top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Mistari ya kipimo cha SD Bioline HIV 1/2

Maswali ya msingi

  1. Je, kipimo cha SD bioline HIV1/2 kina mistari mingapi?

  2. Je, rangi ya mstari inatakiwa kuwa ipi ili majibu yawe sahihi?


Majibu

Kipimo cha SD Bioline HIV 1/2 kina mistari miwili au mitatu kulingana na aina yake iliyotengenezwa kwiandani. Hapa chini kuna maelezo ya aina hizi mbili za vipimo:


Kipimo chenye mistari miwili

  1. Mstari wa Kudhibiti (C): Lazima uonekane ili kuthibitisha kuwa kipimo kimefanya kazi sahihi.

  2. Mstari wa Majibu (T ): Ikiwa unaonekana, inaonyesha kuwa mtu ana kingamwili za HIV (HIV-positive).

Kipimo chenye mistari mitatu

  • C (Mstari wa kudhibiti): Lazima iwepo ili kuhakikisha kipimo kimefanya kazi sahihi.

  • T1 (Mstari wa majibu na 1): Inaonyesha uwepo wa kingamwili za HIV-1.

  • T2 (Mstari wa majibu na 2): Inaonyesha uwepo wa kingamwili za HIV-2.

  • Ikiwa mistari yote miwili ya T (T1 na T2) itaonekana, mtu anaweza kuwa na mchanganyiko wa HIV-1 na HIV-2. Hali hii ni nadra sana kutokea.


Matokeo ya Kipimo cha SD Bioline HIV 1/2

  • Mstari mmoja tu kwenye C → Hasi (Negative)

  • Mistari miwili (C na T/T1/T2) → Chanya (Positive)

  • Hakuna mstari wa C → Kipimo hakifai


Rangi ya mistari ya kipimo cha SD bioline HIV1/2

Kwa kipimo cha SD Bioline HIV 1/2 Rapid Test, rangi ya mistari inapaswa kuwa kama ifuatavyo ili matokeo yawe sahihi:

Mstari wa Kudhibiti (C):

  • Mstari huu lazima uonekane kwa rangi nyekundu au rangi ya shaba kama ishara kwamba kipimo kimefanya kazi.

  • Ikiwa mstari huu hauonekani, matokeo yatakuwa batili , na kipimo kinahitaji kurudiwa.


Mstari wa Majibu (T):

  • Ikiwa kipimo kinagundua uwepo wa kingamwili za VVU ( VVU-Chanya au VVU+), mstari huu utaonekana kwa rangi nyekundu au shaba.

  • Ikiwa mstari huu hautaonekana, inamaanisha VVU- au VVU hasi.

  • Katika kipimo cha SD Bioline HIV-1/2 kinachotumia mistari miwili, mstari wa T hautaonekana kama hakuna VVU.

  • Kwa Kipimo cha HIV-1/2 chenye Mistari Mitatu, mstari wa T1 na T2 utakuwa na rangi nyekundu au shaba ikiwa kingamwili za VVU1 bna VVU 2 zinapatikana. HIi inamaanisha +Ve (VVU chanya)


Mwonekano wa mistari ya rangi nyingine katika kipimo

Wakati wa kupima, utakaposoma majibu ndani ya muda ulioandikwa na mtengenezaji wa kipimo ( mara nyingi ndnai ya dakika 10 hadi 20 unaweza kuona mistari yenye rangi tofauti na zilizotajwa hapo juu. Mfano kuonekana kwa mstari wenye rangi nyekundu kwenye mstari wa kudhibiti (C) (kama kwenye picha ya kipimo D hapo juu), na mistari miwili mingine ambayo ina rangi nyeupe au rangi ya maji kwenye T1 na T2. Kutokea kwa mistari hii haimaanishi kuwa kuna maambukizi kwa kuwa mistari hii kwa kawaida itaonekana na humaanisha kuwa eneo hilo ndipo sehemu ambayo kipimo kingechora kama kuna maambukizi.


Baadhi ya nyakati kipimo kinaweza kuongeza mistari mingine ya ziada yenye rangi nyekundu au shaba katika eneo ambalo haikuwepo awali baada ya kusoma, majibu haya ya wakati huu huwa si sahihi endapo yamesomwa nje ya muda ulioonyeshwa na kipimo.


Endapo una wasiwasi na majibu yako, unapaswa kurudia kipimo na kusoma ndani ya muda au kutumia kipimo kingine cha HIV unigold.Pia unashauriwa kuwasiliana na daktari wako kwa maelezo zaidi na tafsiri.


Wapi unaweza kupata maelezo zaidi

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu kipimo hiki katika makala zifuatazo. Unaweza kubofya ili kusoma zaidi;


Rejea za mada hii:

  • Standard Diagnostics, Inc. SD Bioline HIV-1/2 3.0 Rapid Test. Imechukuliwa 03.04.2025 kutoka: https://www.sdi.co.kr

  • World Health Organization (WHO). HIV Testing and Counselling. Imechukuliwa 03.04.2025 kutoka: https://www.who.int

  • Centers for Disease Control and Prevention (CDC). HIV Testing Overview. Imechukuliwa 03.04.2025 kutoka: https://www.cdc.gov

  • Ahmad SN, Khan MA, Ahmad T. Evaluation of diagnostic accuracy of SD Bioline HIV-1/2 Rapid Test in clinical settings. J Virol Methods. 2012;186(1):28-34.

  • International Journal of STD & AIDS. Evaluation of SD Bioline HIV 1/2 Rapid Test Performance in Field Settings. Int J STD AIDS. 2013;24(12):958-63.

  • Lynskey MT, De Vooght L. Advances in HIV Testing and Diagnosis: A Focus on Rapid Tests. Clin Microbiol Rev. 2014;27(2):315-31.

14 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page