top of page

Mwandishi;

Mhariri:

Jaza jina na cheo cha mwandishi

Alhamisi, 31 Desemba 2020

Kushikwa ghafla na hofu na kupumua haraka haraka- Huduma ya kwanza
Kushikwa ghafla na hofu na kupumua haraka haraka- Huduma ya kwanza
Kushikwa ghafla na hofu na kupumua haraka haraka- Huduma ya kwanza
Kushikwa ghafla na hofu na kupumua haraka haraka- Huduma ya kwanza

Kushikwa ghafla na hofu na kupumua haraka haraka- Huduma ya kwanza

Mtu hushikwa na hofu kubwa ya ghafla endapo endapo alikuwa na shauku kuu, hofu hii huambatana na dalili za kimwili ambazo ni kupumua haraka haraka, kutokwa na jasho, mapigo ya moyo kwenda harakaharaka au kuruka na kukakamaa kwa misuli


Kushikwa na hofu kuu ya ghafla huweza kuogopesha sana kwa kuwa hutokea bila taarifa. Dalili zinazotokea zinaweza kupelekea kufanya tatizo la shauku likawa kubwa zaidi na pia kufanya mtu aendelee kuwa na hofu zaidi na dalili kuendelea kuwa nyingi Zaidi.


Kupumua haraka haraka ni dalili kuu ya kushikwa na hofu kuu ya ghafla, endapo tatizo ni kubwa, dalili zingine zinazoletwa na tatizo hili la kupumua haraka haraka huwa ni kupata ganzi au kuhisi mikono na vidole vinachomachoma. Mtu anapata dalili hizo kwa sababu anapopumua haraka haraka huathiri kiwango cha hewa ya kabon dayoksaidi kwenye damu. Tatizo la hofu ya ghafla huchochea shauku kuu na hii huchochea dalili na dalili huchochea hofu na mzunguko unaendelea hivyo na tatizo linakuwa kubwa Zaidi.


Ukiwa unatoa huduma ni vema kufahamu kuwa, kupumua harakaharaka huweza pia kusababishwa na matatizo menfine mfano mshiko wa pumu na mshituko wa moyo hivyo ni vema kujiuliza sababu hizi ambazo huweza kuwa za hatari Zaidi kwa mgonjwa na kupiga simu kwenye kituo cha afya haraka Zaidi unavyoweza ili kupatiwa msaada wa haraka.


Watu wenye tatizo la kushikwa na hodu ya ghafla mara kwa mara wanaweza kuwa wanatumia dawa jamii ya antianxiety na hivyo huweza kuwa amebeba ili kuzitumia wakati wa mshiko.


Dalili


Dalili za hofu ya ghafla huwa pamoja na


  • Mapigo ya moyo kwenda kasi pamoja na kuhisi mapigo ya moyo yanasimama au moyo kuruka pigo

  • Kuishiwa pumzi

  • Kuhisi umekabwa na kitu kooni

  • Kutetemeka, kupata ganzi kwenye ncha za vidole vya mikono na miguu

  • Kutokwa na jasho

  • Kupata hamu ya kwenda haja kubwa

  • Fikra za kufa

  • Kuhisi kupoteza uwezo wa fikra zako au kuchanganyikiwa

  • Kuwa mharibifu


Namna ya kutoa huduma ya kwanza


Fuata maelekezo haya ili kuweza kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyepatwa na hofu ya ghafla na kupumua haraka haraka;


  1. Usipaniki na mpe matumaini mgonjwa ya kupata msaada

  2. Muulize mhanga kama kuna kitu unawez akumsaidia kufanya mfano kuondoa kisabababishi cha hofu

  3. Angalia upumuaji wa mhanga, mwambie avute pumzi kwa kina kirefu Zaidi na taratibu kwa kumwonesha mfano. Hii itapunguzai upumuaji wa haraka haraka na madhara yatokanayo na kupumua huko.

  4. Myie moyo sana mhanga huku ukulinda utu wake mfano hakikisha watazamaji wengine wameondoka kwenye eneo hilo la tukio

  5. Piga simu ya dharura kwa watoa huduma ya dharura endapo mhanga amepoteza fahamu, akiwa anaonekana ana hali kali ya kupumua kwa shida, au endapo unadhani atakuwa na mshiko wa pumu ya kifua(asthma)


Mambo usiyopaswa kufanya


Usitumie mfuko wa plastiki kumfunika mgonjwa ili asipumue haraka haraka kwani inawez akusabaisha kuongezeka kwa kiwango cha kabon monoksaidi kwenye damu na kifo haswa kwa wagonjwa wenye asthma na mshituko wa moyo.

ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri zaidi kabla ya kuchukua thatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa suhauri zaidi kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba'  chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

1 Oktoba 2021, 08:12:22

Rejea za mada:

First Aid for life. Panic Attacks: How to Help. https://firstaidforlife.org.uk/how-to-help-someone-having-a-panic-attack/#. Imechukuliwa 31.12.2020 2. Web MD Panic Attacks Treatment. https://www.webmd.com/first-aid/panic-attacks-treatment. Imechukuliwa 31.12.2020 3.Recovery village. Mental Health First Aid for Panic Attacks. https://www.therecoveryvillage.com/mental-health/first-aid/panic-attacks/ 4. the complete first aid Pocket book

bottom of page