top of page

Dalili na viashiria bonyeza herufi ya kwanza kusoma zaidi

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [#]

Mwandishi:

Dkt. Mercy M, M.D

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

28 Mei 2020 05:18:52

Matibabu ya kukosa usingizi

Matibabu ya kukosa usingizi

Insomnia ni tatizo endelevu linalosababisha mtu kushindwa kuanza kusinzia, kutodumu kwenye usingizi ama vyote viwili licha ya kupata fursa ya kulala ipasavyo. Kwa kukosa usingizi, mtu huyu kwa kawaida huamka hajihisi kuwa mpya , hali hii inasababisha kupunguza uwezo wa kufanya kazi wakati wa mchana.kukosa usingizi hakumalizi nguvu tu na hali yako, bali hudhuru afya na ubora wa maisha.


Usingizi kiasi gani unatosha hutegemea mtu moja na mwingine,mara nyingi watu wazima huhitaji masaa 7 hadi nane ya kulala.


Watu wengi pia walishawahi au watapata tatizo la kukosa usingizi kipindi Fulani katika maisha yao lakini huwa si endelevu lakini baadhi wanaweza kupata tatizo hili na kuwa endelevu. Kukosa usingizi kupo kwa aina mbili yaani aina ya kwanza na aina ya pili amabayo husababishwa na madawa au ugonjwa mwilini.


Huhitaji kutolala usiku, mabadiliko ya mambo Fulani katika maisha yako yanaweza kukusaidia kupata usigizi.


Matibabu


Kuwa na tabia ya kulala kiafya, tabia hii inahusisha mambo yafuatayo;


  • Oga maji ya uvuguvugu, soma kitabu au sikiliza muziki laini

  • Hakikisha umeweka vema eneo lako la kulala na litumie kwa kulala tu au kufanyia mapenzi na sio shughuli zingine

  • Lala kila siku muda ule ule ikiwa pamoja na siku za mapumziko

  • Fanya mazoezi kwa ratiba maalumu, mazoezi hupelekea kupaa usingizi kirahisi

  • Angalia dawa unazokunywa kama zinasababisha kukosa usingizi na wasiliana na daktari wako endapo unaweza kuzitumia wakati wa mchana

  • Zuia kula vyakula vyenye kahawa na usitumie nikotini

  • Zuia kula vinywaji na mlo mzito wakati wa kulala

  • Zuia kulala mara kwa mara

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasilianane na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga namba za simu  au kubonyeza sehemu imeandikwa "Pata tiba" chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

21 Julai 2023 16:18:59

Rejea za mada hii;


1. What is insomnia? National Heart, Lung, and Blood Institute. https://www.nhlbi.nih.gov/health/health-topics/topics/inso#. Imechukuliwa 28.05.2020

2. Insomnia fact sheet. WomensHealth.gov. http://womenshealth.gov/publications/our-publications/fact-sheet/insomnia.html. Imechukuliwa 28.05.2020

3. Sleep-wake disorders. In: Diagnostic and Statistical Manual of Mental Disorders DSM-5. 5th ed. Arlington, Va.: American Psychiatric Association; 2013. http://www.psychiatryonline.org. Imechukuliwa 28.05.2020

4. Sleep disorders: The connection between sleep and mental health. National Alliance on Mental Health. http://www.nami.org/Learn-More/Mental-Health-Conditions/Related-Conditions/Sleep-Disorders. Imechukuliwa 28.05.2020

5. Approach to the patient with sleep or wakefulness disorder. Merck Manual Professional Version. http://www.merckmanuals.com/professional/neurologic-disorders/sleep-and-wakefulness-disorders/approach-to-the-patient-with-a-sleep-or-wakefulness-disorder. Imechukuliwa 28.05.2020

6. Insomnia. Natural Medicines. https://naturalmedicines.therapeuticresearch.com/databases/medical-conditions/i/insomnia.aspx. Imechukuliwa 28.05.2020

7. Sleep and aging. National Institute on Aging. https://nihseniorhealth.gov/sleepandaging/aboutsleep/01.html. Imechukuliwa 28.05.2020

8. Kliger B, et al. Complementary/integrative therapies that work: A review of the evidence. American Family Physician.

9. Bonnet MH, et al. Clinical features and diagnosis of insomnia. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 28.05.2020

bottom of page