top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeandikwa:

Dkt. Adolf S, MD

Dkt. Sospeter M, MD

23 Septemba 2022 05:35:32

Augumentin

Ni jina la kibiashara la dawa inayotumika kutibu maradhi ya bakteria yenye muunganiko wa dawa mbili za Amoxicilin na clavulanate potassium. Dawa hii hutumika kutibu maambukizi mbali mbali mwilini yanayosababishwa na bakteria


Uzito wa Augmentin


Dawa hii hupatikana katika fomu ya vidonge na dawa ya unga ambayo huchanganywa na maji kupata dawa ya maji katika uzito ufuatao


Vidonge

  • 250 mg/125 mg (amoxcilin miligramu 250 na clavulanate potassium miligramu 125)

  • 500 mg/125 mg (amoxcilin miligramu 500 na clavulanate potassium miligramu 125)

  • 875 mg/125 mg (amoxcilin miligramu 875 na clavulanate potassium miligramu 125)

  • 1000 mg/62.5 mg (amoxcilin miligramu 1000 na clavulanate potassium miligramu 125)

  • 200 mg/28.5 mg (amoxcilin miligramu 200 na clavulanate potassium miligramu 28.5)

  • 400 mg/57 mg (amoxcilin miligramu 400 na clavulanate potassium miligramu 57)


Dawa ya maji

  • (200 mg/28.5 mg/)5 ml - amoxcilin miligramu 200 na clavulanate potassium miligramu 28.5, katika ujazo wa mililita 5

  • (250 mg/62.5 mg/)5ml- amoxcilin miligramu 250 na clavulanate potassium miligramu 62.5, katika ujazo wa mililita 5

  • (400 mg/57 mg/)/5ml- amoxcilin miligramu 400 na clavulanate potassium miligramu 57, katika ujazo wa mililita 5

  • (600 mg/42.9 mg)/5ml- amoxcilin miligramu 600 na clavulanate potassium miligramu 42.9, katika ujazo wa mililita 5


Wapi unaweza kupata maelezo zaidi?


Kupata maelezo zaidi kuhusu Augmentin/amoxiclav soma mada inayohusiana na amoxiclav


Majina mengine ya kibiashara ya Augmentin


Yafuatayo ni majina mengine ya kibiashara ambayo humaanisha amoxcilin/clavulanate potassium ni:


  • Augmentin XR

  • Augmentin ES-600

  • Cledomox

Uly clinic inakushauri siku zote wasiliana na daktari wako kwa ushauri wa matumizi ya dawa yoyote. Usitumie dawa bila kushauriwa na daktari ili kuepuka madhara na kufanya vimelea kuwa sugu kwenye dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia linki ya 'Pata tiba' au 'Wasiliana nasi' chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii:

  1. Amoxicillin-potassium-clavulanate .https://www.medopharm.com/radiant/cledomox-625-amoxicillin-potassium-clavulanate-tablets/. Imechukuliwa 23.09.2022

  2. Amoxicillin-potassium-clavulanate. https://www.drugs.com/search.php?searchterm=amoxicillin%2Fclavulanate&a=1. Imechukuliwa 23.09.2022

  3. Amoxicillin clavulanate . https://www.drugs.com/amoxicillin_clavulanate.html. Imechukuliwa 23.09.2022

  4. Augumentin. https://reference.medscape.com/drug/augmentin-amoxicillin-clavulanate-342474. Imechukuliwa 23.09.2022

Imeboreshwa:

27 Septemba 2022 16:53:18

bottom of page