Mwandishi;
Mhariri:
Jaza jina na cheo cha mwandishi
Jumatano, 30 Juni 2021
Kutapika safarini
Kutapika wakati wa kusafiri ni sindromu inayotokea mtu anapokuwa kwenye mwendo aina Fulani na mara nyingi huisha mara mwendo unaisha na hutokea sana wakati wa kusafiri. Ingawa kichefuchefu ndo dalili kuu, uchomvu na dalili kali zaidi zinaweza kuambatana
Kuzuia Kutapika safarini
Mara nyingi kutapita safarini huanza ghafla na dalili ya kujihisi vibaya kisha kutokwa na jasho ikifuatiwa na kizunguzungu na baadae kutapika. Kuwa na tatizo hili na kufahamu njia za kujikinga au kufanya itasaidia kujiandaa kabla ya safari. Makala hii imeelezea namna ya kuzuia na kudhibiti kutapika ukiwa safarini.
Mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza safari ili kuzuia kutapika
Kabla ya kuanza safari hakikisha unakaa siti ya mbele au siti ambayo hutaona vitu vya nje kuwa vinatembea au kukaa siti yenye mitikisiko mikubwa na kufanya mambo yanayofuata;
Kama utasafiri kwa meli, chagua siti ya mbele au katikati ya meli
Kama utasafiri kwa ndege chagua siti karibu na bawa la mbele la ndege
Kama utasafiri kwa treni chagua siti ya karibu na mbele au kaa karibu na dilisha
Kama utasafiri kwa gali, endesha gari au kaa siti ya mbele kabisa
Kunywa dawa jamii ya antihistamine dakika 30 au 60 kabla ya safari ( mfano wa dawa ni dimenhydrinate au meclizine). Hakikisha unawasiliana na daktari wako kama ni salama kwako.
Unaweza kutumia pia scopolamine ya kubandika kwenye ngozi
Epuka kupanga safari wakati wa hali ya hewa mbaya au kutumia usafiri
Usile mlo mkubwa kabla ya safari na usisafiri bila kula chochote haswa vitu vikavu
Mambo ya kufanya baada ya safari kuanza ili kuzuia kutapika
Jikite kutazama anga badala ya vitu vya nje vinavyoonekana kuwa vinatembea
Acha kusoma au kutumia vitu vya kielekronia kama simu n.k
Egamisha kichwa na mgongo kwenye kiti na zuia mtikisiko mkubwa kwenye kichwa
Endesha gari mwenyewe au kama huendeshi na umepanga kuwa macho kuinamisha kichwa gari inapokunja kona
Fumba macho wakati wa safari endapo huwezo kukaa kwenye siti ya mbele au vaa miwani ya jua au lala huku umefumba macho unapokuwa safari
Epuka kuvuta sigara au kutumia kemikali ya nicotine kabla ya kusafiri
Acha vitu vyenye harufu kali
Jaribu kutumika tangawizi au vyakula vilivyotiwa tangawizi kwani huzui kichefuchefu
Kula chakula kikavu kabla na ukiwa unasafiri kama vile popcorn. Kama una kiu, tumia maji ya baridi au vinywaji visivyo na kahawa
Epuka kula vitu vyenye tindikali na vyenye sukari au mafuta kwa wingi
Sikiliza mziki mzuri utakao kustaheresha
ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri zaidi kabla ya kuchukua thatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa suhauri zaidi kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
1 Oktoba 2021 08:12:05
Rejea za mada:
Andrew Brainard, MD, MPH, et al. Prevention and Treatment of Motion Sickness. https://www.aafp.org/afp/2014/0701/p41.html. Imekuliwa 30.06.2021
American Academy of Otolaryngology-Head and Neck Surgery .Dizziness and motion sickness.. http://www.entnet.org/content/dizziness-and-motion-sickness. Imekuliwa 30.06.2021
Priesol AJ. Motion sickness. https://www.uptodate.com/content/search. Accessed July 29, 2017.
Brunette GW, et al. CDC Health Information for International Travel 2018. New York, N.Y.: Oxford University Press; 2017. https://wwwnc.cdc.gov/travel/page/yellowbook-home. Imekuliwa 30.06.2021
Transderm Scop (prescribing information). http://www.transdermscop.com/prescribing-information.htm. Imekuliwa 30.06.2021
Scopolamine. https://www.rxlist.com/consumer_scopolamine/drugs-condition.htm. Imekuliwa 30.06.2021 7. Veronica Takov, et al. Motion Sickness. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK539706/#. Imekuliwa 30.06.2021