top of page

Dalili na viashiria bonyeza herufi ya kwanza kusoma zaidi

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [#]

Mwandishi:

Dkt. Sospeter B, MD

Mhariri:

Dkt. Salome A, MD

13 Desemba 2020 20:14:16

Kutoa mdudu sikioni

Kutoa mdudu sikioni

Mdudu kuingia masikioni ni jambo linaloweza kutokea kwa kila mtu. Muda muafaka huweza kuwa wakati umekaa mchana au wakati umelala usiku. Wadudu wanaoweza kuingia sikioni ni mbu, nzi, mende na wengine. Mdudu anaweza kuingia sikioni na akaishi muda mrefu au akafia ndani bila wewe kufahamu.


Makala hii imezungumzia huduma ya kwanza ya kuondoa mdudu sikioni.


Dalili za mdudu kuingia sikioni


Mdudu anapoingia sikioni hugusa ngoma ya sikio na hivyo huweza kuleta dalili zifuatazo;


 • Maumivu makali ya sikio

 • Hisia za sikio kuwa lina kitu kwa ndani

 • Kuvimba kwa sikio

 • Kutokwa na uchafu au majimaji masikioni

 • Kupungua kwa usikivu


Huduma ya kwanza ya kutoa mdudu sikioni


Endapo wewe, mtoto au nduu ameingiwa na mdudu sikioni fanya mambo yafuatayo ili kumtoa kama huduma ya kwanza;


 1. Mtulize ndugu na mwambie unaweza msaidia

 2. Usijaribu kumtoa mdudu kwa kuingiza kitu masikioni kama vile vijiti vyenye pamba kwa sababu utamsukuma ndani zaidi kisha kushindwa kutoka au kuharibu ngoma ya sikio

 3. Inamisha kichwa kwenye upade ambao mdudu ameingia, usipige pige kichwa bali unaweza kukitikisa tikisa huku umeinama ili kufanya mdudu atoke

 4. Kama huna matatizo yoyote ya sikio, na mdudu hachatoka kwenye hatua namba 3, tia mafuta ya kupikia au mafuta ya nazi kwenye sikio. Wakati wa kutia mafuta unaweza lalila upande ambao hakuna mdudu kisha imamisha kichwa kwenye upande mdudu alipo ili kufanya atoke, wakati huu tena tikisa kichwa huku umeinamia upande wa sikio lenye mdudu.

 5. Kumbuka unapotia mafuta kwenye sikio unafanya mdudu akose hewa na kufa

 6. Endapo mdudu amekufa na hatoki bado licha ya kutikisa na kuinamia upande mdudu alipo, chukua maji ya uvuguvugu kisha tia ndani ya sikio ili kumuondoa kwa presha

 7. Tumia bomba la sindano kusukuma maji kwa nguvu ndani ya sikio ili kuweza kumtoa. Fanya hivi kichwa kikiwa kimeinamia upande wa mdudu alipo

 8. Fanya hivi mara tatu hadi nne.


Wakati gani umasiliane na daktari wako?


Kama una mdudu sikioni wasiliana na daktari endapo;


 • Mdudu bado hatoki au huna uhakika kama bado yupo ndani ya sikio licha ya kufanya njia zote zilizo elezewa hapo juu.

 • Endapo sehemu ya mdudu bado imebaki ndani ya sikio

 • Endapo mtoto amepata dalili za maambukizi kwenye sikio ambazo ni homa au kutokwa na uchafu masikioni

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasilianane na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga namba za simu  au kubonyeza sehemu imeandikwa "Pata tiba" chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

21 Julai 2023 16:18:21

Rejea za mada hii;

1.Awad, A. H etal. ENT foreign bodies. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/m/pubmed/29619103/. Imechukuliwa 11.12.2020

2.Craig, S. S. etal. Removal of ENT foreign bodies in children. Emergency Medicine Australasia. https://onlinelibrary.wiley.com/doi/pdf/10.1111/1742-6723.12387. Imechukuliwa 11.12.2020

3.Insects in a Child's Ear. https://www.stanfordchildrens.org/en/topic/default?id=insects-in-the-ear-90-P02828. Imechukuliwa 11.12.2020

4.Insects in the ear. (n.d.). http://www.stanfordchildrens.org/en/topic/default?id=insects-in-the-ear-90-P02828. Imechukuliwa 11.12.2020

5.Olajide, T. G etal. Management of foreign bodies in the ear: A retrospective review of 123 cases in Nigeria. [Abstract]. ENT: Ear, Nose & Throat Journal, 90(11), E16–E19.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/22109927. Imechukuliwa 11.12.2020

bottom of page