top of page

Mwandishi;

Mhariri:

Jaza jina na cheo cha mwandishi

Jumanne, 23 Machi 2021

Mshituko wa moyo- Huduma ya kwanza
Mshituko wa moyo- Huduma ya kwanza
Mshituko wa moyo- Huduma ya kwanza
Mshituko wa moyo- Huduma ya kwanza

Mshituko wa moyo- Huduma ya kwanza

Moyo ni ogani yenye misuli laini, yenye uwezo wa kujienedsha yenyewe. Misuli hii inapofanya kazi kwa kusinyaa na kutanuka, husukuma damu kutoka kwenda maeneo mbalimbali ya mwili kupitia mishipa ya damu, ikiwa pamoja na moyo wenyewe. Kama tunavyofahamu, moyo nao huishi kwa kutumia nishati itokanayo na glukosi na hewa ya oksjeni kutoka kwneye mapafu, endapo moyo utakosa vitu hivi basi utashindwa kufanya kazi yake. Glukosi na hewa safi huingia kwenye moyo kupitia mishipa midogo yenye jina la koronari arteri, mishipa hii inapoziba, dalili za mshituko wa moyo hutokea.


Kwanini mshituko wa moyo hutokea?


Jinsi umri unavyokwenda, mafuta tunayokula kutoka kwenye chakula, haswa yale yenye lehamu kwa wingi, huganda katika kuta za ndani ya mishipa ya damu taratibu. Mafuta yaliyoganda yanaweza kukua kwa kimo na pia kunyofonya damu inapokuwa inapita. Bonge la mafuta lilolonyofoka kutoka kwenye mafuta yaliyoganda, husafiri kwenye mishipa ya damu, inapofika kwenye mishipa midogo kwa kuwa huwa na kipenyo kidogo, mishipa hiyo huziba. Kuziba kwa mishipa ya damu ya moyo hupelekea sehemu ya mbele inayolishwa na mshipa huo kukosa chakula na hivyo kufa, inapokuwa inakufa hutoa kemikali mbalimbali kwenye damu zinazoamsha dalili na kufanya kuonekana kwa dalili za mshituko wa moyo.


Mtu akipata mshituko wa moyo anatakiwa kupewa matibabu ya haraka iwezekanavyo kuzibua mishipa iliyoziba na kuzuia uharibifu kutokea katika sehemu kubwa ya moyo.


Dalili za mshituko wa moyo

Kama mgonjwa ana dalili zifuatazo, hiyo ni ishara ya kuwa na mshituko wa moyo;


  1. Maumivu ya kifua yanayosambaa kwenye taya, mikono, mgongo au tumboni

  2. Kizunguzungu, kuhisi kichwa chepesi au kuzimia

  3. Kuishiwa pumzi

  4. Kupata ganzi kwenye mikono au vidole mara nyingi mkono wa kushoto

  5. Kutokwa jasho jingi

  6. Kuongezeka kwa mapigo ya moyo na upumuaji wa haraka

  7. Kichefuchefu na kutapika

  8. Ngozi kupauka

  9. Uchovu mkali na haswa kwa watu wa makamo


Sifa za maumivu ya kifua kutokana na mshituko wa moyo


Maumivu haya huelezewa kwa namna tofauti na kila mgonjwa, hata hivyo wagonjwa wengi huelezea maumivu hayo huwa ya kuchana chana katikati ya kifua.


Huduma ya kwanza kwa mhanga wa mshituko wa moyo

Piga namba 112 simu ya huduma ya dharura kutoa taarifa


  1. Mtulize mgonjwa kwenye pozi la utulivu

  2. Muulize mgonjwa kama anazo na huwa anatumia nitroglycerin kisha umpatie anywe kwa dozi anayotumia

  3. Mpatie kidonge cha aspirin miligramu 325 kama inaruhusiwa( angalia maelezo chini kinanani wanaruhusiwa)

  4. Legeza nguo zilizobana shingo au mwili na hakikisha anapata hewa ya kutosha

  5. Kama mgonjwa amepoteza fahamu, uwe tayari kufanya CPR (soma katika Makala zingine za ULY CLINIC namna ya kufanya CPR).

  6. Mpe matumaini mgonjwa na hakikisha unampima kwa muda viashiria vya uhai utakavyoripoti kwa mtoa huduma ya dharura atakapowasili


Kwanini umpatie wa mgonjwa wa mshituko wa moyo aspirini?


Aspirini imeonyesha kusaidia sana wagonjwa wenye mshituko wa moyo kwa kuyeyusha bonge la damu lililoganda na kuziba mishipa ya damu ya moyo. Endapo mgonjwa amepatwa na mshituko wa moyo ni vema ukampatia aspirini mara moja atafune kisha kumeza ili kumsaidia kutopata madhara makubwa.

Baadhi ya wagonjwa hawapaswi kutumia aspirini kama wale wenye mzio na dawa hii pamoja na wale wenye hitosria ya ugonjwa wa kutokwa na damu.



Wapi unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu mshituko wa moyo?


Kupata maelezo zaidi ya mshituko wa moyo na namna ya kujikinga, ingia kwenye Makala zingine ndnai ya tovuti hii kusoma zaidi.

ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri zaidi kabla ya kuchukua thatua yoyote baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa suhauri zaidi kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba'  chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

1 Oktoba 2021 08:12:11

Rejea za mada:

  1. Hani Jneid, et al. 2012 ACCF/AHA focused update of the guideline for the management of patients with unstable angina/non-ST-elevation myocardial infarction (updating the 2007 guideline and replacing the 2011 focused update): a report of the American College of Cardiology Foundation/American Heart Association Task Force on Practice Guidelines.https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/22809746/. Imechukuliwa 23.03.2021

  2. AHA. Warning signs of a heart attack. https://www.heart.org/en/health-topics/heart-attack/warning-signs-of-a-heart-attack. Imechukuliwa 23.03.2021

  3. National Heart, Lung, and Blood Institute .Heart attack. https://www.nhlbi.nih.gov/health-topics/heart-attack#. Imechukuliwa 23.03.2021

  4. ST john ambulance. Heart attack. https://www.sja.org.uk/get-advice/first-aid-advice/heart-conditions/heart-attack/. Imechukuliwa 23.03.2021

  5. Heart attack first aid Information.Mount Sinai - New York.https://www.mountsinai.org/health-library/injury/heart-attack-first-aid. Imechukuliwa 23.03.2021

bottom of page