Mwandishi;
Mhariri:
Jaza jina na cheo cha mwandishi
Alhamisi, 31 Desemba 2020
Asthma-(pumu ya kifua)-Huduma ya kwanza
Pumu ya kifua (asthma) ni tatizo sugu la mfumo wa hewa linalotishia maisha. Mtu anaposhikwa na pumu mirija ya njia ya hewa husinyaa na hivyo kusabaisha hewa kutopita vema na kuingia kwenye damu. Hii husababisha kuonekana kwa dalili ya kifua kubana, hata hivyo kubana kwa njia ya hewa hupelekea kufanyika kwa uteute mwingi ambao pia huziba njia ya hewa na kupelekea dalili ya kushindwa kupumua kuwa kali zaidi. Mara nyingi asthma hutokea sana utotoni kwa sababu mfumo wa hewa huwa na mwitikio mkali kwenye mabadiliko ya mazingira na viamsha aleji kutoka kwenye mazingira.
Vitu vinavyoamsha pumu
Poleni za maua
Uchafuzi wa hewa
Kubadilika kwa joto
Mazoezi
Namna tatizo linavyotokea
Mfumo wa mapafu unapokutana na viasha aleji hivi kwenye mazingira husababisha mfumo wa hewa kuitikia kwa kuzalisha kemikali ambazo husababisha kuvimba na kutengeneza kwa uteute mwingi kwenye mirija ya hewa
Dalili za mshiko wa asthma
Kutoa sauti za miruzi
Kupumua kwa shida
Kuhisi kifua kizito
Kuongezeka kwa mapigo ua moyo na mishipa ya damu
Kupata shida ya kupumua hewa nje
Kipindi cha mshiko wa asthma, mhanga anaweza kuishiwa nguvu kutokana na kutumia nguvu kupumua hivyo anaweza kupoteza fahamu, ngozi kubadilika rangi kuwa kama blue nyeusi haswa kwenye maeneo ya midomo, macho nan cha za vidole vya mikono. Dalili hizi humaanisha mshiko mkali wa astha.
Namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa mwenye mshiko wa asthma
Msaidie mgonjwa akae kwenye pozi ambalo linamfanya apumue vema
Msaidi mgonjwa kutumia dawa zake za asthma haswa dawa ya kupuliza kwenye njia ya hewa
Mtie moyo na hakikisha unakagua viashiria vy uhai
Piga simu haraka iwezekanavyo kwa watoa huduma ya dharura namba 112 endapo
Hakuna mabadiliko yoyote baada ya kutumia dawa ya asthma ya kupulizia mdomoni
Mhanga hana dawa za asthma
Unahofu kuhusu hali kali ya asthma
Usichelewe kutoa taarifa endapo unahofu kuhusu mhanga, hii ni kwa sababu mhanga huhitaji matibabu ya haraka ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea hivyo piga simu kwa huduma za dharura haraka Zaidi.
Namna dawa ya kupuliza ya asthma inavyofanya kazi
Wagonjwa wa athma kwa kawaida hutakiwa kutembea na dawa ya kupuliza(inhaler) ili endapo tatizo litatokea watumie dawa hiyo haraka iwezekanavyo. Dawa hii ya kupuliza huwa na kiini cha dawa kinachoitwa salbutamol, salbutamol hupunguza uvimbe na kufungua njia ya hewa hivyo kusababisha mgonjwa apate uahueni. Endapo una hitaji kufahamu Zaidi kuhusu namna ya kutumia dawa hii, soma katika Makala zingine zilizo kwenye blogi ya ulyclinic
ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri zaidi kabla ya kuchukua thatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa suhauri zaidi kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
1 Oktoba 2021 08:12:19
Rejea za mada:
The complete first aid book
British red cross. https://www.redcross.org.uk/first-aid/learn-first-aid/asthma-attack. Imechukuliwa 31.12.2020
Better Health Channel. Asthma emergency first aid. https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/conditionsandtreatments/asthma-emergency-first-aid. Imechukuliwa 31.12.2020
National asthma council. Asthma first aid. https://www.nationalasthma.org.au/asthma-first-aid. Imechukuliwa 31.12.2020