top of page

Imeandikwa na daktari wa ULYclinic

Jumatano, 8 Aprili 2020

Cortisol

Cortisol

Utangulizi

Ni homoni ya Steroid iliyo kwenye kundi la glucocorticoid, homoni hii huzalishwa na tezi za adreno.
Kazi kuu ya homoni hii kurekebisha uchakataji wa glukosi na kuandaa mwili kupambana na msongo.

Homoni ya cortisol huzalishwa viwandani na hupatikana kama dawa ya hydrocortisone
Homoni hii huzalishwa maeneo gani katika mwili?
Homoni ya cortisol huzalishwa ndani ya mwili wa binadamu katika tezi ya adreno iliyokaa juu ya figo. Tezi ya adreo ina ukuta unaoitwa zona fasciculate, ukuta huu huzalisha homoni hii ya cortisol.
Unapokuwa na msongo wa mawazo, homoni hii huzalishwa kwa wingi ili kukusaidia kukabiliana na hali hiyo na pia hutumika kudhibiti hali ya mtu tabia na kuhamasisha.

Jinsi inavyozalishwa:

Homoni ya cortisol huzalishwa na tezi ya adreno kwenye sehemu inayoitwa zona fasciculata
Kuzalishwa kwa cortisol hutegemea maagizo kutoka kwenye tezi ya haipothalamus ambayo humtuma homoni ya corticotropin releasing homoni kwenda kutoa taarifa sehemu ya mbele ya tezi ya pituitari. Tezi ya pituitary baada ya kupata kuweza kutoa homoni inayoitwa adrenocorticotropic ambayo kupitia damu hubebwa na kuja kwenye adrenal cortex ambapo husaidia katika kutengenezwa kwa homoni ya cortisol na glucocorticoid zingine

Kazi za homoni ya cortisol
• Kusaidia mwili kumeng'enya wanga, mafuta na protini
• Husaidia kupunguza uvimbe kwa mtu aliyeumia
• Hurekebisha shinikizo la damu
• Huongeza glukosi kwenye damu kwa kusabababisha ogani zingine zitengenezee sukari na kuzuia matumizi ya sukari kwenye sehemu zingine za mwili
• Kusaidia kuthibiti usingizi
• Huongeza nguvu ili kuweza kupambana na msongo wa mawazo
• Hupunguza utengenezwaji wa mifupa na kuifanya kuwa dhaifu
• Hupandisha kiasi cha amino asidi kuwa juu kwa kuzuia kutengenezwa kwa collagen na kuzuia amino asidi kujikusanya kwenye misuli
• Hudhibiti kiasi cha elekrolaiti mwilini kwa kuongeza kiasi ya uchujaji kwenye figo
• Husaidia kufyozwa kwa madini ya sodiam kwenye utumbo mwembamba
• Huhamasisha uzalishaji wa tindikali tumboni
• Hufanya kazi na homoni ya adrenaline kuweza kutunza kumbukumbu za muda mfupi za kihisia
• Husaidia mtu kupambana na msongo wa mawazo
• Wakati wa ujauzito humwezesha mtoto kutengeneza homoni ya cortisol kati ya wiki 30 hadi 32 pia huchochea ukuaji wa mapafu ya mtoto



Kiasi cha cortisol kinapokuwa juu:

Hupelekea kupata sindromus ya kushing ambayo huambatana na uzito mkubwa kupita kiasi (obeziti) ,kupata michubuko kiurahisi ,udhaifu kwenye misuli na kupanda kwa kwiango cha glukosi kwenye damu pia hupelekea ubongo usifanye kazi vizuri na kuchoka

Kiasi cha cortisol kinapokuwa chini :

• Hupelekea kupata ugonjwa wa Addison, ugonjwa huu huambatana na kubadilika kwa ngozi ,kuchoka muda mrefu ,udhaifu wa misuli ,kuhara ,kichefuchefu na kutapika, kukosa hamu ha kula na presha kushuk.


Vitu vya kufanya ili kuweza kuthibiti kiasi cha cortisol mwilini :

• Pata muda wa kutosha wa kulala
• Fanya mazoezi
• Pata kujitambua unapokuwa na msongo wa mawazo ili uweze kuthibiti msongo
• Jifunze kupumzika
• Kuwa na furaha
• Kuwa na mahusiano mazuri na watu wengine
• Kula mlo wa afya njema kama matunda mengi na kunywa maji mengi

ULY CLINIC inakushauri uwasiliana na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Kwa ushauri zaidi na tiba unaweza kuwasialiana na daktari wa ULY CLINIC kupitia linki ya 'mawasialiano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

9 Aprili 2020 04:38:36

Rejea za mada hii;

bottom of page