top of page

Dalili na viashiria bonyeza herufi ya kwanza kusoma zaidi

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [#]

Mwandishi:

Dkt. Mercy M, M.D

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

9 Aprili 2020 20:38:44

Chakula cha tezi dume

Chakula cha tezi dume

Tezi dume kwa jina la kitiba Prostate ni miongoni mwa tezi muhimu katika mfumo wa uzazi wa mwanaume, tezi dume iko chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Mrija wa yurethra umepita katikati ya tezi hii. Kazi kuu ya tezi ya prostate ni kuzalisha maji ya alkalaini ambayo huchangia kiasi cha wastani wa asilimia 70 ya ujazo shahawa. Majimaji haya husaidia kulainisha na kulisha manii. Hata hivyo shahawa zinapotoka na kuingia ukeni wakati wat endo, maji maji haya ya alkalaini husaidia kupunguza kiasi cha aside ukeni.


Saratani ya tezi dume mara nyingi huwa haina dalili mpaka uvimbe wa saratani usababishe kukojoa damu na kuziba kwa njia ya mkojo. Utambuzi wa saratani hii hushauriwa kwa kipimo cha kucheki tezi ya prostate kwa kutumia kidole kinachozamishwa kwenye njia ya haja kubwa (DRE), kufanya kipimo cha antigeni maalumu za prostate kwenye dam una kufanya kipimo cha yultrasaundi ya tezi.


Saratani huweza kuwa na mwisho mzuri endapo itagunduliwa kwenye hatua za awali kabisa. Matibabu huhusisha kuondolewa tezi ya prostate, tiba mionzi na matibabu saidizi kama kupewa homoni na kemotherapi.



Vyakula muhimu kwa wagonjwa wa saratani ya tezi dume


Katika tiba ya mgonjwa wa saratani ni muhimu kuzingatia suala la lishe kwani kutokana na ongezeko la seli za saratani, ongezeko la mahitaji ya nishati na virutubisho vingine huongezeka pia. Mgonjwa anapaswa kula mlo kamili unaoshauriwa kiafya. Vyakula vilivyoorodheshwa hapa chini ni muhimu kwa wagonjwa wa saratani mbalimbali haswa tezi dume.


Soya

Maharage ya soya yanapatikana katika kundi la vyakula jamii ya kunde, kunde jamii ya soya ni chanzo kizuri cha protini ambayo ni muhimu kwa ajili ya kujenga mwili na kuponya seli zilizoharibika. Soya ina kemikali iitwayo protease inhibitor ambayo kimsingi huzuia saratani na kupunguza ukuaji wa uvimbe


Nyanya

Nyanya ni tunda lenye kemikali za lycopene na beta-carotene. Lycopene huzui na kuharibu kemikali zinazopelekea kupata saratani . Kula nyanya husaidia kuzuia ukuaji wa saratani ya tezi dume. Mgonjwa anaweza kunywa supu ya nyanya au kula kachumbali ili kuipata lycopene na virutubisho vingine.


Mboga za majani

Mboga za majani kama brokoli, spinachi, figiri, kale, chainizi na kabeji hutupatia vitamini na madini yanayo imarisha kinga ya mwili kupambana na magonjwa ikiwemo saratani. Tafiti kadha wa kadha zimeonesha kuwa matumizi ya mboga za majani hupunguza kasi ya ukuaji wa saratani ya tezi dume na kupunguza uwezekano wa kupata ikiwa mwanaume atatumia vizuri kabla hajapatana saratani ya tezi dume.


Komamanga

Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa tunda hili lina kemikali iitwayo anthocyanin ambayo huharibu seli za saratani.


Machungwa

Machungwa, machenza na malimau yanakiwango kikubwa cha vitamin C, beta-carotene na provitamin A ambazo kwa pamoja huimarisha kinga ya mwili na kupambana na saratani mbalimbali ikiwemo ya tezi dume.


Pilipili

Pilipili zina flavonoids, vitamini A na vitamini C ambazo kwa kwa pamoja hupambana saratani. Matumizi ya mara kwa mara hupunguza hatari na uwezekano wa kupata saratani.


Parachihchi

Haya ni matunda yenye mafuta mepesi yasiyo ganda ambayo husaidia kusawazisha rehemu(cholestrol) na kuiweka katika msawazo mwilini, pia maparachichi ya vitamini E ambayo huzuia ukuaji wa saratani ya tezi dume na kupunguza hatari ya kupata saratani ya tezi dume.


Maziwa na mazao ya maziwa

Mgonjwa atumie kiwango cha wastani cha maziwa, matumizi makubwa ya maziwa na mazao ya maziwa huongeza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume, pia huongeza ukuaji na utawanyikaji wa saratani ya tezi dume. Mgonjwa asitumie Zaidi ya lita 1.6 kwa siku.


Nyama

Mgonjwa apunguze matumizi ya nyama zilizosindikwa na kuchakatwa viwandani. Mgonjwa atumie chakula chenye kiwango kidogo cha nyama, sehemu kubwa iwe matunda na mbogamboga. Mgonjwa atumie kiwango kidogo cha nyama nyekundu(nyama ya ng’ombe, mbuzi na kondoo). Ili kupata protini mgonjwa anaweza kula kunde kama maharage na njugu.


Mafuta

Mwili huhitaji mafuta ili uweze kufanya kazi vyema, mafuta hayo yanapoliwa kwa wingi yanaweza kupelekea uzito uliokithiri kisha kupelekea ukuaji wa saratani ya tezi dume. Mgonjwa mwenye saratani ya tezi dume wanapaswa kuacha kutumia mafuta yatokanayo na wanyama(animal fat) mfano korie na kuanza kutumia mafuta yatokanayo na mimea(vegetable oils) kama sundrop au mafuta ya alizeti na mengineyo mengi. Matumizi ya kiasi ya mafuta yatokanayo na mimea hupunguza kukua na kutawanyika kwa saratani ya tezi dume.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasilianane na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga namba za simu  au kubonyeza sehemu imeandikwa "Pata tiba" chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

21 Julai 2023 16:18:59

Rejea za mada hii;

1.MSD manual professional version. J. Ryan Mark , MD etal .Prostate cancer. https://www.msdmanuals.com/professional/genitourinary-disorders/genitourinary-cancer/prostate-cancer. Imenukuliwa 08.04.2020

2.Levi A Deters, MD etal.What is the main function of the prostate gland?https://www.medscape.com/answers/437359-90388/what-is-the-main-function-of-the-prostate-gland. Imechukuliwa 08..09.2020

3.Applegate CC, Rowles JL, Ranard KM, Jeon S, Erdman JW. Soy Consumption and the Risk of Prostate Cancer: An Updated Systematic Review and Meta-Analysis. Nutrients [Internet]. 2018 Jan 4. Imenukuliwa 08.04.2020

4.George D. Pamploma-Roger. Healthy Foods Toleo la kwanza la kiingeleza Januari 2013, Kurasa. 189, 361, 362,367 Imenukuliwa 08.04.2020

bottom of page