top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Novemba 2026, 15:48:56

Akalazia (achalasia)

Akalazia (achalasia)

Majina mengine: achalasia (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa


Maana: hitilafu ya neva na misuli ya umio inayozuia chakula kupita kwenda tumboni.


Maelezo zaidi


  • Dalili: kumeza kwa shida vyakula vigumu na vya maji, chakula kurudi mdomoni bila kumeng'enywa, maumivu ya kifua, kupungua uzito, kukohoa usiku.

  • Hutambuliwa kwa X-ray ya kumeza dawa maalum (barium), kipimo cha shinikizo la umio, na endoscopy.

  • Matibabu: kupanua mlango wa chini wa umio kwa puto, upasuaji, au dawa.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Kumeza kwa shida kunakoendelea au kuongezeka, au kupungua uzito – hasa kwa mtu mzima.

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page