top of page

Dalili na viashiria bonyeza herufi ya kwanza kusoma zaidi

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [#]

Mwandishi:

Dkt. Benjamin M, MD

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

23 Machi 2020 10:32:26

Matibabu ya maumivu ya Hedhi

Matibabu ya maumivu ya Hedhi

Maumivu yoyote yale ya hedhi husababishwa na kemikali zinazoitwa "prostaglandin" na "leukotriene" katika mfumo wa uzazi ambazo ni kawaida kuzalishwa wakati wa yai kutengenezwa na kutoka kwenye ovari.


Kiwango cha kemikali hizi huongezeka sana kipindi cha yai kutolewa kutoka kwenye ovari na wakati ukuta wa ndani ya mfuko wa kizazi unapoanza kubomoka kila mwezi.


Kemikali hizi husababisha mfuko wa uzazi kubana na kuachia ili kutoa kuta zilizojengwa kwa muda wa siku 28 au 31 endapo tu yai lililotoka kwenye ovari halikuchavushwa.


Baadhi ya matibabu ambayo unaweza kufanya nyumbani ili kupunguza au kuondoa maumivu ya hedhi ni pamoja na;


Kufanya Mazoezi kama tiba ya maumivu ya hedhi

Tafiti zinaonyesha kuwa kuushughulisha mwili kwenye kazi za kutoa jasho jingi au mazoezi makali huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza maumivu ya hedhi. Soma zaidi kwenye mada za mazoezi katika sehemu ya chakula na mazoezi


Kutumia maji ya moto kama tiba ya kupunguza maumivu ya hedhi

Kujiloweka kwenye sinki la maji ya moto ambayo hayaunguzi mwili k, au kutumia chupa ya maji moto kujikanda kwa kutumia chupa ambayo imewekewa maji ya moto chini ya kitovu kwa muda wa nusu saa hadi saa limoja kunapunguza kubana kwa misuli ya nyonga na maumivu ya hedhi. Njia hii inaweza kupunguza maumivu kwa kiasi kikubwa kama mtu aliyetumia dawa za kuondoa maumivu.


Matumizi ya dawa virutubisho kama tiba ya maumivu ya hedhi

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa Vitamin E, Mafuta ya Omega 3, vitamin B1, vitamin B6 na madini ya magnesium hupunguza sana maumivu ya hedhi.


Soma zaidi kuhusu Vitamini hizi na Madini kwenye sehemu ya Vitamin na Madini kwa uelewa zaidi


Kujikinga na matumizi ya pombe kama tiba ya maumivu makali ya hedhi

Pombe na tumbaku husababisha maumivu ya hedhi kuwa makali Zaidi.


Kupunguza msongo wa mawazo kama tiba ya maumivu ya hedhi

Msongo wa mawazo unamadhara katika saikolojia ya mt una huongeza hatari ya kupata maumivu ya hedhi yaliyo makali.


Matibabu mbadala ya maumivu ya hedhi


Matibabu ya akupankcha

Huhusisha kuchomwa na kijisindano kidogo sana kinachopita kwenye Ngozi na kwenda kwenye eneo ambalo maumivu hayo yanatokea haswa kwenye mishipa ya fahamu


Matibabu ya umeme (TENS)

Kwa kutumia kifaa maalumu cha kupitisha umeme na kuingiza kwenye mishipa ya fahamu kupitia. Ngozi kunaweza kupunguza maumivu ya hedhi. Umeme huu huamsha mishipa ya fahamu na kuiongezea uwezo wa kuitikia Zaidi maumivu. Mwitikio wa mishipa hii kwenye maumivu husababisha kemikali asili za mwili zinazoitwa endofini kutolewa na mwili. Kemikali hii huwa ni dawa asilia ya maumivu iliyopo ndani ya mwili.


Dawa asilia zinazotibu maumivumakali ya hedhi

Zipo dawa kadhaa za mitishamba ambazo zinaweza kupunguza maumivu ya hedhi, wasiliana na wataalamu wa ULY CLINIC au soma zaidi kwenye mada ya Dawa asilia kwa maelezo zaidi


Kanda tumbo

Masaji hufanyika husababisha mgandamizo kiasi kwenye Ngozi eneo lenye maumivu, mgandamizo huu huweza kupunguza maumivu ya hedhi, hata hivyo hakuna tafiti za kutosha zilizofanyika kuthibitisha hili lakini kutokana na zile zilizofanyika njia hii imeonekana kupunguza maumivu kwa wanaotumia ukilinganisha na wanawake ambao walikuwa hawatumii njia hii.


ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasilianane na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga namba za simu  au kubonyeza sehemu imeandikwa "Pata tiba" chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

21 Julai 2023 16:20:09

Rejea za mada hii;

1.Frequently asked questions. Gynecologic problems FAQ046. Dysmenorrhea: Painful periods. American College of Obstetricians and Gynecologists. https://www.acog.org/Patients/FAQs/Dysmenorrhea Painful-Periods. Imechukuliwa 23.03.2020

2.Harada T. Dysmenorrhea and endometriosis in young women. Yonago Acta Medica. 2013;56:81. Period pain: Overview. PubMedHealth. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmedhealth/PMH0072508/. Imechukuliwa 23.03.2020

3.Smith RP, et al. Primary dysmenorrhea in adult women: Clinical features and diagnosis. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 23.03.2020

4.Dysmenorrhea. Merck Manual Professional Version. http://www.merckmanuals.com/professional/gynecology-and-obstetrics/menstrual abnormalities/dysmenorrhea#v1062408. Imechukuliwa 23.03.2020

5.Smith RP, et al. Treatment of primary dysmenorrhea in adult women. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 23.03.2020

bottom of page