3rd ed. Geneva: World Health Organization; 2022.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

bottom of page