top of page

Boneyeza kusoma zaidi makala zingine hapa

Afya ya mama na mtoto

Mwandishi: Daktari wa ULY CLINIC

Je kuna njia ya kufanya ili kuchagua jinsia ya mtoto?

Jibu la kifupi ni hapana- Hakuna  jambo ama utaratibu fulani wandoa wanaweza kufanya ili kupata mtoto wa jinsia wanayotaka.

 

Ingawa inasemekana kuna baadhi ya mambo ya kufanya yanayoweza kushawishi ama kupelekea kupata jinsia ya kike ama ya kiume. Kabla ya hapo kwanza unatakiwa kujua kuhusu nini kinatokea hadi mtoto anatengenezwa wa kike ama wa kiume. 

 

Kwa kifupi Yai la kike na mbegu ya kiume lazima viungane ili kutengeneza mtoto, mbegu ya kiume huweza kuwa ina X ama Y sasa  tuone sifa za mbegu  X na Y

 

Mbegu yenye Y- huwa na mwendo kasi mkali ,huwa na hifadhi ya nguvu kidogo na huishi masaa machache

mbegu yenye X huwa na mwendo kasi wa taratibu, huwa na hifadhi ya nguvu nyingi na huweza kuishi masaa mengi

 

Mbegu Y ikikutana na yai huleta mtoto wa kiume na mbegu X vilevile ikikutana na yai huleta mtoto wa Kike. Kutokana na sifa zilizotajwa hapo juu inasemekana  kwamba (maana hakuna utafiti wa kisayansi ulioonyesha hili) endapo wanandoa watashiriki tendo la ndoa siku 3 kabla ya yai kutoka, kunauwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa kike kwa sababu mbegu Y zote zitakuwa zimeshakufa yai linapotoka kwa sababu zilikuwa na hifadhi ya nguvu kidogo na hivyo mbegu X ndo zitakuwepo bado hai kwa ajiri ya uchavushaji.

 

Vivyo hivyo wanandoa wakishiriki siku ya yai kutoka basi ni kwamba watapata mtoto wa kiume kwa sababu mbegu Y huwa na kasi kali kuliko X na itatangulia kufika na kuchavusha yai mapema zaidi

 

Unawezaje kujua siku yako ya yai kutoka?

 

Kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28 ni dhahili kwamba siku ya 14 ndipo yai lake litakuwa limeanguliwa kiwandani na kuingia katika mirija ya uzazi tayari kwa uchavushwaji. Lakini kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35, siku ya 21 ndo siku ambayo yai la kike litatoka kwenye kiwanda na kuingia katika mirija ya uzazi

 

Hivyo kwa kupata ntoto wa kike kwa mwanamke mwenye siku 35, anaweza kujaribu kushiriki tendo la ndoa siku mbili ama tatu kabla yaani siku ya 19 ya mzunguko toka alipoanza kuona damu ya hedhi. hivyo hivyo mwenye mzunguko wa siku 28 anatakiwa kushiriki siku ya 12

 

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri juu ya afya yako siku zote kabla ya kuchukua hatua inayohusu afya yako.

Wasiliana na daktari wa ULY CLinic kwa kutumia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa mara ya mwisho, 01.07.2020

Rejea za mada hii,

  1. WebMD.https://www.webmd.com/baby/features/choosing-sex-of-your-child#1. Imechukuliwa 01.07.2020

  2. Gender selection. https://www.fertility-docs.com/programs-and-services/gender-selection/select-the-gender-of-your-baby-using-pgd.php Imechukuliwa 01.07.2020

  3. CNBC.https://www.cnbc.com/2018/08/04/fertility-clinics-advertise-gender-selection-ethical-wuandary.html. IMechukuliwa 01.07.2020

Kuchagua Jinsia ya mtoto
bottom of page