Mwandishi;
Mhariri:
Jaza jina na cheo cha mwandishi
Dkt. Sospeter B, MD
Ijumaa, 30 Juni 2023
Maumivu ya koo huduma ya kwanza
Maumivu ya koo ni hali ya kupata hisia za kukwaruza, kukereketa, muwasho au maumivu ambayo mara nyingi huongezeka wakati wa kumeza.
Kisababishi kikuu cha maumivu ya koo ni michomo kwenye koo inayosababishwa na maambukizi ya virusi kama vile kirusi cha mafua au homa ya baridi.
Maumivu ya koo yanayosababishwa na virusi huisha yenyewe baada ya muda, wakati yale yanayosabaishwa na bakteria huhitaji matibabu ya dawa ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea. Visababishi vingine vinaweza kuhitaji matibabu tata ambayo hutolewa hospitali.
Unapaswa kufahamu kisabaishi cha maumivu ya koo kwanza kabla ya kuanza kujitibu mwenyewe nyumbani, endapo utafanya huduma ya kwanza nyumbani, hakikisha unafika hospitali kwa uchunguzi ili upate matibabu sahihi.
Matibabu ya nyumbani ya maumivu ya koo
Bila kuzingatia kisababishi, maumivu ya koo yanaweza kutibiwa nyumbani ili kupunguza dalili kwa kufanya mambo yafuatayo:
Kupumzika vya kutosha.
Kwa kulala muda wa kutosha angalau masaa nane kwa usiku na kuacha kutumia koo kuongea sana au kuimba.
Kunywa maji ya kutosha
Maji hufanya koo liwe na unyevu wa kutosha na hivyo kulainika na kupunguza maumivu. Unaweza kutumia maji ya uvuguvugu pia kwa matokeo mazuri.
Vilevi na pombe
Kuacha kutumia kilevi na vinywaji vyenye kafeini ambavyo hukausha koo na kufanya dalili kuwa kali Zaidi.
Tumia vinywaji na vyakula vinavyotuliza koo
Tumia maji ya vuguvugu yenye asali isiyo na kafeini au kuweka vipande vya barafu kwenye koo kupunguza maumivu ya koo. Asali isitumike kwa mtoto chini yam waka 1.
Sukutua kwa maji chumvi au magani
Maji ya Magadi au chumvi husaidia kupunguza maumivu ya koo. Unaweza kutumia robo ya kijiko cha chai hasi nusu yake kwa kuweka kwenye maji ya glasi 1 ya maji ya kunywa yenye ujazo wa mililita 240
Watoto zaidi ya miaka 6 na watu wazima wanaweza kusukutua kwa maji haya na si walio chini ya umri huu.
Ongeza unyevu kwenye hewa
Kama hew ani kavu, utawapa maumivu ya koo kw akuvuta hewahiyo kavu, unaweza kutumia kifaa cha kuongeza unyevu kwenye unyevu ina kuruhusu hewa hiyo kuingia katika koo kwa kukaa dakika chache kwenye mvuke wake.
Tumia dawa ya kulainisha koo
Watoto wadogo chini ya miaka minne hawapaswi kutumia dawa aina hizi.
Epuka vikereketa koo
Epuka vikereketa koo kama vile sigara, kemikali za kufanyia usafi na kemikali zingine zinazokereketa koo.
Pumzika nyumbani mpaka utakapopona
Kufanya hivi kutazuia watu wengine kuambukizwa homa ya virusi vya mafua au baridi.
ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri zaidi kabla ya kuchukua thatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa suhauri zaidi kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
30 Juni 2023 18:40:59
Rejea za mada:
Sore throats. American Academy of Otolaryngology — Head and Neck Surgery. http://www.entnet.org/content/sore-throats. Imechukuliwa 30.06.2023
Sore throat. Merck Manual Professional Version. http://www.merckmanuals.com/professional/ear,-nose,-and-throat-disorders/approach-to-the-patient-with-nasal-and-pharyngeal-symptoms/sore-throat. Imechukuliwa 30.06.2023
Seven tips to help you prevent a sore throat. American Academy of Otolaryngology — Head and Neck Surgery. https://www.enthealth.org/be_ent_smart/seven-tips-to-help-you-prevent-a-sore-throat/. Imechukuliwa 30.06.2023
Sore throat. Centers for Disease Control and Prevention. http://www.cdc.gov/getsmart/community/for-patients/common-illnesses/sore-throat. Imechukuliwa 30.06.2023
Drutz, JE. Sore throat in children and adolescents: Symptomatic treatment. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 30.06.2023
Stead W. Symptomatic treatment of acute pharyngitis in adults. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 30.06.2023
Slippery Elm. Natural Medicines. https://naturalmedicines.therapeuticresearch.com. Imechukuliwa 30.06.2023
Taking care of your voice. National Institute on Deafness and Other Communication Disorders. http://www.nidcd.nih.gov/health/voice/pages/takingcare.aspx. Imechukuliwa 30.06.2023
Chow AW, et al. Evaluation of acute pharyngitis in adults. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 30.06.2023
Kellerman RD, et al. Pharyngitis. In: Conn's Current Therapy 2019. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2019. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 30.06.2023