top of page

Dalili na viashiria bonyeza herufi ya kwanza kusoma zaidi

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [#]

Mwandishi:

Dkt. Benjamin M, MD

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

28 Machi 2020 11:42:24

Chakula cha presha ya kupanda

Chakula cha presha ya kupanda

Kabla hatujaanza kuangalia vyakula vya watu wa haipatensheni ni vyema kujua kuhusu shinikizo la damu la juu ama Haipatensheni kwa ufupi,unaweza kusoma zaidi kuhusu shinikizo la damu la juu sehemu nyingine kwenye tovuti hii.


Haipatensheni kwa jina jingine hufahamika kwa jina la shinikizo la damu la juu, ambalo ni shinikizo la damu lililopita kiwango cha kawaida kinachofahamika kitiba.


Shinikizo la damu la juu huweza kuuchosha moyo kwa kuwa hufanya kazi kubwa kupita kiasi, moyo ukichoka unaweza kusababisha matatizo mbalimbali ndani ya mwili.


Watu wengi wamekuwa wakitumia neno presha kumaanisha shinikizo la damu la juu, kimsingi neno presha humaanisha shinikizo la damu, linaweza kuwa la kawaida au la juu au la chini, hivyo ni vema kutumia neno shinikizo la damu la juu au haipatensheni kumaanisha kuongezeka kwa presha kwenye moyo kuliko kawaida.


Kitiba shinikizo la damu limegawanyika sehemu mbili ambazo ni shinikizo la damu la sistoliki na shinikizo la damu la dayastoliki


Aina hizi zimeelezewa kiundani sehemu nyingine kweney tovuti hii.


Umeshawahi kusikia au kuambiwa presha yako ni 120 kwa 60 au presha yako ya juu ni 120 na ya chini ni 60?

Namba hizi zinaendana na aina mbili za shinikizo la damu zilizokweishwa tajwa, namba ya juu(120) ni shinikizo la damu la sistoliki na namba ya chini(60) ni shinikizo la damu la dayastoliki. Ni muhimu kujua kuhusu namba zote endapo unapima shinikizo la damu.


Mtu husemekana kuwa ana shinikizo la damu endapo shinikizo la damu la sistoliki limezidi 139 na shinikizo la damu la dayastoliki limezidi 79 (Soma Zaidi kuhusu shinikizo la damu sehemu nyingine ya tovuti hii)


Vihatarishi


Vihatarishi vya kupata shinikizo la damu la juu ni;


  • Historia ya familia: Kuwa kwenye Familia yenye mgonjwa wa haipatensheni au ambayo ishawahi kuwa

  • nayo ni rahisi kupelekea wanafamilia wengine kupata

  • Uzito kupita kiasi

  • Kutumia kwa wingi vyakula vyenye chumvi nyingi

  • Kutumia vyakula vya mafuta

  • Kutokufanya mazoezi

  • Kunywa pombe kupita kiasi

  • Kuvuta Sigara


Ni vyakula gani ni vizuri kutumiwa na watu wenye shinikizo la damu la juu?


Vifuatavyo ni vyakula vinavyoshauriwa kwa watu wenye shinikizo la juu la damu na wale ambao hawana shinikizo la damu


Kula matunda kwa wingi

Kula matunda makavu na Juisi ya matunda kwa wingi isiyokuwa na sukari hii hupelekea kuongeza Madini ya Potasiamu na Magniziamu pamoja na nyuzinyuzi kwa wingi . madini ya potasiamu huwa na sifa za kupunguza shinikizo la damu. Madini haya hupatikana kwenye vyakula kama ndizi n.k. soma maelezo Zaidi kuhusu madini ya potasiamu na magniziamu


Kula mboga za majani kwa wingi

  • Tumia

  • Mboga za majani zilizopikwa

  • Juisi ya mboga za majani


Kwanini? Mboga za majani huongeza kwa wingi madini ya Potasiamu , Magneziamu na nyuzinyuzi


Kula vyakula visivyo na Mafuta kwa wingi

Mfano, Maziwa na jibini kwa wingi


Kwanini? husaidia kuongeza madini ya kalisiamu na protini kwa wingi mwilini


Kula vyakula visivyokuwa na chumvi kwa wingi

Mgonjwa wa haipatensheni anapaswa kutumia chumvi isiyopungua miligramu 2400 kwa siku,

kiwango hiki kinapaswa kutumika kwa watu wasio na haipatensheni.

Kwanini? Kuacha kutumia chumvi kabisa hakushauriwi kwani huweza kuleta matatizo mwilini.


Kula vyakula visivyo na sukari kwa wingi

Mfano kutumia unga nafaka zisizokobolewa mfano mtama, mahindi n.k,


Kunywa vinywaji visivyo na sukari kwa wingi

Juisi za mgonjwa wa haipatensheni zinapaswa zisiwe na sukari, Hivyo mgonjwa anapaswa kuepuka

kunywa Soda pamoja na juisi za viwandani zenye sukari.


