top of page

Dalili na viashiria bonyeza herufi ya kwanza kusoma zaidi

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [#]

Mwandishi:

Dkt. Sospeter B, MD

Mhariri:

Dkt. Salome A, MD

6 Julai 2021 19:16:05

Tiba ya kuvia damu kutokana na majeraha

Tiba ya kuvia damu kutokana na majeraha

Kwa kawaida, kuvia kwa damu chini ya ngozi huisha bila matibabu ndani ya siku 10 hadi 14 kwa mtu mwenye afya njema. Baadhi ya watu, damu iliyovia huweza kuendelea kwa muda mrefu hata kama wana afya njema.


Kuvia damu chini ya ngozi kutokana na majeraha mbalimbali kama kuanguka, kupigwa au madhara ya matibabu huweza harakiswa uponyaji wake kwa dawa, upasuaji au matibabu ya nyumbani. Hata hivyo baadhi ya sehemu za mwili zinaweza kubaki na alama endapo damu iliyovia ni nyingi


Nini cha kufanya ili kuharakisha damu iliyovia kupotea?


Muda mfupi baada ya kupata majeraha kwenye ngozi, mwili huamsha mfumo wa kinga ili kufanya kazi yake ya kufyonza na kuondoa damu hiyo mara moja. Mchakato huu huchukua muda mrefu hivyo damu iliyovia huchelewa kuisha.


Endapo mwathirika wa tatizo hili atapata matibabu mapema zaidi, anaweza kupunguza muda wa kupotea kwa damu iliyovia.


Kupata matibabu kwa njia zifuatazo ndani ya masaa 48 kufuatia kuvia kwa damu chini ya ngozi huharakisha kutokea kwa uponyaji;


Kukanda eneo lililovia damu kwa barafu- hufanya mishipa ya damu isinyae na hivyo damu kutoendelea kuvia

Endapo muda umepita zaidi ya masaa 48 tumia maji ya moto kukanda eneo lenye mvio wa damu- kufanya hivyohusaidia kuongeza mzunguko wa damu ambao utaondoa damu iliyovia.

Kupaka mafuta ya vitamin K

Matumizi ya bromelain


Kama huwezi pata dawa zakuvia damu ufanyaje?


  • Endapo huwezi pata dawa zilizoorodheshwa hapo juu unaweza kutumia vitu mbadala kama;

  • Kupaka mafuta ya arnica angalau mara mbili kwa siku au

  • Paka maji ya alovera yaliyoandaliwa muda si mrefu. Paka mara mbili hadi tatu kwa siku kwenye eneo lenye mvio wa damu

  • Kunywa vidonge vya vitamin C. Kunywa vidonge au kupaka krimu au mafuta yenye vitamin C husaidia kuondoa michomo kutokana na kinga ya mwili hivyo kuharakisha uponyaji

  • Kula nanasi kwa wingi katika mlo wako au paka maji yake. Dawa bromelain imetengenezwa kutoka kwenye kiini cha nanasi ambayo huharakisha uponyaji kwa kuzuia michomo inayotokana na kinga za mwili.

  • Kula matunda na mboga za majani kwa wingi ili kupata virutubisho vingine muhimu kwa ajili ya mwili wako kufanya kazi vema ya kuondoa majeraha.

  • Usisahau kutumia vya kula jamii ya protini ambayo ni muhimu kurejesha tishu zilizokufa kwa majeraha. Tumia protini kutoka kwenye nyama nyeupe kama inavyoshauriwa kwenye tafiti mbalimbali.


Matibabu ya uvimbe wa kuvia damu


Kuvia damu nyingi kuliko kawaida husababisha uvimbe chini ya ngozi wenye jina la hematoma. Hematoma huonekana kama uvimbe wenye rangi nyeusi au zambarau chini ya ngozi wenye uwezo wa kuleta mgandamizo sehemu ulipotokea. Matibabu ya hematoma hufanywa na mtaalamu wa afya kwa kufyonzwa damu iliyovia kwa kutumia sindano.


Wakati gani uonane na daktari endpo umevia damu kwenye ngozi?


Kama umevia damu kutokana na majeraha ya kuanguka, kupigwa au matibabu, onana na daktari wako haraka endapo;


  • Kudumu kwa maumivu licha ya kupat amajeraha kidogo

  • Uvimbe umetokea kwenye eneo lililovia damu

  • Unapata mkojo wenye damu

  • Unapata kinyesi cheusi au chenye damu

  • Unapata maumivu ya kichwa au umepoteza fahamu ndani ya masaa 24

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasilianane na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga namba za simu  au kubonyeza sehemu imeandikwa "Pata tiba" chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

21 Julai 2023 16:18:21

Rejea za mada hii;

1. Brennan C. Stop “cruising for a bruising”: mitigating bruising in aesthetic medicine. Plast Surg Nurs. 2014;34(2):75–79. quiz 80–81.

2. Hamman MS, et al. Minimizing bruising following fillers and other cosmetic injectables. J Clin Aesthet Dermatol. 2013;6(8):16–18.

3. . Funt D,et al. Dermal fillers in aesthetics: an overview of adverse events and treatment approaches. Clin Cosmet Investig Dermatol. 2013;6:295–316.

4. Martyn King, MD, et al. The Management of Bruising following Nonsurgical Cosmetic Treatment. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5367875/

5. Leu S, et al. Accelerated resolution of laser-induced bruising with topical 20% arnica: a rater-blinded randomized controlled trial [Abstract]. DOI: 10.1111/j.1365-2133.2010.09813.x

6. Mayo Clinic. Bruise: first aid. mayoclinic.org/first-aid/first-aid-bruise/basics/art-20056663. Imechukuliwa 06.07.2021

7. Nutrition and pain: specific nutrients and botanicals. mayoclinic.org/nutrition-and-pain/art-20208638?pg=2. Imechukuliwa 06.07.2021

8. Rathnavelu V, et al. (2016). Potential role of bromelain in clinical and therapeutic applications. DOI: 10.3892/br.2016.720.

9. Self-care approaches to treating pain.mayoclinic.org/self-care-approaches-to-treating-pain/art-20208634. Imechukuliwa 06.07.2021

10. Shah NS, et al. The effects of topical vitamin K on bruising after laser treatment [Abstract].
ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/12140470. Imechukuliwa 06.07.2021

11. Shenefelt PD. Herbal medicine: biomolecular and clinical aspects (2nd edition). ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK92761/. Imechukuliwa 06.07.2021

12. Staiger C. Comfrey: a clinical overview. ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3491633/. Imechukuliwa 06.07.2021

13. Telang PS. Vitamin C in dermatology. idoj.in/text.asp?2013/4/2/143/110593. Imechukuliwa 06.07.2021

14. Vitamin K [Fact sheet]. ods.od.nih.gov/factsheets/VitaminK-HealthProfessional/. Imechukuliwa 06.07.2021

bottom of page