Mwandishi;
Mhariri:
Jaza jina na cheo cha mwandishi
Jumamosi, 23 Januari 2021

Kizunguzungu- Huduma ya kwanza
Makala hii imezungumzia namna ya huduma ya kwanza kwa mtu mwenye kizunguzungu, endapo unataka maelezo zaidi kuhusu kizunguzungu, tembelea kurasa zingine za kizunguzungu kusoma zaidi
Kizunguzungu ni nini
Kizunguzungu ni hisia za kuhisi kichwa kimekuwa chepesi au hisia za kuzimia
Dalili za kizunguzungu
Kushindwa kusimama wima, kuyumbayumba, kuhisi vitu zinazunguka au unazunguka vitu
Kichefuchefu na kutapita au kuhisi kichwa chepesi
Kuona ukungu wakati mwingine unaweza kupata maumivu ya sikio
Huduma ya kwanza kwa mtu mwenye kizunguzungu
Endapo mtu amepata kizunguzungu, fanya hatua zifuatazo ili kumsaidia
Mlaze chini kwenye sehemu salama na ambayo hatapata majeraha endapo amesimama
Mweleze asibadili mkao kwa haraka
Mweleze asizungushe kichwa kwa haraka
Enadpo ameamua kukaa, msaidie kuweka kichwa katikati ya mapata
Endapo kizunguzungu kimeisha, mfundishe kuamka kwa taratibu, angalau atumie dakika 3 kuamka kutoka kwenye mkao wa kulala kwenda kwenye mkao wa kukaa
Wakkati gani wa kupiga namba 112 au kumfikisha hospitali
Mfikishe mgonja hospitali au piga simu kupata msaada wa watoa huduma ya kwanza namba 112 endapo
Ndo mara ya kwanza kupata kizunguzungu
Kuna mabadiliko kwenye uono au kuongea
Maumivu ya kifua
Kuishiwa pumzi
Mapigo ya moyo kubadilika
Degedege au kutapika
Kupata kizunguzungu baada ya kuumizwa kwenye kichwa
Kuona mara mbilimbili
Kuzimia au kupoteza fahamu
Kushindwa kunyanyua kiungo cha mwili
Kuongea kama mlevi
Kupata ganzi na hisia za kuchomachoma
Homa au kukakamaa kwa shingo
Taarifa zaidi napata wapi?
Kizunguzungu endapo kimeambatana na kuzimia huduma ya kwanza hutakiwa tolewa kama kwa mtu ambaye amezimia. Soma kuhusu huduma ya kwanza kwa mtu aliyezimia kwenye Makala nyingine ndani ya tovuti hii
ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri zaidi kabla ya kuchukua thatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa suhauri zaidi kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
1 Oktoba 2021 08:12:17
Rejea za mada:
VERTIGO.https://alscofirstaid.com.au/first-aid-resources/first-aid-how-to/vertigo/. Imechukuliwa 22.01.2021
Mayo clinic. https://www.mayoclinic.org/first-aid/first-aid-fainting/basics/art-20056606. Imechukuliwa 22.01.2021
American Medical Association Handbook of First Aid and Emergency Care, Random House, 2009
Ileok Jung, etal. Approach to dizziness in the emergency department. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5052860/. Imechukuliwa 22.01.2021