Mwandishi:
Dkt. Benjamin M, MD
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD
22 Machi 2020, 21:59:54

Muda wa kutoa nyuzi za upasuaji
Hili ni swali linaloulizwa na watu wengi ambao wamefanyiwa upasuaji na wale wanaouguza wagonjwa wa upasuaji. Katika makala hii utajibiwa swali hili kitaalamu.
Nyuzi za kidonda, ni nyuzi laini zinazoshonwa kwenye kidonda ili kukutanisha kuta za kidonda ili kiweze kupona. Nyuzi zinaweza kuwa za kuyeyuka au zisizo za kuyeyuka, nyuzi za kuyeyuka mara nyingi huyeyuka ndani ya wiki 4 hadi 8. Nyuzi za kuyeyuka huwa hazihitaji kutolewa kwenye kidonda kwa kuwa huyeyuka zenyewe.
Nyuzi za kuyeyuka hutumika kushona maeneo ya kinywa, ulimi, maeneo ya viungo vya siri au vidonda vinavyozama ndani ya nyama.
Nyuzi za nailoni na zingine ambazo si za kuyeyuka zinapaswa kuondolewa na mtaalamu wa afya.
Kidonda cha kubanwa na stepla
Kidonda cha kubanwa na stepla, ni kidonda kinachobanwa kwa mashine ndogo ya mkono inayotumia pini maalumu kwa ajili ya kubana vidonda. Muda wa pini hizi kukaa mwilini hutegemea aina ya kidonda, mahari kidonda kilipo na aina ya mgonjwa.
Pini hizi hutolewa na daktari ofisini kwake au hospitali. Kidonda cha kuzibwa na pini kinaweza kuwa na rangi nyekundi kwenye maeneo pini zilipopita. Endapo wekundu unaongezeka kwa jinsi siku zinavyokwenda inaweza kumaanisha dalili za maambukizi kwenye kidonda.
Kidonda kilichofungwa kwa Steri strips
Steri strips ni bandeji inayotumika kukutanisha kingo za kidonda cha upasuaji. Bandeji hizi huwekwa mbali mbali kuacha nafasi ili kidonda kitoe majimaji yanayotoka ndani ya kidonda. Kidonda chenye bandeji za steri strips kinatakiwa kuachwa kuwa kikavu ndani ya masaa 24 kabla ya kugusa maji. Huhitaji kwenda kwa daktari kutoa bandeji hizi bali acha zitanyofoka zenyewe ndani ya siku 7 hadi 10.
Kidonda kilichofungwa na gundi
Gundi ya kufunga kidonda kama vile dermabond huweza tumika kufunga vidonda. Daktari ataweka gundi kiasi kwenye mipaka ya kidonda pamoja na filimu ili kukinga kidonda kisipatwe majimaji. Utatakiwa kuacha filimu hiyo ikae kwenye kidonda mpaka itakapoanguka yenyewe baada ya siku 5 hadi 10.
Muda wa kutoa nyuzi ya kidonda
Aina ya kidonda na siku ambazo utakaa mpaka nyuzi au pini kutolewa
Kidonda cha usoni- nyuzi zitatolewa baada ya siku 3 hadi 5
Kidonda cha juu ya kichwa- nyuzi zitatolewa kuanzia siku 7 hadi 10
Kidonda kwenye mikono- nyuzi zitatolewa ndani ya siku 7 hadi 10
Kidonda kwenye kiwiliwili- nyuzi zitatolewa kuanzia siku 10 hadi 14
Kidonda kwenye mikono au miguu - nyuzi zitatolewa siku 10 hadi 14
Kidonda kwenye kiganja cha mkono na kiganja cha mguu- nyuzi zitatolewa kuanzia siku 14 hadi 21
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasilianane na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga namba za simu au kubonyeza sehemu imeandikwa "Pata tiba" chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
21 Julai 2023, 16:20:09
Rejea za mada hii;
1. Surgical site infections. John Hopkins University. www.hopkinsmedicine.org/healthlibrary/conditions/surgical_care_site_infections_134,144. Imechukuliwa machi 22.2020
2. Weller R, Hunter H, Mann MW. Clinical dermatology. Toleo la 5. Hoboken, NJ:Wiley-Blackwell; Imechukuliwa mach 22.2020.
3.Sarvis C. Postoperative Wound care. Nursing 2006. 2006; 36(12):56-57
4.U.S. Department of Jealth and Human Services. Agency for Healthcare, Research and Quality (AHRQ). Surgical site infection: prevention and treatment of surgical site infection www.guidline.gov/content.aspx? id=13416. Imechukuliwa mach 22.2020
5.National Instituete for health and Care Excellence (NICE)
6. Surgical site infections: prevention and treatment. October 2008; www.nice.org.uk/guidence/cg74. Imechukuliwa machi 22.2020 murphy PS, Evans GR. Advances in
10.1155/2012/190436.Epub2012 March 22.