Homa ya manjano
Imeandaliwa na ULY-Clinic
Utangulizi
Homa ya manjano ni nini?
Homa ya manjano au homa ya njano ni ugonjwa unaosabababishwa na kirusi cha manjano. Unaweza pata maambukizi ya homa ya manjano endapo utang’atwa na mbu jike mwenye jina la anopheles aegypt na Haemogogus hasa kama unaishi Barani Afrika au umesafiri kwenda Amerika kusini.
Baada ya kung’atwa na mbu mwenye kirusi, inakadiliwa kuchukua siku 3 hadi 6 kabla ya kupata dalili na baada ya dalili kutokea itachukua siku 3 hadi 4 ugonjwa kupotea.
Dalili za wastani ya homa ya manjano ni zinajhusisha homa, maumivu ya kichwa, kichefuchefu na kutapika, baadhi ya watu hupata dalili kali zinazoashiria uhalibifu kwenye ogani mbalimbali ndani ya mwili kama moyo, ini na figo na damu. Wagonjwa wenye dalili kali asilimia zaidi ya 50 hufa na ugonjwa wa homa ya manjano.
Matibabu ya homa ya manjano hulenga kutibu dalili tu, endapo utaweza kupata chanjo pia ni vema maana utakuwa umepata kinga ya ugonjwa huu.
Vidokezo muhimu kuhusu homa ya njano kutoka WHO
-
Zaidi ya asilimia 50 ya walioambukizwa, watapoteza uhai kama wasipopata tiba kutokana na homa ya manjano
-
Kila mwaka inakadiliwa kwamba wagonjwa laki mbili (200,000) wanapatikana na 30,000 hufa kila mwaka na asilimia 90 ya vifo hutokea afrika kutokanana homa ya manjano
-
Kirusi hiki kwa wastani huishi katika maeneo ya ukanda wa hari wa afrika na latini amerika, ambapo kuna watu zaidi ya ilioni 900
-
Kiwango cha maambukizi ya homa ya manjano kimeongezeka kwa miongo miwili iliyopita kutokana na kutopata chanjo ya kinga ya virusi hawa, ufyekaji misitu, kutokea kwa miji, shughuli za kusafili au uhamaji na abadiliko yahali ya nchi
-
Hakuna matiabu maalumu ya homa ya manjano,matibabu huhusihs kutibu dalili tu na hulenga kuondoa dalili na kumpa mgonjwa kujisikia vyema
-
Chanjo dhidi ya homa ya manjano ni ya umuhimu katika kukinga homa yamanjano, chanjo huwa salama na bei ndogo na hukinga kwa kiwango kikubwa. Kwa kupata chanjo moja tu inamkinga mtu dhidi ya ugonjwa wa homa ya manjano kwa zaidi ya miaka 30. Na mara anapopata chanjo huanza kumkinga mtu kwa asilimia 80 hadi 99 ndani ya siku 10 na kwa asilimia 100 ndani ya siku 30