top of page

Mwandishi;

Mhariri:

Jaza jina na cheo cha mwandishi

Jumatatu, 5 Aprili 2021

Kushuka kwa sukari- Huduma ya kwanza
Kushuka kwa sukari- Huduma ya kwanza
Kushuka kwa sukari- Huduma ya kwanza
Kushuka kwa sukari- Huduma ya kwanza

Kushuka kwa sukari- Huduma ya kwanza

Kushuka kwa kiwango cha sukari kwenye damu (au kuishiwa na sukari mwilini) hufahamika kwa neno la kitatibu kama “hypoglycemia” humaanisha maana ya kupungua kwa kiwango cha sukari kwenye damu kuliko kawaida.


Kutokana na sababu mbali mbali, ni kawaida kwa kiwango cha sukari katika damu hupanda na hushuka kwa siku nzima, ingawa si rahisi kugundua kwa kuwa mabadiliko hayo hayana mashiko. Hata hivyo, kiwango cha sukari kinaposhuka chini ya miligramu 70 kwa kila desilita (70mg/dl) au uniti ya millimoles 3.9 kwa kwa lita (3.9mmol/L) kwa mujibu wa kipimo cha sukari, dalili huonekana na tatizo hili lisipochukuliwa hatua huleta madhara makubwa hata kupelekea kifo.


Kushuka kwa sukari si ugonjwa bali ni ishara ya tatizo fulani la kiafya ndani ya mwili, na dalili hii hutokea mara chache kwa watu wazima na watoto walio na umri wa zaidi ya miaka 10, na mara nyingi huwapata watu wenye kisukari aina ya kwanza.


Mambo ya kufanya kwa mtu aliyeishiwa sukari mwilini


Mambo ya kufanya hutegemea dalili za mtu, kuna dalili za awali na dalili za hatari. Fanya yafuatayo unapokua na mtu mwenye shida ya kushuka kwa sukari.


Mambo ya kufanya kupandisha sukari kwa mtu mwenye dalili za awali

Endapo dalili zimeaza kuonekana, mpatie mwathirika moja ya vitu hivi kwa haraka


  • Vidonge au maji yenye glukosi

  • Sukari

  • Asali

  • Pipi

  • Soda

  • Glasi ya juisi ya matunda yenye sukari nyingi


Kwa mtu mwenye kisukari unapaswa kumpima kiwango cha sukari kwa kutumia glucometer na kisha kufanya kama ilivyoainishwa hapo juu, kisha subiri kwa dakika 15-20 na upime tena kiwango cha sukari. Endapo kiwango cha sukari bado kipo chini mpatie tena vitu vyenye sukari nyingi, subiri tena kwa muda wa dakika 15-20 na upime tena. Fanya hivi mpaka kiwango cha sukari kitakapofika 70-180 mg/dl (3.9-10.0mmol/dL)


Mambo ya kufanya kwa mtu mwenye dalili za hatari za kushuka kwa sukari

Kwa mtu mwenye dalili za hatari za kushuka kwa sukari fanya yafuatayo;


  • Muwekee asali au sukari ndani ya mashavu, kisha kanda kanda nje ya mashavu. Atajihisi vema baada ya dakika 10-20

  • Ikiwa amepotea fahamu au anapata degedege piga namba ya simu ya dharura (112) kuomba msaada wa huduma za dharura na epuka kumuwekea kitu chochote mdomoni


Mambo ya kufanya kuzuia kuishiwa sukari mwilini


Kwa mtu ambaye yuko katika hatari ya kupata tatizo la kushuka kwa sukari, na hasa mgonjwa wa kisukari unashauriwa kufanya mambo yafuatayo,


  • Kula kidogo kidogo na mara nyingi , walau mara tatu kwa siku

  • Kula vyakula vyenye wanga usiokobolewa

  • Wasiliana na daktari wake kuhusu dawa za kisukari unazotumia

  • Kupima kiwango cha sukari mara kwa mara

  • Kuepuka kunywa pombe bila kula

  • Kutembea na chakula cha tahadhari

  • Pima kiwango chako cha sukari na kula pale ambapo kiwango cha sukari kipo chini

  • Kula chakula cha wanga kabla ya kufanya mazoezi


Kumbuka

  • Dalili za kushuka kwa sukari hufanana na dalili za magonjwa mengine

  • Njia pekee ya kuwa na uhakika kama dalili za kushuka kwa sukari ni kupima kiwango cha sukari katika damu. Kama huna kifaa cha kupima sukari basi msaidie mwathirika kama ilivyoainishwa hapo juu. Ukiona dalili zinaendelea baada ya huduma ya kwanza, wasiliana na huduma za dharura kwa kupiga simu haraka iwezekanavyo.

ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri zaidi kabla ya kuchukua thatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa suhauri zaidi kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba'  chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

1 Oktoba 2021 08:12:11

Rejea za mada:

  1. Hypoglycemia in Adults. https://www.reliasmedia.com/articles/78107-hypoglycemia-in-adults. Imechukuliwa 05.04.2021

  2. Low Blood Sugar (Hypoglycemia). https://www.healthline.com/health/hypoglycemia#symptoms. Imechukuliwa 05.04.2021

  3. American diabetes association. Hypoglycemia (Low Blood sugar). https://www.diabetes.org/healthy-living/medication-treatments/blood-glucose-testing-and-control/hypoglycemia. Imechukuliwa 05.04.2021

  4. All about hypoglycemia (low blood sugar). https://www.medicalnewstoday.com/articles/166815#takeaway. Imechukuliwa 05.04.2021

  5. Blood Sugar Level Ranges. https://www.diabetes.co.uk/diabetes_care/blood-sugar-level-ranges.html. Imechukuliwa 05.04.2021

  6. Learn first aid for someone who is having a diabetic emergency . https://www.redcross.org.uk/first-aid/learn-first-aid/diabetic-emergency. Imechukuliwa 05.04.2021

  7. Hypoglycemia in adults without diabetes mellitus: Clinical manifestations, diagnosis, and causes. https://www.uptodate.com/contents/hypoglycemia-in-adults-without-diabetes-mellitus-clinical-manifestations-diagnosis-and-causes#H22. Imechukuliwa 05.04.2021

  8. Centre for disease control and prevention. Manage Blood Sugar. https://www.cdc.gov/diabetes/managing/manage-blood-sugar.html. Imechukuliwa 05.04.2021

  9. M L Virally, et al. Hypoglycemia in adults. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/10633872/. Imechukuliwa 05.04.2021

bottom of page