Kwanini? vyaakula vyenye sukari na kalori nyingi huongeza uzito na hatari na magonjwa ya mishipa ya damu. Tumia chakula kulingana na mahitaji ya mwili au kwa kuzingatia ushauri wa daktari.


Kula nyama isiyo na Mafuta na zile yenye rangi nyeupe kama nyama ya kuku batamzinga, nyama nyekundu kama ya nguruwe iliyoondolewa.


Kuepuka kunywa pombe kupita kiasi

Kunywa pombe ni hatarishi kwa watu wenye shinikizo la damu la juu. Soma kuhusu kiwango cha pombe

kinachotakiwa kwa mwanamme na mwanamke sehemu nyingine kwenye tovuti hii.


Mambo mengine muhimu ya kufanya


Mbali na chakula pia fanya mambo yafuatayo;


Fanya mazoezi kwa ratiba maalumu

Mfano Kutembea na kuendesha baiskeli kwa dakika 30 hadi 45 kwa muda wa siku 3 hadi 4 za wiki, kama ukiweza fanya kila siku ni vizuri Zaidi. Mazoezi yanapaswa kufanywa na watu wote siowagonjwa tu. Jifunze Zaidi kuhusu mazoezi kwenye mada ya mazoezi na chakula


Acha kuvuta Sigara

Uvutaji wa sigara huongeza uharibifu kwenye mishipa ya damu


Punguza Uzito

Kama uzito wako ni mkubwa au una obeziti na shinikizo la juu la damu , njia mojawapo nzuri ya kupunguza shinikizo hilo kupunguza uzito kiwango kinachofaa kiafya. Kupunguza uzito kunaweza kupunguza shinikizo la dama kiasi kwamba kusiwe na uhaja wa kutumia dawa. Wasiliana na daktari wako kwa ushauri Zaidi kuhusu kupunguza uzito na shinikizo la damu.


Athari za presha ya kupanda



Athari hizi zimegawanyika katika makundi yafuatayo :


Moyo

Shinikizo la juu la damu hufanya moyo kufanya kazi zaidi kupita uwezo wake,Hivyo hupelekea misuli ya moyo kupanuka na kuwa mikubwa, hali hii ikitokea hupelekea moyo kuwa dhaifu na kushindwa kufanya kazi ipasavyo


Mishipa ya ateri

Shinikizo la juu la damu hupelekea mishipa hii ya damu kuwa mikubwa na kupasuka kutokana na presha kuwa juu, hii ni hali ya hatari sana na hupelekea kifo


Ubongo

Shinikizo la juu la damu hupelekea Kiharusi(stroku) endapo mshipa ya damu itapasuka au kuziba kwenye ubongo


Figo

Kazi mojawapo ya figo ni kusawazisha kiwango cha maji na madini yaliyo kwenye damu ili kuhakikisha kuwa shinikizo la damu linadhibitiwa. Presha inapokuwa kubwa kwenye mwili hupelekea kuharibu mfumo huu wa Figo, na hivyo huanza leta matatizo mengine mwilini.


Macho

Shinikizo la juu la damu huweza kuathiri macho, mishipa ya damu kwenye macho huwa ni midogo na huweza kupasuka au kuviliavu damu nje ya mishipa ya damu hivyo kupelekea upofu au kuvimba kwa retina.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasilianane na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga namba za simu  au kubonyeza sehemu imeandikwa "Pata tiba" chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

21 Julai 2023 16:20:09

Rejea za mada hii;

1.Kitabu kinaitwa Davidson’s Essential of medicine Edited by Alastair Innes Ukurasa wa 242 -245

2.Encyclopedia of foods a guide to Health Nutrition Ukurasa 53-57, ISBN-13: 978–0–12–219803–8

3.What is high blood pressure? American Heart Association. http://www.heart.org/HEARTORG/Conditions/HighBloodPressure/GettheFactsAboutHighBloodPressure/What-is-High-Blood.Pressure_UCM_301759_Article.jsp#.WrqtReR1rcs. Imechukuliwa 28.03.2020

4.Hypertensive crisis: When you should call 9-1-1 for high blood pressure. American Heart Association.http://www.heart.org/HEARTORG/Conditions/HighBloodPressure/GettheFactsAboutHighBloodPressure/Hypertensive-Crisis-When-You-Should-Call-9-1-1-for-High-Blood-Pressure_UCM_301782_Article.jsp#.WrqtoOR1rcs. Imechukuliwa 28.03.2020

5.Hypertension in adults: Screening and home monitoring. U.S. Preventive Services Task Force. http://www.uspreventiveservicestaskforce.org/Page/Document/RecommendationStatementFinal/high-blood-pressure-in-adults-screening. Imechukuliwa 28.03.2020

6.Thomas G, et al. Blood pressure measurement in the diagnosis and treatment of hypertension in adults. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 28.03.2020

7.Blood pressure monitoring kiosks aren't for everyone. U.S. Food and Drug Administration. http://www.fda.gov/forconsumers/consumerupdates/ucm402287.htm. Imechukuliwa 28.03.2020

bottom of page